Bosi wa Toyota ajiuzulu kupisha mabadiliko ya kampuni kuingia kwenye Magari ya Umeme

Thanks brother, umeongea point sana sana!
Natamani wengi wetu tungekuwa na mawazo kama haya.
 
The late would be the best ila ubaguzi, majivuno, na kiburi vilim-let down sana. Angetuvusha.
 
Hivi huyo, ni tajiri namba ngapi duniani?
 
The late would be the best ila ubaguzi, majivuno, na kiburi vilim-let down sana. Angetuvusha.
Masifa tu
Alikuwa anafanya vitu kwa kushangiliwa ndio anaona raha
Alikuwa na vision ila alivuka mipaka mingi sana na kujiona yeye ndio alfa
Ila hakujua kuwa anatengeneza maadui kwa kuwachamba waliokuwa kwenye system
He suffered a lot as a result of it
Ndio ukawa mwisho wake
 
Mfalme Suleiman aliomba vitu vichache sana kwa Mola wake; HEKIMA na MAARIFA ya kuliongoza taifa. Only that!
 
Thanks brother, umeongea point sana sana!
Natamani wengi wetu tungekuwa na mawazo kama haya.
Natamani kungekuwa na mji ukajitenga na watu wenye uelewa sio waizi sio wajanja wajanja na sio matapeli

[emoji631] kuna watu walijitenga na wengine na kuchukua land kubwa na kuanzisha mji wao ila utafanyiwa uchunguzi sana mpaka kuingia humo
Hakuna violence kabisa na wanafanya mambo yao

Sisi tunashindwa hata kuwa na uchungu wa mali zetu hatuwezi kufanya kitu
Hata nikisema nishirikiane na watu tufanye kitu naishia kuibiwa tu

Najua maisha ya huko natamani angekuja Rais mwenye uthubutu na kukataa ujinga wa kuagiza hata bolt
 
Ni vile tu tulimwelewa Magufuli vibaya au yeye alieleweka vibaya kwetu au kweli alikua haieleweki, lakini angelifikisha taifa mahali ambapo tusingejutia uwepo wake.

Lakini pia chief ninyi wachache ambao nuru imewatokea kuna mahali hamjafanya vyema kutushuhudia jinsi dunia ilivyo pambazuka, I consider mfano ulioutolea juu kujitenga kwa hao jamaa huko Usa
 
Huyo new CEO kama ndio alisimamia Lexus basi anastahili na nina imani atawavusha, ile gari matata sana, dashboard ni kama uko kwenye ndege na finishing yake ya ndani , wood yake ni top notch
 
Kweli mkuu tatizo lake alipiliza na kusahau malengo yake yalikuwa nini na anatupeleka wapi?

Anyway hayo yamepita na tumejifunza na atakumbukwa kwa mengi kama Rais aliejaribu

Mkuu nilikuwa naangalia YouTube kuhusu watu walioondoka ulaya au Amerika na kurudi kuwekeza Africa kweli kuna nchi nyingi wanawekeza ambazo wanakubali dual citizenship na wamewekeza miradi mikubwa mikubwa

Imagine mimi nimekaa miaka 35 [emoji636] na ninakaribia kustaafu nitahitaji kuja kuwekeza Africa na kuwa na sehemu ya kumalizia umri wangu

Unafikiri nikirudi nyumbani nitapokelewa kama mtoto wa nyumbani? Hasha mimi nitaitwa majina ya kila aina

Ila wenzetu ukiangalia hadi raha wanavyopokelewa na kupewa mashamba makubwa makubwa na wana invest pakubwa na kuajiri wazawa kibao

Nawajua wengi sana waliorudi Botswana, Kenya, Uganda, Ghana na wengine
Mkuu hebu imagine wakigusia dual citizenship utasikia ooh kwa sababu wakubwa watoto wao wana uraia

Hivi kiongozi mkubwa wanafikiri watoto wao hawana passport mbili?
Na wanaingia na kutoka na wakikaa huko wana passport ya huko?

