Botswana ndio wamechagua huyu wakamuacha Progressive Masisi?! Majanga matupu

Botswana ndio wamechagua huyu wakamuacha Progressive Masisi?! Majanga matupu

Demokrasia wakati mwingine huwa inaleta vitu vya ajabu sana, ni kama hamna kitu humo kwa huyo Rais mpya wa Botswana, ila ndio hivyo raia wakishachoka huwa wanasema bora wapigie hata jiwe kura kuliko establishment.

View attachment 3147305
View attachment 3147306
Mkuu ni mkewe? Naskia jamaa anaungwa mkono na bwana sata.
Halafu huenda wanawake kupiga magoti ni utamaduni wao labda.
Nenda uganda hapo, mwanamke anapga goti hadi cha kwa mwanaume.
 
Heri huyu kuliko mtukufu Mungu wa Danganyika ambaye anaweza kila kitu japo hawezi. Heri huyu ananyenyekewa lakini hafugi chawa. Heri yake anamuinua huyo binti kuliko mama anayezamisha kila mmoja isipokuwa familia yake. Pia, mfanyie utafiti Masisi ujue ni kwanini amebwagwa.
 
Kwani kuna shido gani
Mwanamke kumpigia magoti mumeww kawaida sana kwa afrika
 
Kama wanaharakati mnakiri kuwa Demokrasia sio mfumo mzuri maana unaweza kuleta matokeo mabaya, kama haya.

Naamini mataifa makubwa kama Russia na Uchina wamejifunza na kuona sio mfumo mzuri kiutawala.

Tuepushwe tu na wehu kama hawa maana mmekiri wenyewe , demokrasia inaweza tuletea wehu.
 
Huyu Rais mteule simjui sana ila Masisi ndio nilikuwa namjua na aliyemtangulia Ian Khama , baada ya Masisi kumrithi Khama ulizuka ugomvi mkubwa baina yao na kukipasua chama chao hadi wakapoteza madaraka.
Asa mbona umemponda kumbe hata kumjua humjui wala sera zake huzijui
We itakua ni kada wa chadema maana hua akili hakuna nyie .
Chadema nanyi mkitaka mshinde mwekeni kiongozi imara achaneni na harakati hazina tija kwa taifa
 
Hata sisi hapa tulikuwa na tamaduni za kuketa watoto wa kike ili wasiwe na matamanio ya ngono, kuna tamaduni ni za hovyo na kutupiliwa mbali katika dustbin la historia.
Inahusika vipi na mada ,.
 
Kama wanaharakati mnakiri kuwa Demokrasia sio mfumo mzuri maana unaweza kuleta matokeo mabaya, kama haya.

Naamini mataifa makubwa kama Russia na Uchina wamejifunza na kuona sio mfumo mzuri kiutawala.

Tuepushwe tu na wehu kama hawa maana mmekiri wenyewe , demokrasia inaweza tuletea wehu.
Wapi nimekiri demokrasia sio mfumo mzuri wewe kibuyu?,
 
Demokrasia wakati mwingine huwa inaleta vitu vya ajabu sana, ni kama hamna kitu humo kwa huyo Rais mpya wa Botswana, ila ndio hivyo raia wakishachoka huwa wanasema bora wapigie hata jiwe kura kuliko establishment.

View attachment 3147305
View attachment 3147306
Chama tawala cha Botswana, Botswana Democratic Party (BDP), na kushindwa kwake kwa kihistoria, nini kilitokea?

Part 1:
Chama tawala kinachomaliza muda wake, Botswana Democratic Party (BDP), kilipata pigo la kihistoria katika uchaguzi, kikifanikiwa kupata viti vinne tu vya ubunge kati ya 61. BDP imeiongoza Botswana kwa miaka 58 mfululizo hadi leo walipokutana na wakati wao mgumu kisiasa.

Chama cha upinzani kilichoshinda na kuwa chama tawala kipya, Umbrella for Democratic Change (UDC), kilishinda kwa wingi wa viti 35, ikionyesha mabadiliko makubwa katika taswira ya kisiasa ya Botswana. Botswana Patriotic Front (BPF), kinachoungwa mkono na Rais wa zamani Seretse Khama Ian Khama, kilishinda viti vitano vya ubunge, wakati Botswana Congress Party (BCP) ilipata viti 14.

