Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

Naomba mwenye kitabu cha Rich dad, poor dad by Robert Kiyosaki aniwekee hapa. Huyu kijana wenu aliyemaliza darasa la saba anataka kukisoma. Asanteni
 
Screenshot_20231219-195531.png
Mwenye PDF ya hiki kitabu, msaada please.
 
The Alchemist by Paul Coelho umewahi kukisoma? Ni kitabu kizuri sana, kirahisi pia kwa lugha na ukimaliza kukisoma hautojutia muda wako.
The boy!

Kitabu kizuri sana kuhusu maisha na utafutaji, kuna wakati nilijua Santiago baada ya kukutana na Fatima story ingeisha kumbe bado.

Kuna maoni pale kwamba mali tunazotafuta mbali zipo kwenye milango yetu.

Sehemu nzuri kwangu ni pale walikamatwa, Alchemist akasema, Santiago anaweza kujibadilisha kua upepo na Santiago akaamua kuongea na upepo, jua na jangwa na akawa upepo
 
SAsa nimeanzisha mfumo rasmi wa kusoma vitabu na notebook pembeni.

Nikisoma kitabu nikiona quote imenibamba na kugonga nyoyo na ina mafundisho basi nainote down.

Kwa hivyo nina kitabu rasmi cha mafundisho niliyopata vitabuni.


Jim rohn aliwahi kusema kwamba "usiiamini sana akili yako,kama kitu kina umuhimu kiandike sehemu"
 
yaani ukiwa na hela kwenye Mpesa, inakuwasha kuitumia, ukiwa na laki hutulii—ni ASILI.
mkuu hii sio asili,nimechunguza sana hii kitu wala haihusiani na asili,hii kitu tumekuwa programmed nayo tokea utotoni kwetu.

The way tunabehave,the way tunaspend money,the way tuna resct tunapokuwa na pesa au tunapokuwa hatuna hayo yoooote yametokana na namna ambavyo tumekuwa programmed.

Familia zetu nyingi za kitanzania tunalelewa katika malezi ambayo yanatufanya mwisho wa siku tuangukie katika mfumo ulioutaja kwamba ukiwa na pesa inakuwasha,unatamani kuitumia tu.

Hayo ni malezi na mazingira tuloyokulia nayo utotoni mpaka hivi leo tupo watu wazima na sio kwamba ni asili mkuu.

Hata suala zima la nidhamu ya fedha ama nidhamu ya jambo lolote hilo suala linategemea na namna ambavyo umelelewa huko nyuma na walezi wako.

Hivyo katika mambo ya tabia suala la kusema kwamba ni asili ndio inatufanya tuwe kadhaa mimi kwa maoni yangu nahisi bado hatujagundua tatizo.
 
Savings ni mwanzo wa kuelekea kwenye utajiri. Kadiri unavyoweka akiba, ndivyo utakavyohamasika kutafuta hela nyingi zaidi. Na siyo ajabu, akiba uliyoiweka inaweza kutumika kuanzishia mradi utakaokuja kukuingizia kipato kikubwa sana cha kukufanya kuwa tajiri.

Anza kuweka akiba, hata kama ni sh 20,000/= tu kwan mwezi. Muhimu, hakikisha huitumii kwa matumizi ya kawaida isipokuwa ya kukuongezea kipato.
Lengo la saving sio kutengeneza utajiri moja kwa moja.

Lengo la saving ni kutengeneza TABIA ambazo zinahitajika ili uwe tajiri.

So mtu ambaye anasave alfu 3 tu kila apatao mshahara wa laki 5 kwa muda wa miaka mi3 huyo atakuwa ameshadevelop tabia ya kusave.

tofauti na ukilinganisha na mtu ambaye anasave laki 1 kila akipata milioni 2 ila kwa mwaka husave labda miezi mi3 au mi4 anasema kuna miezi majukumu yanambana,huyu hatoona faida ya saving kwa sababu lengo la kwanza la saving ni kutengeneza TABIA katika ubongo.

Lengo la saving.

1.kutengeneza tabia kwanza.
2.kutunza pesa.
3.kuiwekeza pesa uliyoitunza kwa muda kadhaa.
4.pesa uliyoiwekeza ianze kuzaa.
5.baada ya kuzaa unaendelea kusave ili utafute jambo lingine la kufanya kwa ajili ya kutengeneza vyanzo vingi vya mapato.
 
JaMani mwenye soft copy kitabu hiki anitumie:" the occult sciences by anthony norvell pdf"
 
I am grateful that you are back, I had planned to tell you how I and my heart feel about by the time you left. I never thought you will be back again, now you are here like you never left. It was one hell of the wait.

So, I am putting myself smart before I do an approach, collecting all beautiful lines there are to tell.
Kweli Hakuna mkate mgumu mbele ya Chai,..( kwikwikwi 🤭🤭)
 
1.Atomic habits by James clear- Kama Kuna tabia zinakusumbua hauzipendi unataka kuacha , au Kuna tabia mpya unataka kuanza kufanya lakini unashindwa au unaishia njiani this book will help a lot.

2.When breath becomes air by Paul kalanithi( a memoir)-a true story kuhusu daktari(neurosurgeon) aliyegundua ana kansa akiwa ndio kwanza anaanza kuenjoy career yake na akiwa na umri mdogo sana.(heartbreaking and humbling).Ukisoma Kuna namna utaanza kuyaangalia maisha in a different perspective, life is a gift cherish it.

3.Educated by Tara Westover (a memoir)- hii pia ni true story kuhusu msichana mmarekani aliyelelewa na wazazi wenye itikadi kali ya din, walikua hawaamini kuhusu kutibiwa hospitali,kwenda shule( walikua homeschooled) na masharti mengine mengimengi.ule msemo unaosema elimu ni ufunguo wa maisha ndio unadhirika kwa Tara.(funny, heartbreaking and educational)

4.Finding me by viola Davis(a memoir):hii ni story ya maisha ya muigizaji maarufu wa Hollywood kwa wasio mfahamu ameigiza kwenye tv show inaitwa 'how to get away with murder' hii ukisoma utajifunza vitu vingi Ila kikubwa zaidi Ni kwamba jana yako sio kesho yako.

5 Born a crime by Trevor Noah(a memoir) hii story ingawa imeandikwa n Trevor Ila inaongelea zaidi maisha ya mama Trevor pia ( funny, inspiration, emotional ) utacheka Sana, kinaaliza pia Ila zaidi sana kinafundisha I recommend kina mama wote mkisome.

6 I am malala(a memoir) - hatimaye niliweza kusoma hiki kitabu nilikuaga nakiruka mara nyingi ( inspiring, heartbreaking, educational) hiki kitabu kilinifanya nikajiulizq maswali mengi Sana hasa yanayohusu imani.i recommend wenye watoto teenegers wawape hiki kitabu pia wasome Kuna vitu watajifunza, kuleta impact kwenye jamii haijalishi umri ulionao you might as well start early(simnawaona chipukizi😊).

7.I'm glad my mom died by Jeanette maccurdy (a memoir)
Hii ni story ya child actor wa marekani miaka ya 2000 mwanzoni aliigiza na kina Ariana grande, hii story inaelezea mahusiano kati ya mama na mtoto, ( hilarious, emotional, ).
 
Other Side of me. 🔥🔥🔥🔥
If tommorow comes. 🔥🔥🔥🔥
 
Back
Top Bottom