Zamani kabla sijaanza shule 1994, nilikuwa napitia kila gazeti na kitabu kaka zangu walicholeta ,kushangaa tu picha. Ma-broo wakaona bora wanifundishe kusoma wenyewe. Kweli, yaani nilianza shule nasoma kama cherehani. baadaye nikagundua napenda mno vitabu vya biashara na vya kiislam. Mpaka sasa, nimesoma zaidi ya vitabu 100.Zaidi. Nikaunda whatsapp group kuelezea kwa kifupi concept ya kila kitabu cha biashara kwa kiswahili bure. Hapa nashindwa upload audio zake. Kuna kitabu kizuri kinaitwa ''Blue Ocean Strategy'' kinaelezea umuhimu wa kujikita kwenye skill moja na ku-imaster kiasi cha kukosa mpinzani . Halafu kila kitabu nikisoma nahusianisha na mazingira ya biashara ya Tanzania , napata kitu kipya :Ngoja niwape hapa summary ya hiki kitabu cha ''Blue Ocean Strategy''
Kumbuka biashara nyingi ( ukiacha chache mno) bila kutangaza kwa social media unakuwa Unafanya kitu sahihi ila kwa wakati ulopita, wakati tunahama toka ujamaa kuja soko huria ( 1985 mpaka 1990) ambapo wafanyabiashara wachache walihudumia wateja wengi mno.
Kufika mwaka 1995, sera za wahisani zilitutaka tupunguze waajiriwa wa serikali, hivyo kuongeza wafanyabiashara
Kufika mwaka 2010 Hadi 2015, idadi ya vyuo vikuu vinavyozalisha wahitimu, ikifika vyuo 50 toka chuo kimoja( udsm) wakati tukipata uhuru
Hapa ukazuka msamiati mpya wa ' ujasiriamali' yaani vijana na watu wazima wanajiajiri kwa kutatua matatizo yanayoizunguka jamii ( fursa) na kujipatia kipato
Kama haitoshi, toka 2016 Hadi 2019 wimbi la waajiriwa kujifunza na kufanyia kazi suala la kipato Cha ziada limekuwa likiongezeka
Hivyo, Kama wafanyabiashara Ni mapapa, na wateja Ni samaki, tunasema , mapapa Wengi wanagombea samaki Wengi lakini kwenye bwawa moja, Kuna hatari ya mapapa kuumizana, kung'atana na kumwagana damu. Madhara ya ya papa kuchangia bwawa ndo Kama vile: mjasiriamali kulazimika kushusha bei licha ya kuwa na bidhaa Bora ili aendane na papa wavamizi
NINI SULUHISHO:
Swali zuri wanalouliza wanafunzi wangu Mara kwa mara
Jibu Ni kuwa: Wewe Kama papa, unatakiwa ujitenge na mapapa wengine, kwa kuweka himaya yako na kujilia samaki wa peke yako, na kila papa atayeingia katika himaya yako utajua jinsi ya kumuangamiza. Najua ujaelewa, nakupa mifano
Tuanze ya kimataifa
Bill gates alivyoanza alikuta IBM wanazalisha computer hardware, akaona himaya yake Ni kujitenga , yeye akazalisha software na kuwauzia IBM
Yahoo walivyoona bill gates anazalisha software,wao wakatoa huduma ya email
Google walivyoona emails imeshikwa na Yahoo, wao wakatoa huduma ya search Engines
Hadi kuja kwa Facebook wakaona hawawezi compete kwenye search engine, wakaja na social media, mwanzo Facebook, wakanunua Instagram na Sasa wamenunua Whatsapp
Ukija kwa Tanzania, watu mwanzo waliona watoto wadodo na wakubwa wote wanachanganywa primary, wao wakalenga watoto wadodo tu (3 to 5 years) Wana shinda nao day care
Hii strategy ya biashara inaitwa BLUE OCEAN STRAGETY ( hili Ni jina la kitabu pia, kitafuteni kwa reference). Nishachambua vingi mno