Wakuu mwaka unaelekea ukingoni na ni wakati wa kujitathmini. Mi napenda tujitatmnini juu ya vitabu tulivyosoma mwaka huu kama ilivyo desturiyetu ya kila mwaka. Mimi nimesoma vifuatavyo.
MOSSAD: kimeandikwa na Nissim Mishal na Michael Bar-Zohar. Hiki kitabu kinazungumzia missions kubwa kuwahi kufanywa na shirika la kiijasusi la Israel (Mossad). Toka kukamatwa kwa wanazi walioua wayahudi, kupambana na waarabu, kupambana na "magaidi" , na hadi leo wanavyopambana na jitihada za Iran kuwa nuclear power. Ni kama novel ya kijasusi tofauti ni kwamba haya yalitukia kweli.
THE DARK SIDE OF NYERERE: kimeandikwa na Ludovick Kaijage. Anaelezea jinsi alivyoshikwa na kuwekwa kizuizini na usalama wa taifakipindi cha cha Nyerere kwa kuhisiwa uhaini. Ni kitabu rahisi chenye kurasa 87 na kinavutia kusoma. Shida ni kuwa mhandishi hajasema kama kweli alipanga uhaini au la. Ila kinasaidia kutoa mwanga jinsi usalama wa taifa wanafanya kazi na incompetence yao.
AFRICA IS IN A MESS, what went wrong and what should be done: kimeandikwa na Godfrey Mwakikagile. Kakitabu simple kenye kurasa 60 . kakitabu hakachoshi kusoma. Ila naona jamaa kaelezea tu jinsi Africa iko kweny mess ila hajasema what went wrong and what should be done.
THE FATE OF AFRICA: kimeandikwa na Martin Meredith. Kinaelezea historia ya Africa kiuchumi na kisiasa toka uhuru mpaka miaka ya 2000's. hakuna nchi imeachwa humo. Ni kitabu kizuri mno na sehemu zingine kinachekesha sana.
CURRENCY WARS; kimeandikwa na James Rickards. Kinazungumzia jinsi sarafu zinatumika kama silaha. Leo kuporomoka kwa ruble ni sehemu ya currency war. Ni kitabu kizuri.
THE ART OF WAR: ili kikuingie usome kikiwa na maelezo ya ziada. Mi nilikisupplement na documentary ya history channel inaitwa the art of war.
AMERICA THE BEAUTIFUL: kimeandikwa na Ben Carson. Kinazungumsia principles zilizoifanya marekani ifike ilipo, jinsi inavyochepuka na jinsi ya kuzirudia.
THE BRIEF HISTORY OF TIME: kimeandikwa na prof Stephen Hawking. Kinaelezea historia ya universe toka big bang. Kuna mambo yanachangamsha sana akili japo kuna concepts sikuweza kuzielewa. Nilikusupplement na documentaries kama through the wormhole na Hawking.
WHY NATION FAIL: kimeandikwa na Daron Acemoglu na James Robinson. Hiki kitabu bado nakisoma ila naona ndiyo best kati ya nilivyosoma mwaka huu. Hiki kinajibu ishu ya Mwakikagile ya what went wrong and what should be done.
THE KNIGHT IN AFRICA: kimeandikwa na mtanzania ambaye ni freemason, sir Chande. Kkinazungumzia maisha ya huyu jamaa aambaya kafanya ishu mbalimbali ndani yah ii nchi. Bibliographies na memoirs huwa zinavutia kusoma ila uhonest wake unakuwaga questionable.
NO LONGER AT EASE: ni kitabu kizuri cha Chinua Achebe.
We mwaka huu umesoma nini?
Katika nyuzi za miaka iliyopita naona hawa walikuwa wachangiaji, karibuni nyote.
Kiranga,
Roulette,
EMT,
The Boss,
Nyani Ngabu,
nyumba kubwa Mzee Mwanakijiji,
Horseshoe Arch,
LORDVILLE,
jeba,
Mwelewa,
Laleyo,
Habdavi,
AL SHARPTON,
leo.leo,
Mjuni Lwambo,
MSEZA MKULU,
Makirita Amani,
Kanigini,