JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 7,808
- 16,972
Hiyo masters ni akiba,na silaha kwa fulsa za siku za usoni,sio hasaraHio pesa aliyosomea digrii na master angekuwa na worksop nzuri tu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiyo masters ni akiba,na silaha kwa fulsa za siku za usoni,sio hasaraHio pesa aliyosomea digrii na master angekuwa na worksop nzuri tu.
Kasome veta,harafu kaombe ajira Songas,bwawa la Nyerere,Vodacom data centre,uone kama utapata,huko wanaenda watu "waliomezeshwa madude"ya vyuo vikuu."veta kozi ya la saba.." sasa ulitaka akae tu asikilizie ajira tu kwasababu ana masters?..binti ka analyse mambo kaona vocational training ni dili kuliko hayo madude mengine mnayomezeshwa kwenye vyuo vikuu...na mtonyo ana piga..
AiseeKasome veta,harafu kaombe ajira Songas,bwawa la Nyerere,Vodacom data centre,uone kama utapata,huko wanaenda watu "waliomezeshwa madude"ya vyuo vikuu.
Watu waliomezeshwa madude,wakiamua kuwa fundi seremala,wanawaza ku supply thamani Ikulu na kwenye balozi,wakati nyie wa veta mtaishia kutengeneza vitanda vya nne kwa sita kwa ajiri ya wateja wenu wa buza,temeke,buguruni
Exactly my point..tatizo hujafuatilia mjadala kuanzia mwanzo...huyo jamaa alikuwa ana ponda kwanini alisoma kwanza hayo madude ya masters then akahamia kwenye useremala...Ila on the side note, elfu kumi ya balozini ndio hiyo hiyo ya raia wa kawaida anaetaka kitandaKasome veta,harafu kaombe ajira Songas,bwawa la Nyerere,Vodacom data centre,uone kama utapata,huko wanaenda watu "waliomezeshwa madude"ya vyuo vikuu.
Watu waliomezeshwa madude,wakiamua kuwa fundi seremala,wanawaza ku supply thamani Ikulu na kwenye balozi,wakati nyie wa veta mtaishia kutengeneza vitanda vya nne kwa sita kwa ajiri ya wateja wenu wa buza,temeke,buguruni
Thanks for this, very InspirationalBrenda, msomi mwenye 'masters' aliyejikita kwenye ufundi seremala
Kote duniani vijana walio wengi wamepata elimu, lakini changamoto kubwa imekuwa ni suala la ajira, hivyo wanaamua kuutumia ujuzi wao kama muarobaini kukabiliana na changamoto hiyo.
Dar es Salaam. “Vijana wengi tukimaliza kusoma tunasubiri ajira, lakini hatuhangaiki kutafuta fursa za kazi, kazi zipo nyingi sana Tanzania, ni vijana kuchakarika kuziona hizo fursa na kuanza kuzitumia,” alisema Rais Samia Suluhu Hassan, Januari 07, 2022 katika maadhimisho ya kilele cha matembezi ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Suala la kusubiri ajira baada ya kumaliza masomo kama alivyosema Rais Samia, ni tofauti kwa Brenda Mihanjo (33). Licha ya kuwa na elimu ya Shahada ya Uzamili ya usimamizi wa masuala ya biashara (Masters), aliiweka kando na kuanza kujihusisha na ufundi seremala.
Mwananchi ilifanya mahojiano na Brenda ili kujua nini kilisababisha ajiingize kwenye kazi hiyo, iliyozoeleka kufanywa na wanaume na pia ni msomi wa elimu ya juu.
Anasema kitu kilichomshawishi kufanya shughuli hiyo ni kupenda bidhaa za mbao asilia.
Anasema kuwa mwaka juzi ndio alijiunga rasmi kwenye ufundi seremala, akijifunza nyumbani na baadaye akaenda Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya ufundi Stadi (Veta) kusomea ufundi seremala kozi fupi ya miezi mitatu.
Anabainisha kuwa alikuwa anavutiwa na jinsi mbao zinavyoweza kudizainiwa bidhaa mbalimbali, hivyo akatamani kufahamu namna vinavyotengenezwa
“Napenda sana bidhaa za mbao asilia, navutiwa na mitindo ya bidhaa mbalimbali watu wanazotengeneza kutokana na mbao na mwonekano wake,” anasema.
Anafafanua: “Kwa kweli nilipata changamoto sana ya kwenye vipimo na ndio kilichonipeleka Veta...Maana kutojua vipimo kulinipa shida ya kuagiza mbao, kuna wakati nilikuwa ninazidisha au kupunguza kwa sababu ya kutokujua vipimo kamili. Kwa kweli sitasahau hili jambo,” anasema.
