Acronomy hebu fafanua kidogo.
Nimepata fursa ya kuishi na watu wanaosoma vitabu, wa kwanza alikuwa Uncle wangu, huyu kwake alikuwa ''book shelf''kubwa na alikuwa msomaji mzuri sana wa vitabu. Nilianza kusoma vitabu nilipokuwa naishi kwake, hakunilazimisha wala alikuwa hajisifu kwa usomaji wake wa vitabu lakini alikuwa na msemo wake ''ubongo unahitaji kulishwa vitu tofauti kila mara, na njia nyepesi ni kusoma vitabu vya kila aina'' . Kauli hii ilinivutia na nikaanza kusoma vitabu. Watoto wa huyu uncle wangu sio wasoma vitabu kabisa na anko wala haonyeshi kuwalazamisha.
Wa pili ni baba yangu, ni msomaji mzuri sana wa vitabu hasa Spiritual Books na Bible Commentaries. Tumezaliwa kadhaa kwetu, mzee alituandalia mazingira ya kuwa wasomaji wa vitabu ikiwemo kuwa na ''book shelf'' kubwa na kununua vitabu vingi tofauti tofauti, lakini kamwe hakuwahi hata kutulazimisha kusoma vitabu.
Nadhani utambuzi mmoja wapo wa muhimu sana unaoupata kwenye usomaji wa vitabu ni kutambua kuwa watu wapo tofauti hivyo unaanza kuelewa binadamu wengine na kuheshimu ''interest'' zao.
Wasoma vitabu wazuri huwa na tabia hizi
1. Huwa na misamiati mingi katika lugha husika
2. Huandika na kuongea kwa ufasaha
3. Huwa na ujuzi wa kuelewa namna ya kuishi na watu
4. Sio watu wanaochangia kila mada, huwa wasikilizaji wazuri na ikitokea akaongea basi huwa anaongea kwa kujiamini na kwa usahihi.
5. Hawana ubishani sana hata kama yupo sahihi.
6. Uelewa mpana wa dunia na mambo yake.