Brenda Mihanjo, msomi mwenye Masters aliyejikita kwenye ufundi seremala

Yule mwenye masterz ya marekani anaeuza makande vipi?
Nae hana tofauti na huyu.
Hakuna ubunifu pale ni mamantilie mwenye master.
Alichoongeza pale ni vyombo na mavazi mazuri kitu ambacho hata Shilole kakifanya kwenye mgahawa wake japo hana master.
Tunaendelea kuaminishana kuwa wenye master ni sahihi kuuza makande, kuendesha boda, kuuza mboga mboga, kuuza samski feli.
Binafsi sioni faida ya hizo master bali wamepoteza muda wsmao na pesa zao bure na kuishia kufanya vitu visivyohitaji master.
 
Umuhimu veta ni certification mzee
Unaweza ukawa na skillz kibao ukaleta dizaini za kipekee

Ila unapofika time unataka tenda kwenye mashirika na makampuni wanataks uthibitisho wa kimaandishi na kazi za kuonekana utsjikus unakosa deals

Mimi mwenyewe nina bachelor ila nataka niende veta nikapate abc tu za ufundi fulani halafu nije kitaa nifanye manuva maana access ya mtaji ninayo
 
Wee nawee 🤔

Mambo ya interior designing ni taaluma za watu etii , tena ni biashara kubwa. Tatizo wewe unawaza padogo na exposure huna unaonekana, we unakomalia kumfananisha na mafundi wa keko tatizo.

Taaluma yake ya biashara itamsaidia kukuza biashara yake, kuleta ubunifu n.k

Kuna stage mfanyabiashara hata Kama ni darasa la Saba atahitaji elimu tu ili biashara yake ikue zaidi. Hata Kama hajasoma itabidi aajiri watu wenye taaluma zao.
Ndio maana familia za wakina bakheresa na dewji ziliwapeleka watoto wao shule na vyuo vya gharama ili waje wasimamie biashara. Sasa kwanini wao hawakupotezea elimu kwa watoto wao

Hizo biashara na kampuni kubwa unazoziona zimekuzwa na kusimamiwa na wasomi. Hata Kama mmiliki ni std seven Kuna stages za biashara inabidi utafute watu na utaalamu wao wakushauri n.k amabao ni wasomi pia, wewe std seven unabaki Kama mbeba maono na kuangalia mambo yanaendaje.

Wasomi kinachowafelisha ni uoga wa kuanzia chini na kutake risk tu sio kwamba hawana akili msiwadharau ndio maana std seven wanawategemea kusimamia na kuwaendeshea biashara na kampuni zao.
 
Aliekuambia veta ya darasa la Saba Ni nani ? Yeyote unaruhusiwa kwenda kuchukua ujuzi Fulani.
Yeye ameenda veta kusoma useremala kwasababu alitaka kufanya biashara ya furniture Kuna ubaya gani ?
Au Ulitaka akanunue Vipodozi na nguo China ndio uone biashara ya kisomi ?

Watu Kama nyie ndio mnaofanya wasomi washindwe kujiajiri kutokea chini kwa kuogopa kusemwa na kuchekwa
 
Hahaha wewe akili yako bhana ... kwahiyo unataka aishi kimisheni town na kampuni za mfukoni ?

Yeye kapenda na kavutiwa na idea ya biashara ya kutengeneza na kuuza furniture . Wewe Kama unapenda idea ya consultation fanya wewe , usikariri . Kuna ideas chungu mzima ni wewe tu na umeona fursa gani

Masters yake ya biashara itamsaidia Kwenye biashara yake hiyo
 
We muache aendelee kumcheka m, siku akiskia anauza fenicha zake wizarani na balozi mbalimbali ndio atatia akili.
 