Hata hivyo, Brenda anasema mwanzoni alikuwa anakutana na changamoto ya watu kutokumuamini kwa sababu ni mwanamke, lakini sasa hivi wameanza kumuamini.
“Hii kazi inachukuliwa ni ya kiume, pia watu wanaofanya useremala wanadharauliwa na kuonekana ni maskini.
“Kwa hiyo wakati naanza watu walikuwa hawaniamini kabisa, mtu anaona akinipa kazi yake nitamharibia, lakini sasa hivi namshukuru Mungu wameanza kuniamini, hivyo napata oda nyingi,” anasema.
Anasema, wapo watu ambao wanamcheka na kumdharau kwa sababu ana elimu kubwa lakini ameamua kuwa fundi seremala, lakini yeye hawajali watu hao.
“Hii ndiyo kazi yangu na ninaichukulia kama nyingine, najua ningeamua kuwa na mgahawa au duka la mavazi hakuna ambaye angeshangaa. Lakini niliamua kuchagua useremala nikiwa na nia ya kuwa na biashara kubwa Tanzania yenye kuzalisha samani na bidhaa nyingine za mbao za kuuza ndani na nje ya nchi.
“Na najua kuwa ni sekta inayolipa kama ikifanywa kwa usahihi. Kwa hiyo kwa ujuzi, elimu na maono niliyonayo kuhusu hii kazi najua naweza kufika sehemu nzuri,” anasema.
Kuhusu mafanikio anabainisha kuwa amefungua karakana yake maeneo ya Chang’ombe mkoani Dar es Salaam pamoja na kuajiri vijana zaidi ya wanne wa kumsaidia kazi.
Mbali na hayo, anasema ameweza kutengeneza samani kwa kampuni mbalimbali pamoja na wazungu.
“Mafanikio sio makubwa, lakini nimefanikiwa kuwa na karakana yangu na pia kuajiri vijana ili wanipe nguvu ya kuzalisha bidhaa nyingi zaidi.
“Lakini pia napata oda nyingi sana kwa sasa tofauti na nilivyoanza na nyingi nazipata kutoka katika mitandao ya kijamii, hususan Instagram,” anasema.
Anaeleza kuwa haikuwa kazi rahisi, lakini alisimamia kile alichokipenda na kuamua kukifanya.
Anasema kuwa alipokuwa anataka kufanya kazi hiyo watu wengi walimkatisha tamaa, lakini yeye alipambania kwa kuwa alikuwa na nia.
“Najivunia sana, kwani nilivyoanza mwanzo na sasa ni tofauti, yaani sio Brenda yule aliyekuwa na vyeti vya elimu ya juu bila cheti cha ufundi seremala.”
Brenda anawashauri wanawake wasikate tamaa na wasimamie mawazo wanayoyaamini kwa sababu hakuna kazi ya mwanamke au mwanamume, vyote vinawezekana, kikubwa ni nia tu pamoja na kujiamini.
Anaongeza kuwa malengo yake ya baadaye ni kuja kufungua kiwanda kikubwa cha kuzalisha samani mbalimbali.
“Niamini mimi hii ndoto ya kuanzisha hiki kiwanda itafanikiwa, tofauti na watu wanavyodhani, kazi ya kuchonga samani ukiwa na soko la uhakika inalipa sana.
“Na nikifanikiwa najua nitatatua tatizo la ajira kwa vijana wengi, hususan wasomi kama mimi ambao wanaamini zaidi kupitia ajira,” anasema.
Hata hivyo, anasema changamoto anayokutana nayo kwa sasa ni mashine ndogo aliyonayo ya kupasulia mbao, hivyo kumlazimu kutoa gharama kupeleka mbao kwenye mashine kubwa.
Brenda anasema kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kupanua karakana yake ili iendane na vigezo vinavyohitajika.
“Nilipumzika kwa muda wa miezi miwili ili kufanya tathmini, kuangalia wapi nilikosea, ili ninapouanza mwaka nianze na kasi na mabadiliko zaidi, na hii itanisaidia kufikia malengo yangu haraka,” anasema Brenda.
Historia yake kwa ufupi
Brenda ambaye ni mama wa mtoto mmoja amezaliwa mwaka 1988 mkoani Dar es Salaam. Alianza elimu ya msingi mwaka 1995 katika Shule ya Msingi Kurasini na baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari Zanaki ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Anaeleza kuwa baada ya kuhitimu kidato cha nne alifaulu na kujiunga kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Tambaza.
