Brigadier Ahmed Takadiri Kitete: Shujaa aliyepiganisha vita toka Kagera mpaka Koboko alikozaliwa Idi Amin

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Huyu ni mmoja kati ya makamanda walioongoza vita vya Kagera lakini siyo maarufu ktk vyombo vyetu vya habari, lakini ukisoma VITABU mbalimbali vinavyohusu VITA VYA KAGERA utagundua kwamba alikuwa na mchango mkubwa toka mwanzo mpaka mwisho wa vita, yaani toka Mutukula/Kagera mpaka Koboko kijiji alikozaliwa Iddi Amin Dada.

Baada ya majeshi ya Uganda kuvamia ardhi ya Tanzania na kuikalia, Tumainieli Kiwelu [meja jenerali wakati huo] ambaye alikuwa Chief of Staff JWTZ alipewa jukumu la kuandaa majeshi yetu na kuongoza mapigano ya kukomboa ardhi yetu.

Ahmed Takadiri Kitete [kanali wakati huo] ametambulishwa ktk kitabu cha " Vita vya Kagera -- 'kagera hadi arua' "kama mkuu wa mipango ya uamrishaji kivita ktk operesheni ya kuyaondoa majeshi ya Uganda ktk ardhi ya Tanzania.

Ahmed Kitete alipandishwa cheo na kuteuliwa kuongoza Brigade ya Minziro ambayo ilipigana maeneo ya Bushenyi, Kasese, Fort Portal, Hoima, Masindi, Karuma Falls, Pakwach, Bondo, Arua, Yumbe, na Moyo mpakani na Sudan [sasa hivi South Sudan].

Brigade ya Minziro ndiyo iliyohitimisha vita vya Uganda na Brigadier.Kitete ndiye kamanda wa Tanzania aliyefika mpaka kijiji cha Koboko alipozaliwa alipozaliwa Iddi Amin Dada.

Makamanda wote wakuu waliopiganisha vita vya Kagera walikuwa na majina yao ya kimapigano au nom de guerre, kwa mfano Major General Kimario alijulikana kama "kamanda mbogo."Major General Imran Kombe alijulikana kama "kamanda ngono" kwasababu aliongoza mapigano kuvuka mto ngono. Colonel Tumbi ambaye alikuwa mkuu wa vikosi vya mizinga aliitwa "kamanda radi." Ahmed Takadiri Kitete alipewa jina la " kamanda supersonic. "

Baada ya vita vya Kagera Ahmed Kitete alikuwa mkuu wa operesheni na mafunzo wa Jwtz. Kwa bahati mbaya alifariki kwa ajali ya gari jijini D'salaam.

Nakaribisha michango ya wengine wenye taarifa za Ahmed Takadiri Kitete shujaa na kamanda mahiri wa jeshi la wananchi Watanzania.


Kushoto Brigedia Tumainieli Kiwelu kamanda mkuu wa operesheni chakaza ya kuondoa majeshi ya Uganda ktk ardhi ya Tanzania. Kulia Kanali Ahmed Kitete mkuu wa mipango ya kivita ktk operesheni chakaza.

cc Echolima, Manyerere Jackton , gobore, Mohamed Said, Nguruvi3, gobore, The only, Ukwaju
 
hawa jamaa ni wabaguzi sana, wanawatambua watu wao wa pwani tu.

kwa mfano akitokea mtu anaitwa ahmed suleiman mapunda, huwezi kuona wakimzungumzia hata kama aliwahi kuifanyia nchi mambo makubwa.
Wewe weka hata na donkey wacha mapunda, mradi kuna "Ahmed' huyo hafai kabisa, atakuwa ni "mfia dini" tu huyo.

Hata Mkwawa alikuwa ni Abdallah, ndiyo wale wale.
 
Alifariki akiwa na rank gani?

..alikwenda vitani kama Kanali.

..akiwa vitani akapandishwa cheo kuwa Brigadier.

..siku hizi brigadier wanaitwa Brigadier.General.

..baada ya kupandishwa cheo huko vitani, akakabidhiwa jukumu la kuongoza brigade ya Minziro.

..aliporudi toka vitani alikuwa mkuu wa operesheni na mafunzo wa Jwtz.

..kwa kumbukumbu zangu, Ahmed Takadiri Kitete " kamanda supersonic " alifariki akiwa na cheo cha brigadier.
 
Kwa vile umemTAG Echolima tutapata uhakika na kuendeleza Historia hiyo
ila navyokumbuka Kamanda Mbogo ndiye aliyeipasua Uganda hadi kaskazini kabisa kuna wanaodai baada ya kupewa Kikosi cha Kamada Lupogo aliomba idhini ya kumkamata Nduli

Ila Kamanda Ben Msuya wa brigedi ya Tabora ndiye aliyeingia Kampala, baadaye nafasi yake kuchukuliwa na Kamanca Mayunga ambaye chini yake alikuwemo Brigedia Hemedi Kitete

luteni col Ben msuya ..alistaafu jeshi akiwa MEJA JENERALI..na jukumu lake la mwisho alikuwa mkuu wa kamandi ya tabora...yenye jukumu la kuangalia hadi Kigoma, Rukwa ..Masaka na Mbarara zilikuwa smoothered na mizinga kabla ya kutekwa. Hapo hatukupoteza askari wengi.

