Ukiacha hicho mnachoita wizi ila binafsi ukiniuliza Kwa nini tuna maendeleo ya kusuasua nitakwambia tuna shida ya kuchagua vipaombele na pia kufanya mambo kiujumla Jumla.
Mfano mdogo ni kwenye Barabara.Tunahitaji Barabara zaidi kuifungua Nchi kuliko miundombinu mingine ya usafiri.
Lakini hapo hapo kwenye Barabara tunatapanya Rasilimali bila kuwa na Barabara za vipaombele utakuta Kila Mkoa tunajenga vibarabara vya km 10,6,6,15,30,8,50 nk wakati tungekuwa na Barabara kadhaa za vipaombele zingeisha Kwa wakati zinaendelea Kuzalisha na tunahamia kwingine.
Angalia hapa yaani Waziri anaenda kuweka Jiwe la msingi Barabara ya km 6 out of 60 zinazoktakiwa Sasa hizi ni akili au ujinga wa Watanzania?
View: https://twitter.com/WizarayaUJ/status/1776596912470139079?t=WAehp_fLCnWhiGbT7Xhi8Q&s=19
Nchi haiwezi kuendelea Kwa utaratibu wa kutapanya Rasilimali Kwa maslahi ya Kisiasa Kwa sababu ya watu wajinga.