Anaongeza kuwa alipomaliza kidato cha sita, mwaka 2010 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akisomea shahada ya awali ya biashara na masoko, na mwaka 2012 alisoma stashahada ya uzamili katika diplomasia ya uchumi.
“Mwaka 2019 nilisoma Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara (MBA), niliyoisoma katika chuo cha Eastern and Southern Afrika Management Institute (ESAMI),” anasema.
Gazeti la mwananchi 10/01/2022
Wazambuli mnataka mjithaminishe kama ana ta*****ko!!!weka picha ya Brenda
Ubarikiwe.Numejifunza kitu kikubwa hapa kwetu TANZANIA. Kwasasa nitakuwa ninashare ishu muhimu katika, kuendeleza taifa langu.
VIJANA tupambane, soko la ajira ni changamoto na ni suala la dunia nzima sio hapa tu TZ.
Ukiwa unatafuta ajira basi jitahidi pia ujue gari, uwe na angalau pasi ya kusafiria, uwe na kaujuzi kadogo hivi, mfano uwe na ABC za maintanance ya PC au hata UMEME nk nk.
Tujitahidi sana muda ambao tunatumia kutafuta kazi, basi pia tuwe tunasoma kozi za online ambazo ni free kama vile excel, PP, Word, Lugha (Chinnese, French etc) hizi kozi hupatikana online tu ambapo unaweza kutenga muda hata kuanzia saa 3 usiku mpaka 4 unalala.
Lingine, tuache tamaa ya kupata mali kwa haraka, hali hii inapelekea hata uaminifu finyu tupatapo kazi. Niseme ukweli kati ya vijana 1000 wenye umri wa miaka 25-35 basi vijana kati ya 10-30 ndio wanamiliki NYUMBA/GARI au hata Mali ambazo tunatamani. Tuwe wavumilivu ikizingatiwa umri wa watu kutusua almost huanzia 40 Yrs so wala msijihisi wakosaji sana.
Tusichague kazi za kufanya, kumbuka ni rahisi kupata kazi ukiwa na kazi. Hakikisha tu kazi ni halali na haitokuvua utu wako. Wengi wamepata kazi walizotamani kupitia kazi za ajabu tu, ila uaminifu na ubunifu wao ukapelekea connection.
Mfano, mimi nina Msc ya Finance lkn nina cheti cha ujenzi (Masonry and Bricklaying) cha miaka m3, pia nina ujuzi wa kurekebisha PC, nyongeza ya hilo, I've a Driving licence, TZ Passport and more over niko najua lugha 5 kwa ufasaha japo sio kwa level kubwa sana ila nazijua (Kireno, Spanish, English, French na Kiswahili). Kwa mantiki hiyo ni ngumu sana mtu kuniwin kwenye hizi Saili mchuzi.
Pia vijana, tuko radhi kutumia muda wetu mwingi kubishania kuhusu ALIKIBA na DIAMOND lkn hatuko tayari kubishania namna ya kutoboa kwenye haya maisha. Hivyo tunageuka mizigo kwa wazazi wetu kila uchao. Wazazi wanaishi kwa stress kisa watoto hawana uelekeo wowote.
Lets us put down hizi bad idea kuwa ukiwa msomi basi hupaswi kubeba zege, kulima, kujenga au hata kuuza duka.
TUBADILIKE.
Ameandikwa kwa sababu amemaliza master vipi wale waliomaliza la7 na kwenda veta kujifunza huo ufundi, si watakuwa mbali zaidi kiufundi kuliko huyo mdada.
Huyo dada ameshindwa kuibadili digrii ya BBA kuwa pesa mpaka kaamua kurudi veta kozi ya la7.
Vocational skill anaweza kujifunza hata ambae hajasoma shule kabisa, sio mchongo wa maana.
Amesoma kozi za ujasilia mali ameshindwa kuwa mjasiliamali kaamua kuwa fundi hivyo wajanja watamtumia kupiga pesa.
Yeye alitakuwa afanye business sio ufundi hatotoboa.
Mihanjo yule wa Philosophy?Nawakumbusha tu huyo demu baba ake ni Professor Mihanjo, na napajua hadi kwao Kinyerezi. Watu wasiache shule wakakimbilia useremala bure!
Mkuu, ahsante sana kwa hii komenti yakoNumejifunza kitu kikubwa hapa kwetu TANZANIA. Kwasasa nitakuwa ninashare ishu muhimu katika, kuendeleza taifa langu.
VIJANA tupambane, soko la ajira ni changamoto na ni suala la dunia nzima sio hapa tu TZ.
Ukiwa unatafuta ajira basi jitahidi pia ujue gari, uwe na angalau pasi ya kusafiria, uwe na kaujuzi kadogo hivi, mfano uwe na ABC za maintanance ya PC au hata UMEME nk nk.
