hiyo sababu wameitangaza wapi in public? au ni wewe umefikiri kwa fikra zako?...
kabla ya kuchanja hiyo 70% unafikiri kwanini hawakuwaacha watu waendelee na maisha na baadala yake wanataka waendelee na maisha baada ya kuchanja 70%?..
unazijua takwimu za vifo na maambukizi huko UK kabla ya kuchanja hiyo 70%?......Kwanini isiwe maambukizi na vifo vimepungua baada ya kuchanja hiyo 70% na iwe hivyo unavyotuaminisha?...
Unazijua takwimu za vifo na maambukizi Tanzania kuanzia august 2020?...tunasimamaje kifua mbele kuambia dunia Covid Tanzania haina madhara?
Tusilete mchezo na hii kitu aisee, tumuombe Mungu, tuielimishe jamii juu ya hili gonjwa, tuache propaganda, tutumie kila mbinu tunayoona inaweza kunusuru maisha ya watu na sio kujidanganya hamna tatizo huku watu wanakatika kimyakimya, tushare mbinu na wenzetu kila zinazofaa ili kunusuru jamii maana huwezi jua wave yeyote ikikukuta inaweza kuleta athari kiasi gani...