BoT, toeni matangazo kupitia vyombo vya habari kukumbusha kuwa kufanya biashara ya kukopesha mitaani bila leseni ni kosa la jinai

Hawawezi kwenda bank, bank zina vgezo. Siku hizi kuna mikopo ya halmashahuri. Waipambanie hiyo.
 
Mkuu Salary Slip naamini BoT wamekusikia. Najua kuna Mkurugenzi mpya wa Usimamizi wa Sekta ya Fedha, very active, hataacha hili lipite bila kulifanyia kazi kama kuna ukweli. Najua anatembeleaga humu.
 
Mkuu Salary Slip naamini BoT wamekusikia. Najua kuna Mkurugenzi mpya wa Usimamizi wa Sekta ya Fedha, very active, hataacha hili lipite bila kulifanyia kazi kama kuna ukweli. Najua anatembeleaga humu.
Huyu mkurugenzi mpya inampasa kuangalia na wakopeshaji. Hawa watu wanakpesha sekta iliyoshindikana bank. Mtu hakopesheki sekta rasmi wala hana makazi ya kudumu, hana uthibitisho wa kuwa biashara yake inalipa na ana uwezo wa kurudisha hiyo fedha still kampuni inafunga macho kumwezesha halafu akisumbua hataki asumbuliwe anataka atetewe sababu kakwama.
 
MWIZI PEKEE NDIYE ANAOMBA UFANIKIWE ILI AKUIBIE OVER
 
Reactions: Tsh
Hawa ambao hawana leseni hawatoa mikataba kwasababu wanajua itakula kwao.
Ukishaona hakuna mkataba usichukue hiyo pesa au itakula kwako. Mtu ametafuta pesa yake kwa shida ww unataka uichukue tu bila mkataba halali? Hata akili hutumii? Serikali ina kazi sana.
 
Biashara ya mkopo usipokaza wateja wanakufilisi huku wanacheka, kuhusu leseni wengi wanazo hiyo sheria ya Microfinance Act 2018 na Kanuni zake za 2019 zinatoa nafasi hata kwa watu binafsi kutoa mikopo (individual money lender) ujanja ujanja unazidi kuisha tukikopa tujitahidi walipa wenye mitaji yao
 
Reactions: Tsh
Ni kweli. Ukikopa ukalipa sidhani kama kuna tatizo. Matatizo yote yanaanza pale unapokopa halafu usilipe na unataka ueleweke kuwa umekwama hivyo unatakiwa kulindwa.
 
Hawawezi kwenda bank, bank zina vgezo. Siku hzi kuna mikopo ya almashahuri. Waipambanie hiyo.
Basi uzi ungepaswa uwe wa kuwaasa hao wanaowakopa street guys wakakope hiyo ya halmashauri kuepuka riba kubwa na kupata sheria za kuwalinda maana street guys wao pia wanaangalia maslahi yao pia, na wanajua kabisa wakizembea hawalipwi pia kwa kuwa hawana sheria za kuwalinda.... Kingine hao wamama sometimes wanafeli sana unakuta anafurahia kukopa alafu kulipa hataki ndo unakuta mwisho wa siku anazalilishwa
 
Basi uzi ungepaswa uwe wa kuwaasa hao wanaowakopa street guys wakakope hiyo ya halmashauri kuepuka riba kubwa na kupata sheria za kuwalinda
Kabisa boss. Serikali pia ingeweka ukomo wa dhamana kwa microfinance. Mfano sheria ikataze kuweka dhamana ya nyumba kwa microfinance zenye mtaji chini ya m500, na kwa wenye mtaji huo kuwe na mfumo maalum wa kufata. Asitokee mtu akapoteza nyumba kwa pesa ndogo.
 
I Umeshakopa mtaani sasa unatafuta njia ya kudhulumu fedha za watu, nenda kalipe mkuu acha hizo, ulikopa kwa amani nenda kalipe kwa amani serekali inatatambua ya kwamba wapo wanaokopeshana kidugu mitaani kwa dharura mbalimbali za kijamii.
 
Mnatia umasikini wamama wa watu. Hii biashaara imekuwa holelala kuliko holelala yenyewe.
Kwanini hawaendi kwenye mabenki husika, Kwanini mchezo ya Akina mama ya kupeana fedha imekubuhu mitaani? Ipo shida pahala fulani bank ndizo zilipaswa kutoa solutions za maswala yote ya kifedha kwa watanzania mpaka ikaanzishwa TWB sijui kama bado ipo, BANK ZETU ZILEGEZE MASHARTI NA WA TANZANIA HAWATAKI VIJITAASISI ENDAPO BANK ZITAKUWA RAFIKI.
 
Kitu ambacho akiwezi kutokea iziofic kufungwa kwasababu wakopaj wenyew wanavipenda ila wakikosa ela ya rejesho ndo wanakumbuka kuwa riba nikubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…