BRELA: Kalynda ilipewa leseni ya kuuza vifaa vya kielektroniki

Directors ni kina nani? Wameshatapeli wasio na akili, Serikali inaelewa kabisa kuwa ina raia wa aina gani sijui kwann haiwalindi? Au wahusika wapo ndani ya serikali?
 
Hata matangazo ya ITV , ya hao Kalynda - yalikuwa hayaonekani kwa BRELA ?

Yawezekana ni mradi wa kigogo serikalini , kwa sababu kampuni ina leseni zaidi ya 3 , zote zimetoka serikalini na zinaoneshwa public na pili matangazo ya yalikuwa wimbo ITV
Na je wakitoa leseni hakuna ufuatiliaji kuona kama biashara iliyoombewa leseni ndiyo inayofanyika?

Serikali inayoongozwa na rais anayelipwa mshahara na wananchi, usalama wa mali za wananchi umewekwa rehani na hajali.

Bado mnanishauri tu kkuna serikali na TISS yake nchi hii?
 
Brela wanaibuka kusema hayo baada ya watu kulizwa. BRELA walikuwa wapi siku zote wakati Kalynda wakipiga promo na watu wakijiunga?
Sio kazi ya brela kusaka waalifu bali nikutoa ushirikiano kama walivyofanya
 
Unaongea simple coz hujaliwaπŸ˜…
 
Ni mamlaka gani inajua biashara ni halali na sio halali?

Kwa nini BRELA anatoa leseni?
 
Namsikitikia yule dada whatsapp nilimwambia kalynda ni pyramid scheme akaniambia atakufa ndani ya kalynda, πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„leo hii nahisi anakufa na presha
 
Brela wanaibuka kusema hayo baada ya watu kulizwa. BRELA walikuwa wapi siku zote wakati Kalynda wakipiga promo na watu wakijiunga?

Wote huo ni ujinga wa watu wacha waliwe tu! Wewe uliona wapi hela zinajazwa mfukoni mwako zisizo na jasho? Hata wanaoshinda pesa za betting wanatoa jasho la kuliwa kwanza! Mimi hii nimeipenda sana, wacha wajinga na wapumbavu wakomeshwe ili liwe fundisho kwa siku zijazo! Kalyanda hoyeeee! Kanyaga twende Kalyanda!
 
Kwa hio naweza kwenda kutangaza biashara za.magendo ITV kisa wanafanya biashara za matangazo?

Kama una ubavu nenda mradi kama umelipia watakutangazia tu, moto utakaoupata siyo wa ITV babu!
 
Haya tuimbe woteee....
 
Watzn wanapenda kitonga,acha wapigwe hadi akili zikae sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…