Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Boris Johnson akiwa na Rishi Sunak na Sajid Javid Bungeni, Picha na PA.
Mawaziri wawili waandamizi wa serikali ya Uingereza jioni hii wamejuzulu nafasi zao.
Mawaziri hao ni waziri wa fedha Rishi Sunak na waziri wa afya Sajid Javid.
Katika barua zao za kujiuzulu mawaziri hao waandamizi wameelezea sababu za kujiuzulu zikiwemo kutokuwa na imani na waziri mkuu Boris Johnson na kushuka kwa viwango vya uendeshaji wa Serikali.
Pamoja na mawaziri hao pia viongozi wengine waandamizi wamejiuzulu nafasi zao akiwemo makamu mwenyekiti wa chama cha wahafidhina bwana Bim Afolami, katibu wa bunge bibie Saqib Bhatti, balozi wa Uingereza nchini Morocco Andrew Murrison wa masuala ya biashara na Jonathan Gullis ambae ni mwakilishi wa Serikali kwa upande wa Ireland ya kaskazini.
Kujiuzulu kwa viongozi hao kunafuatia habari kwamba waziri mkuu Boris Johnson alikuwa anafahamu kuhusu tuhuma za ubazazi zilokuwa zikimkabili aliekuwa kiongozi wa wabunge bwana Chris Pincher kabla ya kumpa nafasi hiyo lakini akapuuzia.
Bwana Chris Pincher amekuwa na tabia ya kulewa na kisha kuanza kuwashika wanaume wenzie awapo katika klabu ya wanaume ya chama cha wahafidhina iliyopo katikati ya jiji la London.
Lakini wiki ilopita alipolewa alianza kuwashikashika (groping) wanaume wenzie zaidi ya wawili ambao baadae walitoa malalamiko kupitia watu mbalimbali, malalamiko kufikia kwenye vyombo vya habari.
Waziri mkuu alipojulishwa juu ya jambo hilo alipuuzia na kusema binadamu hukosea lakini akasahau kwamba mwezi Februari alijulishwa juu ya malalamiko juu ya tabia za bwana Pincher na akapuuzia na kumteua katika nafasi nyeti serikalini.
Lakini sababu zingine za kujiuzulu kwa viongozi hao zasemwa kuwa ni kuogopa kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao ambapo hadi sasa chama cha wahafidhina kimepoteza imani kwa wananchi kwa kutodhughulikia uzuri masuala ya mfumuko wa bei, kupanda kwa hgharama za maisha na kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali yakiwemo mafuta ya petroli na dizeli.
Bwana Johnson jioni hii aliendelea kuketi na mawaziri kadhaa huku akiwa na muda mrefu na waziri wa elimu bwana Nadhin Zahawi ambae huenda akawa waziri wa fedha.
Zahawi ni mmoja wa mawaziri waandamizi walobakia lakini mwenye kupewa nafasi kubwa ya kuwa waziri wa fedha ambapo ofisi yake yaitwa namba 11.
Zahawi alihamia nchini Uingereza mwaka 1976 akiwa na miaka 9 yeye na familia yake walokimbia madhila ya aliekuwa raisi wa Iraq Sadam Hussein.
Hiyo kumaanisha kuwa Uingereza itakuwa na waziri wa fedha ambae hakuzaliwa Uingereza lakini amekulia hapo na kupata elimu yake nchini humo.