Umbrella for Democratic Change (UDC) ni muungano wa vyama vitatu vya upinzani, ambavyo ni Botswana National Front (BNF) ambacho ndicho chama kikuu katika muungano huo, na kinaongozwa na rais ajaye, Duma Gideon Boko. Vyama vingine viwili katika muungano wa UDC ni Botswana People’s Party (BPP) na Alliance for Progressives (AP).

Ili kuelewa kilichotokea katika uchaguzi huu wa kihistoria ulioleta matokeo ya kushangaza, tunahitaji kuangalia kilichotokea kabla ya hapo, na ndicho nitakachojaribu kuelezea kupitia makala hii, ingawa si kwa kina, lakini ili kumpa msomaji uelewa mzuri wa masuala muhimu.

Nilipokea simu kutoka kwa mwanahabari mmoja wa Afrika Kusini, ambaye pia ni rafiki yangu wa kuaminika kwa miaka mingi, mwezi Machi mwaka jana, akiniambia kuwa rais wa zamani wa Botswana Ian Khama alikuwa akinisubiri nyumbani kwake huko Johannesburg.

Nilifika asubuhi ya katikati ya tarehe 14 Machi na kukaribishwa na wasaidizi wake, walioniongoza hadi chumba cha mapokezi cha nyumba hiyo kubwa na nzuri. Rais huyo wa zamani aliingia, tukasalimiana, na alinifanya nijisikie huru kwa mazungumzo ya kawaida kabla ya kuingia kwenye masuala mazito ya kisiasa ambayo wote tulijua yalikuwa sababu ya mkutano wetu.

Tulizungumzia mambo mengi, ikiwemo muda wake madarakani, majuto yake, na matarajio yake kwa Botswana na ukanda wa Kusini mwa Afrika. Kisha nikamuuliza kama alidhani alifanya uamuzi mbaya kwa kumteua Rais Mokgweetsi Masisi kuwa mrithi wake alipoanza kumteua kama Makamu wa Rais mwaka 2014, akichukua nafasi ya Makamu wa Rais wa awali, Ponatshego Kedikilwe, aliyejiuzulu kwa sababu za kiafya.
 
Part 2:
Utamaduni nchini Botswana daima umekuwa kwa Rais kuteua Makamu wa Rais ambaye kisha huwa Rais ajaye, hivyo kwa maana hiyo, Masisi alikuwa rais kwa bahati tu kwa sababu bila Kedikilwe kustaafu, asingekuwa rais mwaka 2018.

Baada ya kumuuliza rais wa zamani Ian Khama kama alikubaliana kuwa alionyesha hukumu mbaya kwa kumteua Masisi, kwa mtindo wa kawaida wa Ian Khama, hakuzungusha maneno, alikubali na kusema kuwa hata yeye alikuwa amedanganywa, kwani Masisi hakuwa kile alichokuwa amemwamini mwanzoni.

Kama mwanajeshi mstaafu, Khama anajulikana kwa uwazi wake, yeye ni jenerali wa jeshi mstaafu ambaye aliwahi kuwa Kamanda wa majeshi ya ulinzi ya Botswana kabla ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais na rais wa zamani Festus Mogae ambaye alirithi mwaka 2008.

Khama alikiri kujuta kuteua Masisi, na alionyesha kuchukizwa jinsi Masisi alivyoanza kumtesa yeye na wengine wengi kwa kutumia mamlaka ya dola kulipa kisasi. Aliahidi kufanya kazi kurekebisha kosa lake lililompelekea kuwa mkimbizi nchini Afrika Kusini.

Nilimtazama machoni na kumuuliza kama alidhani Botswana Democratic Party (BDP) ingepoteza madaraka. Alinitazama na kusema, “Ndiyo, itapoteza madaraka.” Nilidhani ni jibu la kimazungumzo kutoka kwa mtu aliyevunjika moyo zaidi kuliko uwezekano halisi ambao ungeweza kutokea miezi 19 baadaye baada ya siku hiyo jua lilipokuwa likiwaka Johannesburg, alikuwa sahihi, BDP sasa ni historia, na huenda ikaanguka kama chama cha UNIP cha Zambia na KANU cha Kenya vilivyopoteza madaraka na kufa.

