DOKEZO Boti inayosafirishwa kutoka Mtwara kwenda Mwanza ni Kero barabarani. Waichinje wasafirishe Vipande

DOKEZO Boti inayosafirishwa kutoka Mtwara kwenda Mwanza ni Kero barabarani. Waichinje wasafirishe Vipande

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii ni Ambulance ya gharama kwa ajili ya wananchi wanaopata tabu kule ziwani kupeleka wagonjwa pale Bugando na nadhani ni mali ya serikali, kushusha Mtwara inategemea na meli iliyoleta kituo ni wapi, kupitia Tanga au Dar kuna madaraja ya reli na flyover pale Hale na Ruvu, kupitia Mombasa kwanza yapaswa kuangalia usalama na utulivu wa nchi husika na mahusiano ya kidplomasia kwa wakati tulionao, na kutumia njia ya anga gharama ni kubwa, nadhani hayo yote yalifanyiwa tathmini kabla ya kuanza safari.
 
Napenda kufuatilia safari ya huu mzigo, wakuu hii boti imepita wapi kwa sasa, tupeni picha waliyokutana nayo njiani, niko Morogoro naisubiri.
Haiwezi kupitia Morogoro kama inapitia njia ya Ruvuma na Njombe... Makambako-mafinga-iringa-dodoma-singida-tabora-shinyanga-mwanza
 
Kuna Boti inasafirishwa kutoka Mtwara Kwenda Mwanza. Itatumia muda wa Mwezi mmoja au zaidi, kutumia barabara ni kutojali watumiaji wengine wa barabara.

Kama umekutana nayo, hii Boti ni Kero sana. Najiuliza kwanini haijasafirishwa Vipande? Mzigo kama huu unatakiwa Uchinjwe ndo usafirishwe
View attachment 3358312
View attachment 3360031
Kuna wakati Marehemu Magufuli alishakataa kutumia Barabara kusafirisha Boti kubwa hivi.

Mzigo huu wa abnormal umeanza safari jana tarehe 05.06.2025 leo tumekuata nalo Ndanda. Unatoka Mtwara kupitia Ruvuma - Njombe - Iringa - Morogoro - Dodoma - Singida - Tabora - Shinyanga - Mwanza

VIPIMO
Urefu mita 29
Upana mita 5.6
Kimo mita 7.4

Kwa upande wangu naona si sawa. Barabara zetu nyembamba sana.
View attachment 3358313
Hii picha ni ya leo wakiwa wamefika Ndanda. Kisa kaomba kibali.

TUPEANE UPDATES

Kutoka Mtwara
View attachment 3359185
📍Leo tarehe 07/06/2025 Masasi Stand mataa saa 13:05
Uelekeo Lake Zone.
Km 200 Siku 3 😂😂
View attachment 3359973
VIWANGO VYA UPANA WA BARABARA NCHINI TANZANIA
Kwa mujibu wa Kanuni ya 27 ya Kanuni za Sheria ya Barabara yam waka 2007
I. Upana wa lane (saiti) kila upande ni kama ifuatavyo
(a) Barabara Kuu, mita 3.25
(b) Barabara za Mikoa, mita 3.25
(c) Barabara za Wilaya, mita 3.1
II. Upana wa Hifadhi ya Barabara (Road Reserve) ni kama ifuatavyo
(a) Barabara kuu, ni mita 30 kila upande kutoka katikati ya barabara kwa barabara zenye single varriage way.[ yaani kila upande inaenda gari moja]
(b) Barabara kuu zenye dual carriageway, [yaani zinaenda gari mbili kila upande], ni mita 30 kila upande kutoka katikati ya dual carriageway
(c) Barabara zinazolisha barabara kuu (feeder roads) ni mita 15 kila upande.
III. Hifadhi ya barabara kuu ya morogoro (Morogoro road) ni kama ifuatavyo ikipimwa kutoka makutano ya barabara ya Umoja wa mataifa
(a) Km 10-16 ni mita 90
(b) Km 16-37 ni mita 120
(c) Km 37-69 ni mita 60
(d) Km 69-70, ni mita 60 (daraja la ruvu)
(e) Km 90 na kuendelea, ni mita 60

mkiambiwa tatizo ni uislamu wa tanzagiza mnasema sijui udini ona sasa, hivi unafikiri Magu angekuwepo wangeshindwa kutafuta suluhisho la kuifikisha hiyo meli mwanza? kwanza gharama tu wanaoyutumia hapo achilia mbali risk za ajali kuharibika nina uhakika mpaka kufika watahitaji kuleta wahandisi walioitengeneza kufanya repair Magu lazima angekuja na suluhisho tu.

kumbuka hiyo meli walitoa oda, ikaundwa wakalipa na lkn hawakufikiria wataisafirishaje? …
 
Ujenzi SGR ukikamilika ndiyo mwisho wa hii abnormal!

Pale reli ina-cross barabara kwa juu hii mizigo itapitishikaje?
Hivi inapita wapi
Mtwara
Songea
Njombe
Makambako - Mbeya au
Makambako - Iringa
Wakipita Mbeya - Uyole kuna daraja la TAZARA juu,
Wakipita Dodoma na Mwanza kuna SGR juu
 
Haiwezi kupitia Morogoro kama inapitia njia ya Ruvuma na Njombe... Makambako-mafinga-iringa-dodoma-singida-tabora-shinyanga-mwanza
Morogoro linapita kuja Dodoma,, Iringa to Dodoma road limeacha kwa sababu ya Daraja la Mtera ni jembamba.
 
daah umemaliza mkuu sema watu watakula wapi sasa??? unajua imwchukua bilioni ngapi hapo kusafirisha??
Boti yenyewe ni ambulance ya serikali so per diem za kutosha hapo mwezi mzima lazima mtu amalizie nyumba.
Inakwenda kutoa huduma za dharura za afya visiwani kabla ya kufikishwa hospital kuu ya Bugando hakika inakwenda kuokoa uhai
 
Hii ni Ambulance ya gharama kwa ajili ya wananchi wanaopata tabu kule ziwani kupeleka wagonjwa pale Bugando na nadhani ni mali ya serikali, kushusha Mtwara inategemea na meli iliyoleta kituo ni wapi, kupitia Tanga au Dar kuna madaraja ya reli na flyover pale Hale na Ruvu, kupitia Mombasa kwanza yapaswa kuangalia usalama na utulivu wa nchi husika na mahusiano ya kidplomasia kwa wakati tulionao, na kutumia njia ya anga gharama ni kubwa, nadhani hayo yote yalifanyiwa tathmini kabla ya kuanza safari.
Umeeleza vizuri boss,wabheja
 
Umasikini tu tunauendekeza, maantonov yamejaa Ulaya ndio kazi zake hizo heavy loads, wangenipa mimi hilo deal chapu mzigo wao ungekuwa Mwanza Airport.

Hiyo boat ni ndogo sana, ilitosha kudesign au kukodi wheeled trailler la kuvuta halafu unavuta na horse, wangekwenda kwa speed na wangepunguza height kwa kiasi kikubwa.

Yaani hiyo decision ni watu kabisa wamekaa planning meeting na kuchagua hiyo option, unatembea na watu na miti kunyanyua nyaya za umeme? Aisee wajitafakari.
Watu mnafahamu Mambo,daaaa
 
Back
Top Bottom