Book reading: Unasoma au Umesoma kitabu gani ungependa wengine wakisome?

mkuu umeni inspire sana kusoma vitabu ila ebhu niambie ni vitabu gani ulivyovisoma vikakusaidia kupresent vizur

Kwa sasa nina kitabu kinaitwa Perfect presentation cha Peter Levin and Graham Topping (2006) lakini siwezi sema ndio kimenifundhisha nilikuwa nacho muda tu na sikuwa nakisoma kivile...ila sasa miaka kama 3 na nusu ilopita tulipewa kozi bana ya namna ya kupresent...hiyo kozi naweza sema ilikuwa sumu...ilinifanya ni learn from my mistakes...

Alokuwa anatufundisha alikuwa anatusisitizia wote tuwe na talking points always tunapokuwa tuna present...mimi zilinifanya nilipo present proposal yangu hadi supervisor wangu akanambia hakupenda kwani nilikuwa nategemea sana notes...lakini alitupata wengi sababu proposal ni mtihani...kuna kufukuzwa ukichemsha...kwa hiyo suala la muda wa ku pressent ni muhimu kuliko mbwembwe za how you present...tulikuwa na woga... kweli hatukutoka nje ya talking points most of us....matokeao yake inakuwa kama unasoma speech...yani wizi mtupu...afu huyo mama alitufanya tuone bila ile podium mtu huwezi present...sumu tupu...

Nikapata bahati ya kuwa jirani na baba mmoja amestahafu toka UN huyu akanipa trick nyingine...akasema ukitaka uwe good presenter lazima u memorize unachotaka kuongea...that real worked...

Yani trick ni kujua next slide hata kabla haujaifungua...na kujua kwenye hiyo slide utaongelea nini...presentation ni kama acting...you smile ...you tease people with questions that they don't have to answer; or you let them answer if they want to etc...na haina uhusiano wa kujua lugha or not...you don't have to be a native English speaker to be a good presenter ...we have many who are real bad na ni natives....

Sasa wengi unakuta anaanza kushangaa anatafuta cha kuongea na audience nayo inakosa imani na wewe...nikisema memorize haina maana hujui unachoongea ila umepangilia cha kuongea...unakuwa na flow ambayo ni coherent na inayoweka wasikilizaji kwenye suspense of what will be next....wanasema you need to tell your story...hata kama ni Biology you still can tell a story...

Kuna mdada ali present kuhusu topic ambayo ina uhusiano na nutrition (ni medical doctor) ...cha kwanza alichofanya alituonyesha picha mbili...moja ya mtu katoka supermarket kanunu makeki na lots of junk food...nyingine ya mtu alonunua vegetables na other healthy staff.... Akaanza kwa kutuuliza,...if you were the first person how would you feel after stepping out of the supermarket....watu 'Guilty'....unaona aliweza ku involve the audience kiasi kwamba hata miye si mtaalamu wa lishe ninaikumbuka presentation yake..she had a story to tell us...while presenting her technical work...begin with a story and finish with something memorable...yani kila mtu alikuwa anamsikiliza mwanzo mwisho maana we felt like we knew her topic already...

Siri kubwa ya kuwa presenter mwenye mvuto ni ku find a story to tell that people can remember... pili be ana expert to whatever you are presenting and memorize what you are to talk...all these needs rehearsal...ukisha master utakuwa unatamani kila siku upewe chance kuongea badala ya kukimbia kwa woga...


Nina ma supervisor wawili...moja hakuwepo akati na present lakini aliniomba eti nimtumie slides zangu maana amesikia habari zangu...nilimtumia lakini moyoni nikawa nasema it's not about slides ...it is about the presentation...na niliwa suprize mbaya maana supervisor alokuwepo alishazipitia slides zangu lakini hakujua kuwa ntamalizia na video clip ya 5 minutes (hiyo ilikuwa siri yangu maana nilijua kama muda hautaruhusu si lazima)...na hapo nilimuuliza chair if I still had time...akasema una 7 more minutes...ndio nikawaambia haya basi tumalize na hii video...siwezi iweka hapa maana nachofanyia research ni sensitive na kinagusa maslahi ya watu...nkiweka watanijua maana walinisumbua sana wakati niko field...
 
By best 3 books kati ya nilivyosoma mwaka huu 2014 ni hivi vifuatavyo;

3. Seven Habit of highly effective people by Stphene Covey

2. The Secret by Rhonda Bryrne

1. Kwaheri Ukoloni, kwaheri uhuru by Dr. Haith Ghasamy
 

ukusoma kwa roho that's why ukagundua huh ushetani ulioandika
 
Last edited by a moderator:
inawezekana haujapata vinavyo kukonga roho. mi kuna vitabu vingi nimeishia njiani ila vingine nasoma hadi usiku mrefu. kuna mdau aliwahisema kusoma isiwe adhabu bali tukufurahie. i hope utapata vinavyokupendeza.

sasa mkuu fanya kunipa list ya vile vitakavyokonga roho nivitafute nisome kwanzia mwakani lakini
 

Hahaha,

The Gleaner as in from Jamdown?

Kingston society ukikosa "Sunday Gleaner" wana ku disown.