Itamsaidia nini wakati imeshindwa kumsaidia sasa hivi. Wakati uliopo imeshindwa ila in future tense itamsaidia! anamkataba na mungu.
Hakuna chochote hapo ataishi kama mafundi wa keko kina piere liquid. Hio hela ya kununua mitambo ya kiwanda kashindwa kuipata kisha utegemee eti ata win.
In future tense hata mimi nitakuwa raisi, hata wewe utakuwa waziri mkuu but to make the dream become true kuna mziki.
Yani mna gurantee atawin kwani wale mafunfi wadio na master hawatawini?
Suala kubwa hapo ni hio master ni useless, huo ndio ikweli japo mnalemba lemba. Ukute hata kuandika business plan keshasahau.
 
We muache aendelee kumcheka m, siku akiskia anauza fenicha zake wizarani na balozi mbalimbali ndio atatia akili.
Akiuza hata wale mafundi wasio na master watauza. Naomba unielewe kwamba master yake mpaka sasa ipo kwenye sifuri kwani haijamsaidia chochote yani mpaka sasa inasoma negative.
Kuwin kila mtu atawini hata muuza nyanya huko mbele ata win.
Kuwini au kutokuwin hakuna uhusuano na master, jambo la msingi tusipoteze muda kusoma vitu tusivyovipenda huyu dada ni funzo kwa vijana, waangalie passion zao wajitupe huko.
Angeanza miaka 10 iliopita angekuwa mbali kwani amepoteza muda mwingi sana kumbe yeye si wa fani ile ya BBA.
Tjifunze kwa wanamziki na wachezaji wanazikimbilia ndoto zao mapema sana na kufaidi matunda ya kazi zao wakuwa vijana.
Kumbuka umri haukusubiri.
 
Mkuu hivi unaweza kupewa tenda kubwa ya kusambaza assets ukiwa huna kampuni ?
 
Yaani wewe umekaa kinegative negative .....hebu fungua ubongo huoo. Fungukaaa

Unasema angefuata passion yake si ndio huo useremala Sasa anafanya , au neno ufundi seremala limekuchanganya tuseme basi interior designing au sijui furniture making kwa kizungu . Pengine baada ya kujitafuta akagundua mapenzi yake yapo Kwenye useremala ndio ameamua kufanya.

Na kuhusu elimu yake aliyosoma Wala hajapoteza kitu itamsaidia kuendesha na kusimamia kiwanda chake . Au ndio Ulitaka akaajiriwe BOT ndio uone kaitendea haki elimu yake ??
Mawazo yako Ni ya kimasikini na kizamani kwa Nyakati hizi.

Mwenzio kaanzisha karakana na ana mpango wa kuongeza mashine kubwa zaidi ,kaajiri vijana na anakuambia wateja anapata kwa wingi ,sasa si ndio kiwanda hicho. Na anasema amehudumia kampuni kadhaa. Sasa unataka nini hapo ?
Elimu yake imepoteaje Wakati anaitumia kuendesha kiwanda chake

Wewe neno fundi seremala limekuvuruga tu , huyo ni mmiliki wa kiwanda huyo anafanya biashara ya furnitures. Ni namna tu ya lugha sababu ameanzia mwenyewe kutengeneza kwa mikono yake
Ni sawa sawa na mmiliki wa restaurants za KFC tutamuita mpishi japo ni mmiliki wa migahawa si alianza kwa kupika mwenyewe kuku zake.

Sasa wewe sijui Ulitaka afanye biashara gani unayosema iendane na Masters yake aliyosoma ??? Hebu niambiee
 
Wazazi wakiwa na pesa halafu mtoto ana akili, basi ni rahisi sana mtoto kufanya anachotaka.

Yaani mtoto anaenda chuo kuelimika tu, na akimaliza kusoma anarudi kwa wazazi wanamuuliza anataka afanye nini, wanampa mtaji.

Ukiwa mtoto wa tajiri hautakiwi kuhangaika na ajira za chini, unajiajiri tu kwa sababu mtaji na back up ipo. Labda upate kazi za mishahara mikubwa!
 
[emoji122]
 
Yule wa makande ni ujinga wa kiwango cha lami. Unaenda kusoma marakeni nchi ya kibepari ambapo kuna kila biashara ambazo huku Tanzania bado hata kufikiriwa unarudi unauza makande kweli!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…