Rais wa kwanza wa BDP na wa Botswana alikuwa Seretse Goitsebeng Maphiri Khama, baba yake Ian Khama, ambaye aliiongoza nchi kutoka mwaka 1966 hadi alipofariki mwaka 1980, mwaka ambao Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ilianzishwa na makao makuu yake kuwekwa Gaborone, mji mkuu wa Botswana.

Tangu wakati huo, Botswana imepata marais wanne baada ya baba mwanzilishi: Quett Masire (1980–1998), Festus Mogae (1998–2008), Ian Khama (2008–2018), na Mokgweetsi Masisi, ambaye aliongoza kutoka mwaka 2018 hadi leo, wakati chama chake kilipokataliwa vikali na wapiga kura wa Botswana, kikifanikiwa kupata viti vinne tu vya ubunge na kumaliza nafasi ya nne katika mashindano ya vyama vinne.

Ian Khama pia anatoka kwenye ukoo wa kifalme, kutoka kabila la Bangwato, na anashikilia cheo cha Kgosi, kinachomaanisha Chifu.

Rais Masisi ndiye rais wa kwanza wa Botswana kutesa mtangulizi wake kwa kutumia taasisi za serikali kama vile mahakama na polisi, huku pia akitumia vibaya vyombo vya usalama kama maafisa wa ujasusi. Hatimaye Ian Khama alikimbilia Afrika Kusini na kuomba hifadhi, akihofia maisha yake kutokana na ukatili wa Masisi na mateso yanayoendelea kupitia matumizi mabaya ya sheria.

Kama alivyonieleza Khama, asili ya kweli ya Masisi haikuwa dhahiri kwake, lakini muhimu zaidi, haikuwa dhahiri kwa ukanda mzima. Hata hivyo, mtu mmoja alijua vizuri sana kuhusu Masisi, rafiki yake Emmerson Mnangagwa, sasa rais wa Zimbabwe, mtawala dhalimu na katili ambaye hana subira kama Masisi kama tulivyoona leo alipokubali kushindwa, jambo ambalo mnangagwa wa Zimbabwe asingefanya isipokuwa kwa kulazimishwa na hatua za umma au jeshi.
 
Hivi kati ya sisi Watanzania tunatawaliwa na chama cha mashetani na waswana walio chagua upinzani ni watu gani wenye majanga.
Yale maneno ya katiba ni vikaratasi au kifo ni kifo tu unadhani wabotswana wangeyavumili na kuendelea kuwa kama makondoo
 
Hata sisi hapa tulikuwa na tamaduni za kuketa watoto wa kike ili wasiwe na matamanio ya ngono, kuna tamaduni ni za hovyo na kutupiliwa mbali katika dustbin la historia.
Kwani hatuna tamaduni za kutembea juu ya wanawake kwenye Kwa baadhi ya watu wa Kusini? Au NI nyani halioni kundule?
 
Part 3:
Masisi alikuwa na tabia ya kumtembelea Mnangagwa kabla ya yeyote kati yao kuwa rais, ilikuwa chini ya rada, na vyombo vya habari vya Zimbabwe havikuandika kuhusu hilo, labda kwa sababu hawakujua, au hawakuona umuhimu wake. Ili kuweka ziara hizo kuwa siri, Masisi alikuwa akikaa na John Bredenkamp, mfanyabiashara mzungu na mfuasi wa ZANUPF aliyeaga dunia mwaka 2020, badala ya kukaa moja kwa moja na Mnangagwa.

Kwa hivyo, uhusiano kati ya Masisi na Mnangagwa haukuwa mpya, ulianza kabla ya wao kuwa marais na ulikuwa dhahiri zaidi walipoanza kupeana msaada hadharani. Ilikuwa bromance ya maumivu kwa WaZimbabwe na Watswana kwani nchi zote mbili zilikuwa zinaharibiwa na watu hawa walipokuwa wanakiuka misingi mingi ya kidemokrasia na walikuwa wakifanya hivyo kwa kutojali kabisa hasa walipokuwa wakifuatilia maadui zao wa kisiasa.

Hii labda inaelezea kiburi cha Masisi, matumizi yake mabaya ya mamlaka ya dola, na mateso yake kwa wapinzani wa kisiasa, ikilingana na matendo ya Mnangagwa huko Harare ambako maadui na wakosoaji wake wa kweli wamefungwa mara nyingi bila idadi.
 
Back
Top Bottom