#COVID19 Boris Jonson: Sheria za kuvaa barakoa na kukaa mbali hazitakuwa lazima Uingereza

#COVID19 Boris Jonson: Sheria za kuvaa barakoa na kukaa mbali hazitakuwa lazima Uingereza

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Jonson amesema kuwa yeye ataendelea kuvaa barakoa katika maeneo ya watu wengiImage caption: Waziri Mkuu Boris Jonson amesema kuwa yeye ataendelea kuvaa barakoa katika maeneo ya watu wengi.

Waziri mkuu, Boris Johnson, alisema alitarajia kupunguza sheria za Covid kumi na tisa katika wiki mbili kutokana na kufanikiwa kwa mpango wa chanjo.

Uvaaji wa barakoa na kukaa mbali zitaondolewa miongoni mwa sheria za lazima katika mwisho wa mpango wa ''lockdown'' ya corona, amethibitisha Waziri Mkuu Boris Johnson. Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour, Sir Keir Starmer, aliishutumu serikali kwa kile alichodai ni kuzembea uongozini.

Sheria ya watu sita ndani ya nyumba itaondolewa na muongozo wa watu kufanya kazi nyumbani kwa miezi 16 itaondolewa.

Wazir Mkuu Boris Johnson amesema anatarajia hatua za mwisho zitaendelea kuanzia tarehe 19 Julai kama ilivyopangwa.
Hii itathibitishwa tarehe 12 Julai baada ya tathmini ya data za hivi karibuni kuhusu corona.

Wakati huo huo chama kikuu cha upinzani cha Uingereza kimeishutumu serikali kwa kutowajibika, baada ya kuthibitisha mipango ya kuondoa masharti mengi dhidi ya Corona nchini Uingereza.

Uingereza ni nchi ya kwanza kufanya hivyo wakati maambukizi yakizidi kuongezeka. Bw Johnson amesema hata baada ya kuondolewa kwa sheria ya kuvaa barakoa binafsi ataendelea kuvaa yake katika maeneo yenye watu wengi kama " adabu’’ .

1625556281328.gif
 
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, amesema alitarajia kupunguza sheria za COVID-19 katika wiki mbili kutokana na kufanikiwa kwa mpango wa chanjo.

Amesema sheria za uvaaji wa barakoa na kuweka umbali baina ya mtu na mtu ni miongoni mwa sheria ambazo zitakuwa si za lazima katika mwisho wa mpango wa ''lockdown'' ya corona.

Sheria ya watu sita ndani ya nyumba itaondolewa na muongozo wa watu kufanya kazi nyumbani kwa miezi 16 itaondolewa.

Waziri Mkuu Boris Johnson amesema anatarajia hatua za mwisho zitaendelea kuanzia tarehe 19 Julai kama ilivyopangwa, Na hii itathibitishwa rasmi tarehe 12 Julai baada ya tathmini ya data za hivi karibuni kuhusu corona.

Aidha, Bwana Johnson amesema hata baada ya kuondolewa kwa sheria ya kuvaa barakoa binafsi ataendelea kuvaa yake katika maeneo yenye watu wengi kama "adabu’’.

#ChanzoBBCSwahili
 
Sasa hapo wao si wamesema wamefanikiwa mpango wa chanjo wakati sisi tumefanikiwa mpango wa nyungu.
 
Wakati huo huo chama kikuu cha upinzani cha Uingereza kimeishutumu serikali kwa kutowajibika, baada ya kuthibitisha mipango ya kuondoa masharti mengi dhidi ya Corona nchini Uingereza.
Hawa nao wanapinga kila kitu - wanakwamisha maendeleo ya waingelezawanakuwa kama CDM.
 
Waziri mkuu wa Uingereza bwana Boris Johnson amesema waingereza lazima wajifunze jinsi ya kuishi na ugonjwa wa Corona ,hivyo anatarajiwa kutangaza mpango wa kuondoa sheria inayolazimisha watu kuvaa barakoa na kufanya social distance.

Bwana Johson anatarajiwa kufanya hivyo huku maambukizi ya kirusi kipya kinachoitwa Delta yanazidi kushika kasi nchini humo.

Screenshot_20210706-104836_millardayo.jpg
 
Ungekuwa mwandishi wa habari, magazeti ya Shigongo yangekuwa ndio ofisi yako
 
Kama ilivyofanya Marekani miezi mitatu iliyopita, Julai 19, ni zamu ya Uingereza kulegeza mashariti ya kujikinga na COVID19 baada ya kugundua chanjo na barakoa hazina msaada wowote.

Rais wetu mpendwa, mzalendo na.1 , mwalimu, mkemia Daktari JPM alilegeza mashariti toka mwaka 2020...alionekana mwendawazimu lakini leo maamuzi yake yanachukuliwa kwa umakini na dunia.

Wallah wote humu JF tutakufa...na haitatokea kupata rais shujaa na imara kama JPM.
 
Tarehe 12 Julai 2021, Uingereza inatarajia kusitisha uvaaji wa barakoa wa lazima, social distancing, uzuiaji wa mikusanyiko mikubwa ya watu, lockdowns na vizuizi vingine vyote vilivyokuwa vimewekwa kukabiliana na janga hili la covid 19.

Kiwango cha maambukizi Uingereza juzi tarehe 4 July yalikuwa wagonjwa wapya 24,170 na vifo 15. Jana tarehe 5 Julai wagonjwa wapya walikuwa 27,334 na vifo vilikuwa 9.

Sisi Tanzania tuna wagonjwa 100 (wapya + wazamani) na kati ya hao, 70 ndiyo wako kwenye mitungi ya gesi. Takwimu za vifo sisi huwa hatuziweki hadharani kutokana na tamaduni zetu kwani huleta taharuki kubwa na social stigmatization kali.

Kama hivyo ndivyo, kamati ile teule ya mapambano dhidi ya corona inapaswa kutathimini upya miongozo yao ya namna ya kushughulikia gonjwa hili. Inaelekea kamati hiyo inakumbuka shuka wakati kumeshakucha. Kwa mfano kwa nini ulazimishe watu kuvyaa barakoa waendapo kupata huduma kwenye tasisi za serikali nk.? Kwanza wengine barakoa ni hatari kwa afya zao. Utasemaje kuwa wagonjwa wote wanaoenda kumuona daktari wawe wamevaa barakoa? Si utawaua baadhi yao hususani wenye matatizo ya upumuaji?

Watu wapatiwe tu elimu. Hayo mengine wafanye kwa hiari. Huu ugonjwa uko hapa na utadumu kuwa hapa, tupende tusipende kama ambayvo ukimwi umedumu na utaendelea kudumu kama kaswende na wenzake walivyodumu! It is here to stay. Tujifunze kuishi nao.

Source: BBC
 
Back
Top Bottom