Brand nyingi za TV za Bongo ni fake

Imani, upendo na miujiza
 
Ukitaka OG nenda kwenye maduka yao kwenye malls na POSTA MPYA sio KARIAKOO
Mfuko uwe umenona, usijekusingizia eti bei ni kubwa kwa ajili ya kulipia frem
 
Ndiyo ujue wazungu wana akili sana. Kila toleo jipya la TV likitoka ananunua. Anauza used Africa kama mtumba anaongezea hela kidogo anavuta mpya. Sasa wewe baada ya miaka 2 imekufa au unatoleo la kichina kama aborder. Ukitaka kununua toleo jipya ujichange tena ununue mpya.
Mzungu ana akili sana. Wewe angalia hata nguo za mitumba.
 
Tech za tv hazibadiliki upesi, mfano hizi flat tv za LED/LCD zipo toka 2006 kama Mainstream, na ukichukua TV highend ya 2006 ukalinganisha na hizi lowend za 2022, ya 2022 inakalishwa.

Na siku mchina akikuharibikia na mfukoni hupo vizuri utamrudia tu huyo Chogo.
 
Kuna brand nyingi tz lakini ukisearch hata google haitambuliki, hawana official website hata weekpedia hawapo je tv hizi ni fake, mfano ni bravo, aboder, mr uk, goodvision, sundar, alitop
Nitoe ufafanuz kidogo kwa uelewa wang wa mambo ya mtandao.
Hzi tv kama goodvision, bravo, national, aborder, mruk, alitop nk hakuna special kiwanda kinachotengeneza hz tv yaan kiwanda special kwa aborder.

Kinachofanyika kinaitwa CUSTOMIZATION yaan tajiri anaenda china anaweka order kiwandani kuwa TV zake zitengenezwe na zichapwe jina analotaka ila kuna minimum quantity ambayo mtu huyo anakuwa anachukua kila mwez au kila baada ya miez 3.
So unakuta kiwanda kimoja kinatoa Brand zaid ya 20 unakuta brand 3 zinakuja TZ, 10 nigeria, 5 kenya nk.
Huduma ya customization inafanyika kwenye product mbalimbali kama electronics, nguo, solar, viatu nk. Customization ata ALIBABA unaweza kufanya na bidhaa zako zikaja kwa jina lako ila kuna wuantity wanakuLIMIT kuchukua ili upate hyo huduma.

China Brand zinazojulikana za TV ni:
TCL
SKYWORTH
HISENSE
Xiaomi (kdogo imeanza kupata support)
Panasonic (skyworth ndio wanazitengeneza kwa sasa).
 
wewe ndio umeongea point bei ya Hisense china ni ghali sana lakn nadhangaa bongo inauzwa bei ndogo sana maana watu washaanza ujanja ujanja.
TCL inch 32 smart mpaka inafika bongo kama unaagiza ni around laki 3.2 ila kariakoo ni 550,000 na wengi wanazikimbia maana bei mkasi.
 
Unaagiza kwa njia gani
 
Ilimradi naliona bunge live fresh tu.. logo hainisumbui hata kama ikiwa ni made in manzese😅😂
Bunge live! Dah binadamu tupo tofauti sana, katika vitu ninavyoona ni upuuzi ni kuangalia bunge au taarifa ya habari.
 
Hii Vp Kwa Matumizi Ya Kawaida Inafaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…