Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema kati ya maombi 16 ya ‘aplikesheni’ yaliyopokelewa kwa ajili ya kutoa mikopo mtandaoni, manne pekee ndiyo yamekidhi vigezo na kupewa leseni za kukopesha, huku aplikesheni 55 zikikabidhiwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili ziondolewe mtandaoni.
Meneja Msaidizi Idara ya Huduma Ndogo za Fedha BoT, Mary Ngasa amesema programu zilizopewa kibali zinatakiwa kuweka wazi kuwa zinafanya kazi kwa mujibu wa leseni inayotolewa na BoT, kuweka wazi masharti ya mikopo pamoja na mawasiliano ambayo wateja wanaweza kuwasiliana nao kwa jambo lolote.
Aidha, amesema BoT imebaini ukiukwaji wa sheria kwa watoa huduma ndogo za fedha (microfinance) kwa kuanzisha programu za kukopesha mtandaoni kinyume cha sheria zilizowekwa.
Soma, Pia:
Aidha, amesema BoT imebaini ukiukwaji wa sheria kwa watoa huduma ndogo za fedha (microfinance) kwa kuanzisha programu za kukopesha mtandaoni kinyume cha sheria zilizowekwa.
Soma, Pia: