DOKEZO Boti inayosafirishwa kutoka Mtwara kwenda Mwanza ni Kero barabarani. Waichinje wasafirishe Vipande

DOKEZO Boti inayosafirishwa kutoka Mtwara kwenda Mwanza ni Kero barabarani. Waichinje wasafirishe Vipande

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Rafael logistics hao wamelewa kibali toka wizarani ,Una lingine?
Kwahiyo Serikali ikifanya kitu kinakuwa sahihi? Yaani mfanyakazi wa Serikali akifanya maamuzi ya kutoa kibali ni sawa na Mungu kasema sio?
 
Kuna Boti inasafirishwa kutoka Mtwara Kwenda Mwanza. Itatumia muda wa Mwezi mmoja au zaidi, kutumia barabara ni kutojali watumiaji wengine wa barabara.

Kama umekutana nayo, hii Boti ni Kero sana. Najiuliza kwanini haijasafirishwa Vipande? Mzigo kama huu unatakiwa Uchinjwe ndo usafirishwe
View attachment 3358312
View attachment 3360031
Kuna wakati Marehemu Magufuli alishakataa kutumia Barabara kusafirisha Boti kubwa hivi.

Mzigo huu wa abnormal umeanza safari jana tarehe 05.06.2025 leo tumekuata nalo Ndanda. Unatoka Mtwara kupitia Ruvuma - Njombe - Iringa - Morogoro - Dodoma - Singida - Tabora - Shinyanga - Mwanza

VIPIMO
Urefu mita 29
Upana mita 5.6
Kimo mita 7.4

Kwa upande wangu naona si sawa. Barabara zetu nyembamba sana.
View attachment 3358313
Hii picha ni ya leo wakiwa wamefika Ndanda. Kisa kaomba kibali.

TUPEANE UPDATES

Kutoka Mtwara
View attachment 3359185
📍Leo tarehe 07/06/2025 Masasi Stand mataa saa 13:05
Uelekeo Lake Zone.
Km 200 Siku 3 😂😂
View attachment 3359973
VIWANGO VYA UPANA WA BARABARA NCHINI TANZANIA
Kwa mujibu wa Kanuni ya 27 ya Kanuni za Sheria ya Barabara yam waka 2007
I. Upana wa lane (saiti) kila upande ni kama ifuatavyo
(a) Barabara Kuu, mita 3.25
(b) Barabara za Mikoa, mita 3.25
(c) Barabara za Wilaya, mita 3.1
II. Upana wa Hifadhi ya Barabara (Road Reserve) ni kama ifuatavyo
(a) Barabara kuu, ni mita 30 kila upande kutoka katikati ya barabara kwa barabara zenye single varriage way.[ yaani kila upande inaenda gari moja]
(b) Barabara kuu zenye dual carriageway, [yaani zinaenda gari mbili kila upande], ni mita 30 kila upande kutoka katikati ya dual carriageway
(c) Barabara zinazolisha barabara kuu (feeder roads) ni mita 15 kila upande.
III. Hifadhi ya barabara kuu ya morogoro (Morogoro road) ni kama ifuatavyo ikipimwa kutoka makutano ya barabara ya Umoja wa mataifa
(a) Km 10-16 ni mita 90
(b) Km 16-37 ni mita 120
(c) Km 37-69 ni mita 60
(d) Km 69-70, ni mita 60 (daraja la ruvu)
(e) Km 90 na kuendelea, ni mita 60
Kwanza huu usafiri ni wa kawaida na hii sio mara ya kwanza,kuichinja gharama yale ni sawa na kutengeneza meli 2 njia ya kupitia mombasa kija kisumu na kuiweka kwenye ziwa,upande wa kenya wanalipisha gharama kubwa sana.
 
Asante kwa ufafanuzi Chief,

Hivi yale madaraja membamba ya hiyo barabara ya Old Shinyanga-Bubiki yalishajengwa mapya!

Nilijua hiyo barabara imetelekezwa baada ya ujenzi wa lami kupitia Maganzo.
Mengi yalishajengwa na lami imeshafika mbali.Uwa inajengwa kila mwaka kwa awamu kilomita kadhaa na madaraja kadhaa.
 
Sasa picha ya samia inafanya nini hapo mbele ya gari. Ama kweli Hauziki
Ili wasisumbuliwe. Hata watu wenye maovu wengi wanaweka Bendera ya CCM ili wasisumbuliwe na Mamlaka. Hata wewe gari ikipata tatizo ukiwa mbali, bandika picha ya Samia na Bendera ya CCM. Hutasimamishwa na mtu.

Ukiona hivyo kuna kitu hakipo sawa.
 
