Kuna brand nyingi tz lakini ukisearch hata google haitambuliki, hawana official website hata weekpedia hawapo je tv hizi ni fake, mfano ni bravo, aboder, mr uk, goodvision, sundar, alitop
Nitoe ufafanuz kidogo kwa uelewa wang wa mambo ya mtandao.
Hzi tv kama goodvision, bravo, national, aborder, mruk, alitop nk hakuna special kiwanda kinachotengeneza hz tv yaan kiwanda special kwa aborder.
Kinachofanyika kinaitwa CUSTOMIZATION yaan tajiri anaenda china anaweka order kiwandani kuwa TV zake zitengenezwe na zichapwe jina analotaka ila kuna minimum quantity ambayo mtu huyo anakuwa anachukua kila mwez au kila baada ya miez 3.
So unakuta kiwanda kimoja kinatoa Brand zaid ya 20 unakuta brand 3 zinakuja TZ, 10 nigeria, 5 kenya nk.
Huduma ya customization inafanyika kwenye product mbalimbali kama electronics, nguo, solar, viatu nk. Customization ata ALIBABA unaweza kufanya na bidhaa zako zikaja kwa jina lako ila kuna wuantity wanakuLIMIT kuchukua ili upate hyo huduma.
China Brand zinazojulikana za TV ni:
TCL
SKYWORTH
HISENSE
Xiaomi (kdogo imeanza kupata support)
Panasonic (skyworth ndio wanazitengeneza kwa sasa).