Brevis Bei nafuu. WHY?

Mawazo tunatofautiana mkuu. Zipo SUV zina sura nzuri zaidi ila sidhani hili ni baya, especially hizi facelifted. Tukubaliane tu labda kwamba sometimes beauty is in the eye of the beholder
Kimuonekano Land Cruiser ina sura mbaya kulinganisha na SUV za BMW, Benz, Audi, VW.

Huo ni mtazamo wangu.
 
Zina shida gani za kiufundi Brevis kwa sababu mi nimetumia kwa miaka karibia minne na tayari ilikuja na km 110,000 toka Japan sijaona shida yake kubwa. Labda uniambie kwamba ina engine kubwa so na mafuta inakula kwa trip za town
hata km inakula mafuta mm bado naiweka BREVIS ni namba One katika saloon
acha wapige kelele, gari inakula mafuta kwani ni bei gani mafuta yameshuka hivyo
gari zikiwa chache na bei ghali ndio zina heshima
waambiwe wapimishe Brevis na Passo au Viits
 
Mimi sizani sana kama yanashida izo..ila nahisi ni magari ambayo fashion yake imeanza kupotea, pia ina engine kubwa ulaji wa mafuta uko juu.

Swala kubwa ni magari ambayo yameingia kwa wingi sana sokoni Tanzania watu wameyachoka ndio maana bei zake ziko chini

Mfano nzuri Toyota alteza, mark x yote bei zake ni izo izo kwa sababu ya fashion na utumiaji mkubwa wa mafuta. Ndio maana hayana soko huwezi uza bei za juu ukilishalitumiaa
 
Unaweza kutaka kutumia oil nzuri mfano ya 50,000 yeye akaweka ya 28,00 utajuaje? Hata asipobadilisha utajuaje kama wewe siyo mzoefu wa magari? Nunua oil &filter na abadilishe ukiwepo.

Hiki ndicho nachofanya mimi, ng’adu kwa ng’adu
 
Niuzie hio gari
 
Nimesoma uzi wote nimegundua
1. Wachangiaji na wajuaji wengi hawana hata gari ya urithi
2. Mtu ana toa uzoefu wa gari bila kuimiliki kasikia tu masimulizi ya gari kwa watu

Niwaambie tu gari ni matunzo, wengi wananunua gari nakufanya service mbovu

Tanzania pia hakuna Mafundi, unaenda gereji unakutana na watoto hajawahi kusomea hata ufundi anatumia experience ya gari jingine kutengeneza lako. Alilokuwa akijifunzia geriji, hana uzoefu

Wengi tunataka gereji uchwara kufanya mantainace kwakuwa ni Cheap

Mwisho wa siku Brevis ni gari nzuri, ila uwe na pesa kuimudu na kuitunza
 
Huelewek kwani unaishi nchi gani?
kiujumla amesema wengi wa wachangiaji humu hawaijui hii gari (Brevis) kwani hawana hata la urithi au la shemeji yake
halafu wanasikia maelezo ya vijiweni
kiukweli hakuna gari ndogo ya safari ndefu yenye starehem mwendo na uhakika barabarani km Brevis, huwezi linganisha na IST, Passo au Harrier,(SUV)
Ni gari isiyotaka nafundi uchwara au wa mitaani, au service ya oil za mitaani za kuchanganya SAE 40 & SAE 90
 
Ave


Average inakula km ngapi kwa liter maana ukiuliza humu, kila mtu anajibu lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…