Tujitahidi sana muda ambao tunatumia kutafuta kazi, basi pia tuwe tunasoma kozi za online ambazo ni free kama vile excel, PP, Word, Lugha (Chinnese, French etc) hizi kozi hupatikana online tu ambapo unaweza kutenga muda hata kuanzia saa 3 usiku mpaka 4 unalala.
Lingine, tuache tamaa ya kupata mali kwa haraka, hali hii inapelekea hata uaminifu finyu tupatapo kazi. Niseme ukweli kati ya vijana 1000 wenye umri wa miaka 25-35 basi vijana kati ya 10-30 ndio wanamiliki NYUMBA/GARI au hata Mali ambazo tunatamani. Tuwe wavumilivu ikizingatiwa umri wa watu kutusua almost huanzia 40 Yrs so wala msijihisi wakosaji sana.
Tusichague kazi za kufanya, kumbuka ni rahisi kupata kazi ukiwa na kazi. Hakikisha tu kazi ni halali na haitokuvua utu wako. Wengi wamepata kazi walizotamani kupitia kazi za ajabu tu, ila uaminifu na ubunifu wao ukapelekea connection.
Mfano, mimi nina Msc ya Finance lkn nina cheti cha ujenzi (Masonry and Bricklaying) cha miaka m3, pia nina ujuzi wa kurekebisha PC, nyongeza ya hilo, I've a Driving licence, TZ Passport and more over niko najua lugha 5 kwa ufasaha japo sio kwa level kubwa sana ila nazijua (Kireno, Spanish, English, French na Kiswahili). Kwa mantiki hiyo ni ngumu sana mtu kuniwin kwenye hizi Saili mchuzi.
Pia vijana, tuko radhi kutumia muda wetu mwingi kubishania kuhusu ALIKIBA na DIAMOND lkn hatuko tayari kubishania namna ya kutoboa kwenye haya maisha. Hivyo tunageuka mizigo kwa wazazi wetu kila uchao. Wazazi wanaishi kwa stress kisa watoto hawana uelekeo wowote.
Lets us put down hizi bad idea kuwa ukiwa msomi basi hupaswi kubeba zege, kulima, kujenga au hata kuuza duka.
TUBADILIKE.
Yeah mkuuMihanjo yule wa Philosophy?
Aisee kumbeYeah mkuu
Hata keko wametoboa bila master.Issue sio kutoboa, issue ni kupoteza muda mashuleni halafu anaenda kufanya jambo dogo lisilohitaji hata diploma.Atatoboa tena vizuri tu
Bishara ikishskua atawaachia mafunfi yeyr atageukia upande wa administration na management, uzuri ni kwamba atakua anamanage kitu anschokifahamu hivyo ataweza kuzikabili janjajanja za mafundi wske kwa kiasu kikubwa kama zitakuelwepo.
Imewasaidia wangapi kujipanua ? We unafikiri yeye ndio wakwanza kuwa fundi msomi ? Wasomi wapo kila mahala wala sio issue kubwa.Hiyo elimu itamsaidia sana kujipanua kikazi/kibiashara. Tusisome ili kuwa chini ya wenzetu.
Kwa wabongo mobet type uwy ndy wanawake wa nguvuHuyo ndo mwanamke sasa
Huwa nawashangaa sana watu kuona VETA ndio suluhisho wakati hao wakufunzi wenyewe wa veta hawana jipya.Kasome veta,harafu kaombe ajira Songas,bwawa la Nyerere,Vodacom data centre,uone kama utapata,huko wanaenda watu "waliomezeshwa madude"ya vyuo vikuu.
Watu waliomezeshwa madude,wakiamua kuwa fundi seremala,wanawaza ku supply thamani Ikulu na kwenye balozi,wakati nyie wa veta mtaishia kutengeneza vitanda vya nne kwa sita kwa ajiri ya wateja wenu wa huwa buza,temeke,buguruni
Yule mwenye masterz ya marekani anaeuza makande vipi?Imewasaidia wangapi kujipanua ? We unafikiri yeye ndio wakwanza kuwa fundi msomi ? Wasomi wapo kila mahala wala sio issue kubwa.
Wengine wanauza Azam juisi za ukwaju wamebeba bonge la begi na kuvaa likofia likubwa.
Huyo dada hajaelimika men!
Ameshindwa hata kuanzisha kampuni la mfukoni ? walau kuwa consultant wa biadhara.
Kuna firsa nyingi sana kama una digrii ya BBA.
Acheni kupongezana vitu vya hovyo.
Alisha feli na master yake wala hanishawishi.