Brenda Mihanjo, msomi mwenye Masters aliyejikita kwenye ufundi seremala

"veta kozi ya la saba.." sasa ulitaka akae tu asikilizie ajira tu kwasababu ana masters?..binti ka analyse mambo kaona vocational training ni dili kuliko hayo madude mengine mnayomezeshwa kwenye vyuo vikuu...na mtonyo ana piga..
Kasome veta,harafu kaombe ajira Songas,bwawa la Nyerere,Vodacom data centre,uone kama utapata,huko wanaenda watu "waliomezeshwa madude"ya vyuo vikuu.
Watu waliomezeshwa madude,wakiamua kuwa fundi seremala,wanawaza ku supply thamani Ikulu na kwenye balozi,wakati nyie wa veta mtaishia kutengeneza vitanda vya nne kwa sita kwa ajiri ya wateja wenu wa buza,temeke,buguruni
 
Aisee

Ila nimependa the way unavyothink big...

Cc: Bill Gates
 
Exactly my point..tatizo hujafuatilia mjadala kuanzia mwanzo...huyo jamaa alikuwa ana ponda kwanini alisoma kwanza hayo madude ya masters then akahamia kwenye useremala...Ila on the side note, elfu kumi ya balozini ndio hiyo hiyo ya raia wa kawaida anaetaka kitanda
 
Thanks for this, very Inspirational
p
 
Numejifunza kitu kikubwa hapa kwetu TANZANIA. Kwasasa nitakuwa ninashare ishu muhimu katika, kuendeleza taifa langu.

VIJANA tupambane, soko la ajira ni changamoto na ni suala la dunia nzima sio hapa tu TZ.

Ukiwa unatafuta ajira basi jitahidi pia ujue gari, uwe na angalau pasi ya kusafiria, uwe na kaujuzi kadogo hivi, mfano uwe na ABC za maintanance ya PC au hata UMEME nk nk.

Tujitahidi sana muda ambao tunatumia kutafuta kazi, basi pia tuwe tunasoma kozi za online ambazo ni free kama vile excel, PP, Word, Lugha (Chinnese, French etc) hizi kozi hupatikana online tu ambapo unaweza kutenga muda hata kuanzia saa 3 usiku mpaka 4 unalala.

Lingine, tuache tamaa ya kupata mali kwa haraka, hali hii inapelekea hata uaminifu finyu tupatapo kazi. Niseme ukweli kati ya vijana 1000 wenye umri wa miaka 25-35 basi vijana kati ya 10-30 ndio wanamiliki NYUMBA/GARI au hata Mali ambazo tunatamani. Tuwe wavumilivu ikizingatiwa umri wa watu kutusua almost huanzia 40 Yrs so wala msijihisi wakosaji sana.

Tusichague kazi za kufanya, kumbuka ni rahisi kupata kazi ukiwa na kazi. Hakikisha tu kazi ni halali na haitokuvua utu wako. Wengi wamepata kazi walizotamani kupitia kazi za ajabu tu, ila uaminifu na ubunifu wao ukapelekea connection.

Mfano, mimi nina Msc ya Finance lkn nina cheti cha ujenzi (Masonry and Bricklaying) cha miaka m3, pia nina ujuzi wa kurekebisha PC, nyongeza ya hilo, I've a Driving licence, TZ Passport and more over niko najua lugha 5 kwa ufasaha japo sio kwa level kubwa sana ila nazijua (Kireno, Spanish, English, French na Kiswahili). Kwa mantiki hiyo ni ngumu sana mtu kuniwin kwenye hizi Saili mchuzi.

Pia vijana, tuko radhi kutumia muda wetu mwingi kubishania kuhusu ALIKIBA na DIAMOND lkn hatuko tayari kubishania namna ya kutoboa kwenye haya maisha. Hivyo tunageuka mizigo kwa wazazi wetu kila uchao. Wazazi wanaishi kwa stress kisa watoto hawana uelekeo wowote.

Lets us put down hizi bad idea kuwa ukiwa msomi basi hupaswi kubeba zege, kulima, kujenga au hata kuuza duka.

TUBADILIKE.
 
Ubarikiwe.

Asante Sana kwa muongozo cc Smart911
 

Atatoboa tena vizuri tu
Bishara ikishskua atawaachia mafunfi yeyr atageukia upande wa administration na management, uzuri ni kwamba atakua anamanage kitu anschokifahamu hivyo ataweza kuzikabili janjajanja za mafundi wske kwa kiasu kikubwa kama zitakuelwepo.
 
Mkuu, ahsante sana kwa hii komenti yako
 
Hata keko wametoboa bila master.Issue sio kutoboa, issue ni kupoteza muda mashuleni halafu anaenda kufanya jambo dogo lisilohitaji hata diploma.
Tutumie vizuri muda.
Hio miaka kumi aliotumia kusoma angekuwa mbali zaidi.
Halafu sio peke yake anafanya ufundi wapo wengi tu, hivyo suala kutoboa ni kupambana wala sio kuwa na master, wanaweza kutonoa wasi na master ya shule bali wanauzoefu wa kutosha na kujua A-z za hio biashara.
Kuwepo kwenye game muda mrefu ni factor kubwa ya kuendelea kuliko makaratasi.
Endeleeni kujipa moyo ila muda mmeupoteza sana.
 
Hiyo elimu itamsaidia sana kujipanua kikazi/kibiashara. Tusisome ili kuwa chini ya wenzetu.
Imewasaidia wangapi kujipanua ? We unafikiri yeye ndio wakwanza kuwa fundi msomi ? Wasomi wapo kila mahala wala sio issue kubwa.
Wengine wanauza Azam juisi za ukwaju wamebeba bonge la begi na kuvaa likofia likubwa.
Huyo dada hajaelimika men!
Ameshindwa hata kuanzisha kampuni la mfukoni ? walau kuwa consultant wa biadhara.
Kuna firsa nyingi sana kama una digrii ya BBA.
Acheni kupongezana vitu vya hovyo.
Alisha feli na master yake wala hanishawishi.
 
Huwa nawashangaa sana watu kuona VETA ndio suluhisho wakati hao wakufunzi wenyewe wa veta hawana jipya.
Chunguza assets zetu mitaani utagundua kuwa VETA hawana innovation zozote za maana wanashindwa na wachina wanaobumba assets kwa vumbi la mbao.
Tanzania kuna kila mti wa mbao lakini mafundi wameshindwa kubuni vitu vizuri kushindana na vya nje.
Upo sahihi kabisa.
 
Yule mwenye masterz ya marekani anaeuza makande vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…