Ili tuende vizuri inabidi tujadili jambo moja kabla ya jingine,
Naomba nianzie suala la elimu,
Mifumo ya elimu kote duniani ipo kwa ajili ya kutengeneza wafanyakazi(labour force), Lengo la elimu ya darasani ni kukufanya wewe uwe mtumish(mtumwa?).
Na kwa maana hiyo ni vigumu sana kujiajiri, hata kama umesoma biashara(bussness) au ujasiliamali(entrepreneurship), nitaelezea ni kwa nini...
Mitaala ya elimu iko facilitated na matajiri wakubwa(tycoons) ili kupata wafanyakazi kwenye viwanda na makampuni yao, hivyo, elimu hiyo haina dhamira ya kukufundisha wewe kuhusu pesa. Kwani ukijua kuhusu pesa utakuwa tajiri na hautakubali kuajiriwa tena, hivyo watakosa mfanyakazi.
Ukisoma kuhusu Bussness Adminstration, unasoma kuhusu KUSIMAMIA PESA TU.
Ukisoma kuhusu FINANCE, unafundishwa mambo yahusuyo, HISTORY OF FINANCE, TYPES OF FINANCE, utasoma hadi FOREX ya
ONTARIO.
Money management jina linajielezea, ni kumanage pesa tu, hakuna la ziada...
Fani zote tajwa hapo zinakufundisha wewe kwa namna moja ama nyingine kusimamia pesa katika kampuni ya mtu and it rarely teaches you how to start your own company na Hufundishwi kabisa kitu cha muhimu kabisa, HOW TO MAKE MONEY/HOW TO MAKE MONEY MULTIPLY, kitu ambacho ni muhimu kabisa ili kutajirika..
Naomba niazime maneno toka kwenye The richest man in babylon, "I decided that i have to learn the principles on how to accumulate wealthy, make it my duty and do it well.." huyo ni Arkad aliyeamua hivyo, and that is the key,
Cha kusikitisha, hata usome finance au biashara, you are never taught, how to accumulate wealthy!
Unafundishwa kusimamia wealthy ambayo iko accumulated!