Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Wakuu Kwema!!!
Tutozane.
Tukamuane,
Tuzinguane,
Tuchapane,
Tuchanane,
Lakini tusiuane.
Kwa kweli Mimi Taikon naona ni mara elfu Tozo kuliko Kutekana, kuuana, kupotezana Kwa kisingizio cha Uzalendo, sijui maendeleo, sijui vitu gani.
Nchi sasa inaenda Sawa Sawa, mambo yamenyooka. Mapungufu kidogo hayakosekani lakini sio Yale ya kutisha, kutishana na kumalizana.
Hakika ni Bora tuwe kwenye nchi Masikini isiyomwaga Damu za watu wake kuliko kuwa na Nchi yenye maendeleo isiyojali maisha ya watu.
Sisi wote ni ndugu ndani ya taifa hili. Hata Kama upo utofauti wa kichama, Kidini, kikabila n.k lakini tunaunganishwa na udongo WA taifa letu.
Kuchikizana kupo, kukwazana kupo, kutofautiana kupo, hayo yote isiwe sehemu ya kumalizana kupotezana.
Kwa kweli, kamwe siwezi jivunia nchi inayoshindwa kuthamini maisha ya watu wake, na hapa namaanisha Uhai.
Niliwahi sema, fanya ufanyalo usiinajisi nchi Kwa kumwaga damu za watu wako mwenyewe Kwa kisingizio chochote kile. Ni laana, na Kama Mungu aishivyo itakutafuna.
Ni Bora Tozo,
Ni Bora umasikini,
Ni Bora malumbano ya hoja yenye lengo la kujenga,
Kuliko chuki zinazopelekea watu kuuana.
Ndugu Watanzania, nasisitiza, usiinajisi Nchi Kwa kumwaga damu isiyo na hatia.
Taikon Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam