Vingine ni kweli na vingine umewaonea Mbeya. Baridi si rafiki wa Swimming pools na nightlife. Uingie kwenye swimming pools na lile baridi, au ulitaka yawe heated, kwa umeme huu?
Mbeya hakuna haja ya masupermarket, kuna masoko kila kona. Masafi na yana bidhaa fresh zinazouzwa. Na masoko ni mazuri sana kwa uchumi kuliko supermarket moja ya kampuni kubwa.
Na miji mingi utakuta maofisi na masoko yamerundikana sehemu moja. Mbeya pametengana, na ni jambo zuri. Sehemu za maofisi hazihitaji vurugu.
Kwenye suala la hotel bado sana. Nafikiri sababu hakuna watalii wala wageni wa kimataifa. Gym hakuna uhitaji, vilima vile ni gym tosha.