Ngambo Ngali
JF-Expert Member
- Apr 17, 2009
- 3,517
- 1,363
Wazee wa mujini najua hili linawezekana kabisa. Natafuta ticket za dili nione mechi ya Brazil na Taifa Stairs, nilikuwa disappointed last time walipokuja Ivory coast, nilinunua ticket za 60,000 mbili na Mzenj wangu! Wakati nanunua ticket pale karibu Steers kule mjini kuna vijana walinifata brother nina ticket za dili nipe hiyo 60,000 nakupa mbili tickets. Nikawa na wasi wasi ila niliambiwa inawezekana ni ticket zenyewe mzee Chilla Tenga huwa anashirikiana na akina Mwakalebela kuwa na ticket za ziada. Niliignore wale vijana kuogopa kupigwa fake.
Tuliingia uwanjani nikiwa nimeshikana mkono na Mzenji. Tukaelekezwa kwenye lile jukwaa husika, nilitegemea kutakuwa na watu wastaarabu maana hata raisi alikuwa hapo kwa VIP. Chakushangaza kulikuwa na jamaa wanakula mahindi ya kuchoma, wachafu chafu hivi, wanaongea hovyo hovyo nadhani pia walikuwa wamelewa pombe za kiasili.
Katika uliza uliza nikaambiwa ujanja wa mjini hizo ticket zao za dili huenda wamenunua ticket za 60,000 kwa buku 10. Na kweli baada ya kuulizia siku ya pili nikaambiwa mjini hapo wajinga ndio wanaoliwa. Kila tukio kubwa huwa kuna mambo ya dili.
Zis time nimeamua nioneka wa mujini nami, nitapata wapi ticket za dili naambiwa kila kitu dili hapo mjini hata ukitaka mega selebriti kuna watu wakuongea nao...
Nataka ticket ya dili siwezi lipia 400,000 hahahaha usawa huu mimi na mzenj
Ticket ya dili
Masa K
Masanilo tulikuwa tunafikiria tukufanye uwe mpangaji kwenye nyumba yetu ya Urithi karibu na ferry kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia Oktoba mwishoni mwaka huu. Hutalipa Kodi yoyote ila sisi warithi ndo tutakulipa kwa kututunzia nyumba yetu, Sasa tena unaleta mambo ya dili bado hata giza halijaingia na unajua nyumba yetu ina vito vya thamani vingi tu. Sasa ukikabidhiwa ile nyumba yetu ya urithi mambo yatakuwaje mungu wangu.
Naomba ukanunue tiketi mbili za bei ya kawaida kwa ajili yako na mzenji wako wananchi tutakuelewa.