Bounty Killer anakwambia atakufanyia halafu kesho watu wasome kwenye Gleaner.
 
Hahaha,

The Gleaner as in from Jamdown?

Yup...you got it.

Kingston society ukikosa "Sunday Gleaner" wana ku disown.

Bounty Killer anakwambia atakufanyia halafu kesho watu wasome kwenye Gleaner.

Nakumbuka wakati niko mdogo sana (early 80s) kuna siku nilienda na mshua Nkrumah hall kusikiliza hotuba ya Edward Seaga, waziri mkuu wa zamani wa Jamaica.

Si kwamba hata nilikuwa najua huyo Edward Seaga ni nani, la hasha. Ni kwamba tu mshua hakupata babysitter baada ya kunichukua kutoka kwenye daycare ya chuo (enzi hizo kulikuwa na daycare ya faculty and staff wa UDSM).

Sikuelewa kabisa huyo jamaa alichokuwa anakiongea lakini kila mara watu walikuwa wanapiga makofi. Wakati tunarudi nyumbani ndo nikaanza kumdadisi mshua.

Baadaye nilipoanza kujifunza kusoma na kuandika nikawa na mazoea ya kusoma soma chochote kilichokuwa kwenye meza ya kahawa.

Kila baada ya muda fulani nikawa naliona hilo gazeti. Ikabidi nimwulize mshua hilo gazeti linaitwaje naye akaniuliza kama nakumbuka nilipoenda naye pale Nkrumah kumsikiliza yule mgeni aliyekuja kutoa hotuba na akanambia hilo gazeti ni la nchi anayotoka huyo mgeni.

Kuna kipindi kwenye miaka ya 70 na 80 UDSM ilikuwa na faculty members kutoka nchi za Caribbean, Jamaica ikiwa mojawapo. Colleague mmoja wa mshua alikuwa na subscription (kupitia snail mail) na ndo huyo alikuwa akimpa kopi mshua.

Hii experience yangu ni ushahidi tosha kwamba wazazi wana influence kubwa sana kwa watoto wao hususan during formative years.

Mimi isingekuwa mshua sina hakika kama hata ningejua kuna gazeti linaitwa The Gleaner.
 

Duh, mchizi umemuona Edward Seaga Nkrumah Hall?

Mimi hata sijajua kwamba Seaga alishafika bongo.

Gleaner ukiwa msikilizaji wa reggae/dancehall halafu unasikikiza lyrics kama mimi huwezi hukosi kulijua.

Wanalitaja sana.
 
sure mkuu, tatizo siyo muda ni nia. inaonekana why nations fail kimetushika wengi.
 
 
great thread indeed,congrats y'all for good readings n insight..
well for me naonaga I read everything I lay my hands on hadi smtym sikumbuki headings,I.simply seek knowledge..
this December nakumbuka two readings I just finished,1.Rules of work na 2.Business Writing...authors ntaweka badae ,they are good ones kwa wanaofanya kazi maofisini
 
mimi wakati huu nilikuwa na wakati mgumu, nimesoma vitabu viwili, THE AUTOBIOGRAPHY OF BEN RANKLIN, POWER OF POSITIVE THINKING na sasa naendelea na THE LIFE OF MAHATMA GANDHI. najitahidi nimalize kabla mwaka haujaisha. kama kuna mwenyeji wa mwanza anielekeze mahala pa kupata novels nzuri maana tokea nihamie hapa napata shida sana
 
ukusoma kwa roho that's why ukagundua huh ushetani ulioandika

Kusoma kwa roho ni turufu inayotumiwa na watawala wanaotumia jina la Mungu ili kuficha mapungufu yao. Biblia ina mikanganyiko mingi ambayo inaitoa thamani ya kuwa kitabu cha rejea kiimani. Kuna mauwaji makubwa, zinaa zilizohalalishwa, sadaka za binadamu, kuhalalishwa kwa utumwa na mambo mengi ambayo si ya Kimumgu.

Kwa kusoma kwa roho na kusubiri mwongozo kutoka kwa kiongozi wa kiimani hakuwezi kukufunulia haya.
 
hongera msomi mwenzangu. nimesoma vitabu kiasi japo ratiba inabana. kati ya vingi nimesoma acres of diamond, the richest man in babylon, (very interesting educative books on how to make money and keep it), nimerudia the merchants of Venice, na the struggle from within, the walk to fredom cha mandela, na the davinch code. na vingine vingi. ( hiyo list yako nitaipata duka gani?)
 
Last edited by a moderator:

welcome to the fans of john Gresham. tafuta the firm-the best of john gresham, hautalala mpaka uimalize.
 
COMPLETE GUIDE IN PUBLIC SPEAKING - by Nick Jackson

WORLD GRAND SPEECHES - by Payal Kalia D.litt

GAY TRAVEL IN THE MUSLIM WORLD - by Michael T. luongo.

SUCCESSS THROUGH POSITIVE THINKING - by S.P Sharma

HOMOSEXUALITY IN ISLAM - Scott Siraj al-Haqq Kugle.
 
snipa ilikuwaje ukawa innterested na homosexuality?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…