1.Atomic habits by James clear- Kama Kuna tabia zinakusumbua hauzipendi unataka kuacha , au Kuna tabia mpya unataka kuanza kufanya lakini unashindwa au unaishia njiani this book will help a lot.
2.When breath becomes air by Paul kalanithi( a memoir)-a true story kuhusu daktari(neurosurgeon) aliyegundua ana kansa akiwa ndio kwanza anaanza kuenjoy career yake na akiwa na umri mdogo sana.(heartbreaking and humbling).Ukisoma Kuna namna utaanza kuyaangalia maisha in a different perspective, life is a gift cherish it.
3.Educated by Tara Westover (a memoir)- hii pia ni true story kuhusu msichana mmarekani aliyelelewa na wazazi wenye itikadi kali ya din, walikua hawaamini kuhusu kutibiwa hospitali,kwenda shule( walikua homeschooled) na masharti mengine mengimengi.ule msemo unaosema elimu ni ufunguo wa maisha ndio unadhirika kwa Tara.(funny, heartbreaking and educational)
4.Finding me by viola Davis(a memoir):hii ni story ya maisha ya muigizaji maarufu wa Hollywood kwa wasio mfahamu ameigiza kwenye tv show inaitwa 'how to get away with murder' hii ukisoma utajifunza vitu vingi Ila kikubwa zaidi Ni kwamba jana yako sio kesho yako.
5 Born a crime by Trevor Noah(a memoir) hii story ingawa imeandikwa n Trevor Ila inaongelea zaidi maisha ya mama Trevor pia ( funny, inspiration, emotional ) utacheka Sana, kinaaliza pia Ila zaidi sana kinafundisha I recommend kina mama wote mkisome.
6 I am malala(a memoir) - hatimaye niliweza kusoma hiki kitabu nilikuaga nakiruka mara nyingi ( inspiring, heartbreaking, educational) hiki kitabu kilinifanya nikajiulizq maswali mengi Sana hasa yanayohusu imani.i recommend wenye watoto teenegers wawape hiki kitabu pia wasome Kuna vitu watajifunza, kuleta impact kwenye jamii haijalishi umri ulionao you might as well start early(simnawaona chipukizi😊).
7.I'm glad my mom died by Jeanette maccurdy (a memoir)
Hii ni story ya child actor wa marekani miaka ya 2000 mwanzoni aliigiza na kina Ariana grande, hii story inaelezea mahusiano kati ya mama na mtoto, ( hilarious, emotional, ).