Hata Rwanda anatushinda amekubali

Ghana mwaka 2019 waliwaita diaspora na kuwapa ardhi kubwa sana wawekeze na kweli walirudi wengi sana na kuwekeza kwenye kilimo na mifugo

Sasa mimi nikilipwa malupulupu yangu nije kuishi kwetu kama mkimbizi? Na hela ninazo si bora nikawekeze Botswana sasa ambapo nitalindwa na mali zangu 24/7?
 
Hayo mawazo tunayo vijana ambao hatupo kabisa kwenye system ya uongozi kazi za juu..
Wazee wetu smart phone tu zinawashinda kutumia hawana uwezo wa kuwaza hayo.
Nitake radhi mimi mzee tena nina wajukuu I swear ila siko kama wao [emoji1]
Hao wazee wamechaguana kwa akili zao finyu ndio maana unawaona miaka na miaka wamo kwenye system

Na wakileta watoto ni wale wale wenye akili kama baba zao maana wamekua wakiona ujinga wa baba zao
Sorry to say that [emoji28] ila ndio ukweli
 
Cobalt Congo, lithium Congo na Zimbabwe, Nickel Zambia, Zimbwabwe, Madagascar,

China amesha Book nchi zote hizo kwenye race ya Batteries, tutakuja kutumikishwa kuchimba watafaidika wengine.
Angalia tunayo yajadili na wao leo wameweka kwenye gazeti lao hapa [emoji636]
Coincidence?
Haki ya Mungu nilipoliona gazeti tu nikaukumbuka huu uzi na kupiga screenshot
Haya ndio maisha ya muafrika na wameyakubali
 
Angalia tunayo yajadili na wao leo wameweka kwenye gazeti lao hapa [emoji636]
Coincidence?
Haki ya Mungu nilipoliona gazeti tu nikaukumbuka huu uzi na kupiga screenshot
Haya ndio maisha ya muafrika na wameyakubali View attachment 2500679
Yah hizi issue zipo mda sana, sema wanazizima, na haya madini si salama wanakufa taratibu
 
Changamoto nyingine ni hili ulilolizungumzia.
Haswa changamoto kubwa ni viongozi wetu na watunga sera wetu.
Nadhani bado wapo kwenye ujima, na wapo bado kwenye usingizi, bado Kwenye fikra zao hakujapambazuka.

Labda ufahamu wangu ni mdogo sana lakini kwa kweli sijaweza kuona ubaya wowote kwenye uraia pacha.
Binafsi naona ilikua ni fursa adhimu sana kwa sababu aliyetoka nje kuna nuru fulani ameipata.

Ukiangalia taifa letu miaka hii ya 2020 na ile miaka 1970 unaweza ukaona ni heri miaka ile ambayo kulikua na viwanda vinavyozalisha kwa vingi na vingi vikiwa property ya Tanzania.
Tofauti na sasa, ambapo dunia inakimbia kwa kasi sana kwenda mbele kwa teknolojia na maarifa makubwa sisi badala yake tunakimbia kurudi nyuma tena kwa kasi sana .

Kama wasomi, na wataalamu waliopo hapa nchini wangekua na uthubutu na maono na nia pengine tungekuwa tunaongea vinginevyo, lakini kila mtu anaona.

Dhania yangu tungeweza sana kusaidiwa na diaspora kwa kiasi kikubwa kama tungekuwa na nia ya kupata msaada wao katika muktadha mzima wa maendeleo.
 
Angalia tunayo yajadili na wao leo wameweka kwenye gazeti lao hapa [emoji636]
Coincidence?
Haki ya Mungu nilipoliona gazeti tu nikaukumbuka huu uzi na kupiga screenshot
Haya ndio maisha ya muafrika na wameyakubali View attachment 2500679
Bora hao wanalipwa dola 2 ambapo ni karibu 5500 ,huku kwetu kuna kampuni na viwanda vyenye majina na status kubwa hapa nchini na pengine Afrika wanawalipa wafanyakazi wao 3,000 mpaka 4,000 ambayo ni kama dola 1.5 .
 
Naona toyota wamenusa hatari na kujifunza kwa kile kilichowakumba Nokia kwa kuchelewa ku-adopt mapema teknolojia ya android.

Wamefanya vizuri kuchukua hatua mapema ktk hili, vinginevyo wangekuja kupoteza umaarufu sokoni siku za usoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…