Kutoa tu boti toka mtwara kwenda Mwanza nayo lazima waingize siasa,hapo lengo lao kuonyesha mama anaupiga mwingi
 
Inawezekana, lakini bado gharama kubwa sana.
Mfizikia kumbuka hesabu za secondary education hasa o-level za linear programming maximization applications.
Oky oky mkuu kweli hapo nimeelewa
 
Wametumia njia ndefu sana wangeishushia mombasa kisha iende hadi Kisumu ni karibu wangetumia siku tano kwa gharama nafuu
Kisha Kisumu Mwanza
daah umemaliza mkuu sema watu watakula wapi sasa??? unajua imwchukua bilioni ngapi hapo kusafirisha??
 
Achana na shida ya gharama kubwa.
Mimi pia mfizikia niliesoma na mambo ya aviation. Nimesoma Aerodynamics, Meteorology, n.k.
Huwezi kufanya long-haul flight yani umbali mrefu unaning'iniza mzigo kwa helicopter hata ziwe 10 ni hatari.

Upepo mkali ukiwakuta hewani hapo katikati ya safari inaweza ikatokea catastrophe, disaster kubwa. Kiasi kwamba mnaweza kupoteza helicopters zote, boat lenyewe na watu.
Mkuu acha masikkhara wewe umesoma
Aviation
Aerodynamics
Plass meterology
Seriously maaana natafutaga watu wa namna hii yaan kiufupi napenda sana kufatilia haya mambo mkuu nimekua nikimsumbua sana faza flan ambaye ni fundi wa ndege.

Kama ndio hvo mkuu naomba niwe nakuuliza baadhi ya mambo ili niongeze ujuzi zaidi ili hapa kijiweni nisikose cha kuchangia ... Maana kila siku mi ni story za mishangazi
 
Kasheshe lipo ruvuma to njombe to iringa, wakitoboa hapo basi wamesha fika, sasa hiko kipande kina ndege za makaa ya mawe muda wote zipo online, msije okota mifupa, unakuta dereva kachoka kamuachia tandiboy
hivi huo mzigo ukifika kwenye kona kalii likapindukaa nani atadaiwa???
 
Lengo wananchi waone boti aliyonunua mama 😀 😀 😀 muhimu sana hiyoo
 
Kuna Boti inasafirishwa kutoka Mtwara Kwenda Mwanza. Itatumia muda wa Mwezi mmoja au zaidi, kutumia barabara ni kutojali watumiaji wengine wa barabara.

Kama umekutana nayo, hii Boti ni Kero sana. Najiuliza kwanini haijasafirishwa Vipande? Mzigo kama huu unatakiwa Uchinjwe ndo usafirishwe
View attachment 3358312
View attachment 3360031
Kuna wakati Marehemu Magufuli alishakataa kutumia Barabara kusafirisha Boti kubwa hivi.

Mzigo huu wa abnormal umeanza safari jana tarehe 05.06.2025 leo tumekuata nalo Ndanda. Unatoka Mtwara kupitia Ruvuma - Njombe - Iringa - Morogoro - Dodoma - Singida - Tabora - Shinyanga - Mwanza

VIPIMO
Urefu mita 29
Upana mita 5.6
Kimo mita 7.4

Kwa upande wangu naona si sawa. Barabara zetu nyembamba sana.
View attachment 3358313
Hii picha ni ya leo wakiwa wamefika Ndanda. Kisa kaomba kibali.

TUPEANE UPDATES

Kutoka Mtwara
View attachment 3359185
📍Leo tarehe 07/06/2025 Masasi Stand mataa saa 13:05
Uelekeo Lake Zone.
Km 200 Siku 3 😂😂
View attachment 3359973
VIWANGO VYA UPANA WA BARABARA NCHINI TANZANIA
Kwa mujibu wa Kanuni ya 27 ya Kanuni za Sheria ya Barabara yam waka 2007
I. Upana wa lane (saiti) kila upande ni kama ifuatavyo
(a) Barabara Kuu, mita 3.25
(b) Barabara za Mikoa, mita 3.25
(c) Barabara za Wilaya, mita 3.1
II. Upana wa Hifadhi ya Barabara (Road Reserve) ni kama ifuatavyo
(a) Barabara kuu, ni mita 30 kila upande kutoka katikati ya barabara kwa barabara zenye single varriage way.[ yaani kila upande inaenda gari moja]
(b) Barabara kuu zenye dual carriageway, [yaani zinaenda gari mbili kila upande], ni mita 30 kila upande kutoka katikati ya dual carriageway
(c) Barabara zinazolisha barabara kuu (feeder roads) ni mita 15 kila upande.
III. Hifadhi ya barabara kuu ya morogoro (Morogoro road) ni kama ifuatavyo ikipimwa kutoka makutano ya barabara ya Umoja wa mataifa
(a) Km 10-16 ni mita 90
(b) Km 16-37 ni mita 120
(c) Km 37-69 ni mita 60
(d) Km 69-70, ni mita 60 (daraja la ruvu)
(e) Km 90 na kuendelea, ni mita 60
Chuma JPM asingekubali huu upuuzi
R.I.P #CHUMAJPM#
 
Back
Top Bottom