BoT mulikeni huu wizi kwenye benki unaitwa "Processing fee"

Acha kukopa..unajipeleka mwenyewe afu unakuja hapa kulia Lia..mtu yeyote ukiwa na nidham na fedha zako hutokopa daima hata kama Kuna project unataka kuanzisha utaanza nayo taratibu Kwa pesa uliyonayo...

Kuchukua mkopo ni tamaaa zilizomo ndani ya binadamu maskin wa fikra..na mtakoma Kwa hzo tamaa zenu...lipa mkopo
 
Hapana bhana,
Bank Gani hiyo?
Kwa benk nyingi makato ya bima na processing fee ya mkopo vinakatwa percentage wise..
 
Hili ni tatizo.Halafu wanapofunga mahesabu huwa wanasoma faida waliyopata kwa sauti kuuubwaaa.Kumbe ni fedha za wizi kimaandishi.
 
Hapana bhana,
Bank Gani hiyo?
Kwa benk nyingi makato ya bima na processing fee ya mkopo vinakatwa percentage wise..
mzee usibishe babu.

hao ni NMB na kama inapungua kidogo hapo nilipotaja basi ni laki au laki na nusu.
kuna bima hapo na ada,zote hizo ndio gharama zake hizo.

kama ni 17%-16% ya mkopo unadhani unadhani itakuwa shilingi ngapi kwa 15ml??
 
Watanzania tunatumia mikopo vibaya. Unakopaje mkopo wa kulipa miaka 5 - 9. Hapo lazima bank wakufurahie.

Kopa mkopo wa miezi 12 - 24
 
Ukitaka riba ipungue shusha miaka ya kufanya marejesho iwe angalau miaka mitatu. Ila ni lazima uwe na vyanzo vingine vya mapato vinginevyo mambo yatakuwa magumu sana. Mkopo uko fair huo
 
Naomba unieleweshe kuhusu hiyo PBZ Kwa Mimi niliyeko Huku mpanda na hakuna wakala nakopaje?
Njoo Dodoma au nenda Dar ndio wana matawi yao. Njoo ukiwa na viambatanisho vyote.

Cha kwanza ona kama nao wameshaanza kukopesha kupitia Watumishi Portal. kama bado, ndio uje. CRDB na NMB wao teyari wameshajiunga na huu mfumo wa online wa serikali. PBZ walikuwa bado ila inawezekana na wao teyari hivyo hutahitajika kusafiri.
 
🤣🤣🤣
Yaani Ukope 1.7mil halafu wanakupa 200k Huo si utapeli kabisa..
Tatizo BOT wamekaa kimya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…