Bora Uishi karibu Kodi kubwa ama mbali na nauli kubwa

Bora Uishi karibu Kodi kubwa ama mbali na nauli kubwa

Swensa

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
2,880
Reaction score
4,295
Screenshot_20250414-094623.jpg
Maoni yako Tafadhali
 
Siku ukikosa kodi unafanyaje? Bora ukose nauli unaeza piga by foot na hata mtu akakupa lifti au mtu kukupa buku la nauli sio shida. Kodi ni kipengele sana haswa kama huna mishe inayoeleweka mjini. Ndio maana mtu anaeza ishi bunju na akafanya kazi zake posta. 🫵
 
Inategemea na kipato chako. Kazi yako. Mazingira ya makazi

Kuishi mbali tegemea kupoteza muda na matukio yatakayotokea njiani
 
Bora inategemea zaidi na kazi na kipato chako
Wakati mwingine kupata hela kubwa kwa pamoja ni ila ndogo ndogo sio shida
 
Ishi Karibu na Kazini kwako ulipe Kodi kubwa;
Utaokoa muda wa kwenda na kurudi kazini;
Utaachana na Frustration za Barabarani; Utawahi kazini kwa wakati na kujijengea Sifa njema hata Promotions kwa Mwajiri; Utapata muda wa kufanyakazi za ziada bila wasi wasi na kulipwa Overtime mara mbili ya kodi unayolipa;
Nauli/mafuta ya kwenda kazini nafuu;

All in all utaifurahia kazi yako kwakuwa unapata Muda wa kulala usingizi wa kutosha. Wakati anayeishi Chanika anaamka saa 11 alfajiri wewe utaamka saa 1 asbh. Huyu wa saa 11 kazini ataishia kusinzia na kutoa lugha za hasira so productivity yake itakua ndogo.

Anyway Maisha hayana formula ishi upendavyo mkuu.
 
ukifanya mahesabu ya mwaka mzima, gharama za usafiri zinaweza kula hela nyingi kuliko ile tofauti ya kodi kubwa.
 
Back
Top Bottom