Botswana imefanyaje kufikia hatua hii?

Ipo siri kubwa kwenye madini ya nchi yetu
Siku ikifika wananchi wakajua ni kwa kiasi gani nchi inanyonywa kwenye madini
Siku wananchi wakigundua nchi yetu hii ina uwezo wa kuendeshwa na madini tu na mambo mengine yakaenda vizuri

Sadly siku hii haitafika
 
Nchi hii Viongozi hawatufai. Sijui kama wanaingia huku na kuona namna wananchi wanavyowatazama. Kuwajibishana ni MSAMIATI mgumu sana!! Hivi ni kwanini? Au watu wanakula pamoja!!? Kwanini Tunashindwa kuwajibishana??

Eeh Mwenyeezimungu Mwingi wa Rehma ninakuomba uwawajibishe Viongozi wabadhirifu pale wanaposhindwa kuwajibishana!! Tazama namna wananchi wa Nchi hii wanavyoteseka huku wachache wakijinufaisha fedha za walipa kodi!!!
 
Shida ya Burundi Iko wazi hakuna usalama na utulivu wa Kisiasa kama Rwanda so Bado nao wanajitafuta.

Wakisettle Kisiasa Burundi Ina nafasi kubwa ya kuendelea kuzidi hata Rwanda maana wanasema Ina Ardhi nzuri ya Kilimo,Madini na beaches.
Ok
Sijakuelewa. Una maana Rwanda Wana ardhi kubwa ya kilimo. Be serious ukubwa wa Rwanda ni kama mkoa mmoja wa Tanzania wewe unakuja kudai Wana eneo kubwa la kilimo. Rwanda chakula Wana import kutoka Uganda Kenya Congo au Tanzania
 
Mzungu kwa kenyata alikuwa kama mchepuko tu.... Lakini bwana Khama alichukua Ruth kama mke halali... Hivyo heshima ya bwana Khama ni tofauti na Kenyatta kwa wakweze
 
Sasa hapo si kama M.city upige picha usiku tu,au Makumbusho usiku achana na posta
 
Ikija kuleta faida nitakula mavi yako
Nimesema kama atatokea kiongozi mwenye weledi kuendesha huo mradi.
Basi italeta faida.
Je huyo kiongozi yupo!?
Kanda ya kati na kanda ya ziwa yote hutumia reli kwa asilimia kubwa kusafirisha mizigo.
Raia wengi wa kanda ya kati na ziwa husafiri kwa reli.
Uganda,Congo,Burundi hawana bandari kama tutaweka ufanisi kwa SGR na tukaingia nao makubaliano kuwasafirishia mizigo yao kwa hii reli faida itaingia kubwa pia.
Maana behewa moja yaweza beba mzigo wa lori tatu tena ukiweka double stock hata mzigo wa lori tano unabeba kwa behewa moja.
Lori hutembea kwa spidi ndogo jumlisha foleni jumlisha kupumzika njiani.
Kama SGR ikitumika kwa UFANISI NA WELEDI zingatia hizo kauli mbili,basi faida itakuwepo.
Shida ndio Tanzania hatuna viongozi wenye weledi.
 
Tzn Ina Rasilimali za kuunga unga ndio maana huwezi ona serious investors wakiweka pesa
Tanzania haina rasilimali za kuunga bali viongozi wapigaji.
Huwezi sema rasilimali za kuunga ilhali kuna viongozi wezi huingia mikataba ya kipumbavu na wawekezaji wezi wa kihindi na pesa zinapigika.
Janja janja zikiachwa basi tutafika mbali,ila ni UTOVU WA NIDHAMU KWA MUNGU ukisema Tz kuna rasilimali unga mwana.
Kuna tukio wazee wa reli walinieleza nilichoka sana akili na nikalegea.
Hii reli ya SGR kama kusingekua na wazee wa kudai ten pasenti alikua ajenge Iran kwa bei nafuu na rafiki.
Ila kisa Iran kakataa kutoa ten pasent kwa mtangaza zabuni basi akanyimwa tenda wakapewa waliokubali kutoa ten pasenti.
Hili taifa la hovyo sana.
 
Ni nchi kubwa kieneo lakini sehemu wanakoishi watu ni sehemu ndogo. Umeshawahi kufika Botswana kwanza ili tuongee ukiwa na ufahamu.
Ningejua km izo Kama sijafika. Udogo wa watu au wingi wa watu hauna maana kimantiki. Sawa ni watu wadogo na wachache na kubali. Kwahiyo unaona wingi wa watanzania ndiyo kunafanya tuwe tulivyo? Kwa china tunaingia Mara ngapi kwa wingi? China ina watu billion Moja na milioni mia mbili. Basi ndiyo wangekua masikini zaidi duniani Kama kuwa wengi ni kuwa masikini na udogo wa watu ndiyo kuwa na uwezo. Narudia kubali kataa Uongozi Bora wenye maono na uzalendo wa kweli ndiyo chimbuko la maendeleo kwa nchi zote duniani.
 
Sawa
 
Nashukuru kwa ufafanuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…