Kaka unapata habari zako wapi?
1. Masharti ya Covid yanaendelea London. Hakuna kitu kilichoondolewa. Soma hapa sheria zilizopo:
(COVID-19) Coronavirus restrictions: what you can and cannot do
2. Kwenye mpira angalau nchi nyingi za Ulaya zinasema ni kosa kuruhusu watu wengi kukutana pale London. Waingereza wanajitetea wakisema
a. hakuna aliyeruhusiwa kuingia asiye na uthibitisho wa chanjo kamili au cheti cha kupimwa Covid
b. wanasema idadi kubwa ya watu waliochanjwa inaunguza hatari.
c. Sehemu za kubanana kama getini au ndani ya jengo wote walipaswa kuvaa barakoa lakini waliruhusiwa kuiondoa wakifika nje kwenye viti vyao.
3. ni kweli watu wamechoka. Hata hivyo sheria ziko.
Kuhusu Chanjo ona matangazo ya leo:
View attachment 1845321
Chanzo: Daily summary | Coronavirus in the UK
Unaona kwamba maambukizi yanaongezeka tena (Virus Delta, kushoto "People tested positive"), lakini vifo haviongezeki (kidogo sana) na watu walikuwa wagonjwa hadi kupelekwa hospitalini waliongezeka kidogo tu. Yote shauri wa chanjo pamoja na sheria ya kuvaa barakoa na kutokutana na watu wengi.