Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Kampuni ya Usafirishaji Makontena, ya Bravo Group Limited Yathibitisha Hakuna Kazi za Kike na Kiume. Madereva Wanawake wa Malori Wapongezwa na Wanawake Wahimizwa Wasichague Kazi
Umetolewa mwito kwa wanawake kote nchini, wasichague kazi, na badala yake wachangamkie kazi zozote wenye uwezo nazo zikiwemo kazi zinazoitwa za kiume, ukiwemo udereva wa mabasi na malori ya mizigo, kwani imethibitishwa wanawake wanauwezo sawa na wanaume kufanya kazi yoyote na baadhi ya wanawake wanafanya vizuri zaidi ya wanaume, zile kazi zilizokuwa inahesabika kuwa ni kazi za kiume kama udereva, madereva wanawake ni madereva wazuri na makini kuliko madereva wanaume.
Wito huo, umetolewa jana (leo) na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Bravo Group na Agricom Africa, Angelina Ngalula, ambaye pia ni mwanamke, katika hafla fupi ya kuwapongeza madereva wanawake wa Bravo Group na Agricom Africa kwa kazi nzuri kuliko hata madereva wanaume.
Angelina Ngalula ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, TPSF, amewapongeza wanawake wote nchini kwa siku ya wanawake duniani na kusema kwenye biashara hakuna kazi za wanawake wala za wanaume, principle ya biashara ni moja tuu, kuzalisha faida, hakuna mwanamke wala mwanaume, biashara ni biashara.
Kuhusu uwezeshaji wa upendeleo kwa wanawake, Ngalula amepingana na kauli ya "wanawake wakiwezeshwa wanaweza", Ngalula amesema wanawake wanaiwezo na wanaweza kwasababu wana uwezo sawa na wanaume na wengine wana uwezo kuliko hata wanaume, ila ili wanawake waweze, kitu wanachohitaji sio nafasi za upendeleo au kubebwa, bali wajengewe uwezo kwa kuwezeshwa kimitaji, ikiwemo mikopo, kuwekewa mazingira bora ya biashara, na kufungunguliwa fursa za masoko, kitu ambacho hata wanaume wanahitaji.
Ngalula amejitolea mfano yeye mwenyewe, japo ni mwanamke, anamiliki kampuni ya usafishaji ya malori ya masafa marefu, ya Bravo Group na kampuni ya zana za Kilimo ya Agricom Africa, inayoongoza kwa kuuza matrekta, zote zinasemwa ni kazi za kiume, lakini yeye ni mwanamke, ameingia huko bila kuwezeshwa kwa mikopo ya upendeleo hivyo kusisitiza wanawanake wanauwezo sawa na wanaume na wengine wana uwezo kuliko wanaume.
Akizungumzia uwezo wa wanawake Angelina Ngalula amemtolea mfano Rais Samia, jinsi anayoonyesha uwezo kwenye baadhi ya mambo kwa kuyaweza mambo mengi ambayo huko nyuma, yalishindikana, na kumalizia kwa salaam za Makampuni ya Bravo Group na Agricom Afrika kumpongeza Rais Samia, kwa kuonyesha kwa vitendo kuwa wanawake wanaweza, na kuwapongeza viongozi wanawake na wanawake wote wa Tanzania.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu, CEO wa Bravo Group na Agricom Africa, Alex Duffar, amewapongeza wanawake wote kampuni hizo kushiriki kikamilifu maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ile Machi 8 na kuwapongeza madereva wanawake na wanawake wengine wote wanaofanya kazi ngumu zilizokuwa zinaitwa za kiume, na kusema madereva wanawake wako makini zaidi kuliko hata madereva wanaume, wawapo barabarani, madereva wanawake hawana zile fujo za madereva wanaume kukimbiza magari hovyo, au kupiga ovateki ovyo, hivyo ni aghlabu sana kwa madereva wanawake kusababisha ajali za kizembe, hivyo madereva wanawake ni madereva salama zaidi kuzidi hata madereva wanaume.
Wakitoa ushuhuda wa kazi ya udereva wa malori ya masafa marefu kwa madereva wanawake, madereva Asha Mkumba, Mosi Khalfani Msengwa na Mwajuma Mohammed Mhando, wamesema kazi ya udereva wa malori ya masafa marefu, ni kazi tuu kama kazi nyingine yoyote, madereva wanawake wanaifanya vizuri tuu kama madereva wanaume.
Madereva hao wamesema changamoto pekee ya kazi ya udereva wa malori ya masafa marefu kwa madereva wanawake, tofauti na madereva wanaume, ni changamoto tuu za mfumo dume, ambapo madereva wanawake licha ya kazi ya udereva, bado majukumu ya kifamilia yako pale pale, hivyo mwanamke kama mama wa familia na mke kwa mwenza wake, hupata muda mchache wa kukaa nyumbani kuangalia familia, hutumia muda mwingi kuwa barabarani na safarini, hivyo familia zao na wenza wao kuwakosa nyumbani kwa vipindi virefu.
Changamoto kubwa inayowakabili madereva wanawake na wanawake wengine wote wanaofanya kazi za kiume ni kwa wanawake wenyewe, kuziogopa baadhi ya kazi, haswa kazi zinazotumia nguvu, kwa kuziogopa na kuziona ni kazi za kiume, wakati kiukweli kwa malori ya kisasa, ili kuyaendesha, hauhitaji kutumia nguvu kama kazi ya kubeba zege, unatakiwa kutumia tu akili na kujituma kwa bidii, kwasababu kazi ya udereva inahitaji akili, umakini na kufanya kazi kwa bidii na kujituma.
Pia madereva hao wanawake wamezungumzia mtazamo hasi wa jamii kuhusu kazi udereva wa malori ya masafa marefu, wafikapo zile sehemu za kupumzika kwa kulala kidogo kabla ya kuendelea na safari, madereva wanaume wanatuhumiwa kuwa wahuni kwa kuwa na wapenzi sehemu za kulala magari, na kuna ukweli kwenye sehemu maarufu za vituo vya madereva kupumzika, kunakuwa na pilika pilika nyingi na uwepo wa wanawake wengi wanaojipitisha pitisha kwa madereva, lakini kwa madereva wa kike, hakuna tuhuma kama hizo.
Paskali