Amini na askari wake waliingia uoga tangu wapigwe na kutolewa Kagera. walianza kudai kuna Wacuba,Wachina,...ati wanasaidia Tanzania.

baada ya Mbarara kutekwa Mayunga alipandishwa cheo kuwa Major General na kupewa Brigade mbili kuziongoza. Chini yake walikuwepo Brig.Hemedi Kitete[rip] na Brig.Roland Makunda.

Ni wengi tu wa Makamanda wetu wanastahili sifa hizo ambapo hata kurasa ya JF itajaa
R.I.P. Kamanda Kitete

[QUOTE
HISTORIA FUPI YA MAKAMANDA. NA UPAMBANAJI WAO DHIDI YA NDULI IDDI AMIN (DADA)

Mwaka 1978 jeshi letu likuwa na Major General wawili tu, Major General Twalipo (aliyekuwa mkuu wa majeshi wakati huo) na Major General Sarakikya ambaye alikuwa balozi wetu huko Nigeria. Baadaya ya Major General kulikuwa na Mabrigadier sita au saba tu: Brigadier Marwa, Brigadier Musuguri, Brigadier Mayunga, Brigadier Walden, Brigadier Kiwelu, Brigadier Yusuf Himid nadhani na Brigadier Mkisi. Chini ya Mabrigadier kulikuwa na makanali kadhaa ikiwa ni pamoja na akina Moses Nnauye, Abdallah Natepe na wengineo.

Jeshi letu lilikuwa limegawanyika katika Brigade kama nne hivi: Kusini, Magharibi, Mashariki, na Zanzibar. Baada ya vita ile, ndipo Twalipo alipopandiswa cheo na kuwa Luteni General wakati Mabrigadier wale walipandishwa kuwa ma-major general;Muundo wa jeshi letu ukabadilishwa kidogo kuwa na division tatu. Miaka miwili baadaye Luteni General Twalipo alipandishwa cheo tena na kuwa General,ambapo chief of staff wa Jeshi akawa na cheo cha Luteni General. Baadaye sana cheo cha Brigadier kikabadilishwa na kuwa Brigadier General.

Kuhusu majina kama 'Black mamba" hayo yalikuwa maalumu au tunaweza kuita "usernames" ili kuficha utambulisho wao halisi hasa kwenye mawasiliano ya kijeshi vitani. Kila kamanda alikuwa na username yake.of course mengine yalitokana na jinsi kamanda alivyokabiliana na changamoto za kivita. Mfano Maj.Gen. Mwita Marwa (Kambale)aliitwa hivyo kwa sababu yeye binafsi na brigade yake walipigana wakiwa ndani ya maji kwa muda wa wiki mbili maji yanayofika kiunoni.Na bado walijitoa kimasomaso kukabiliana na adui. Brigade hiyo ilipata shida sana ya kuharibikiwa vifaa kama vile vya mawasiliano n.k.Radio za mawasiliano zote ziliharibika na maji.

KIPIGO CHA LUKAYA
Hapo mimi mwenyewe nilishiriki na nilijua kabisa kuwa sasa ushindi ni wetu baada ya kufanyia AMBUSH ambayo askari wengi wa Libya walipoteza maisha yao na wengine wengi kutekwa ilikuwa AMBUSH tamu sana yenye mashiko ambayo baada ya saa moja magari mengi sana yalionekana yakiwaka moto na Vilio vilikuwa vimetawala eneo hilo walisikika wakisema ALLAH-AKBAR enzi hizo mimi sikujua wana maana gani
Kilichonihakikishia ushindi ni Amin kuleta askari ambao wana uwezo kupigana Jangwani leo kawaleta kupigana kwenye misitu minene kama ya Uganda nilijua fika kuwa wata-Prove failer tu.

Mateka waliletwa mpaka Dar-es-salaam cha kilichowashangaza wengi ni kuwa walirudishwa makwao Bure kabisa Mwalimu alikataa Msaada wa mafuta kwa mwaka mzima ambayo Libya iliahidi kulipa kukomboa askari wao waliotekwa katika vita hiyo.Hapo Mwalimu alisema sisi hatufanyi Biashara ya kuuza watu. lakini kuna historia nzuri kuhusu kutekwa kwa mji wa kampala, ambapo Brig. Kiwelu (wakati huo) aliongoza mapambano kutokea lukaya, kuanzia usiku wa manane mfululizo kwa karibu masaa nane, BM 24 zikiunguruma na Kampala ikawa mikononi mwa jeshi la ukombozi.

Jambo jingine, Generali Mboma wakati huo alikuwa Pilot na ndiye aliyeongoza kipigo kilichoziacha ndege yingi za amini kwenye uwanja wa Entebe taabani. Kama mnakumbuka ndege yetu iliyotunguliwa na majeshi yetu wenyewe kwa bahati mbaya,Rubani wa kijeshi aliyetunguliwa kwa makosa na JWTZ alikuwa ni Capt. Alexander Kaleya Mshana. Basi hawa akina mbona waliondoka Ngerere bila kutoa taarifa kwa makamanda wa vikosi vya nchi kavu (Hili lilifanyika makusudi) na wakaruka hadi Uganda.

This wa the most precise target JWTZ did. hadi Amin akalalamika kwamba JWTZ ina mamluki wa kukodiwa. Kwa sababu ndege za amini zilikuwa zinajianda kuja kushambulia TZ, lakini ghafla, wakajikuta Ndege zetu zinaruka chini sana usawa wa ziwa hivyo kusababisha taharuki kubwa sana, na kwa kuwa ziliruka chini sana na kwa mwendo wa SUPERSONIC yaani mwendo unaozidi sauti zilisababisha hofu kubwa na majengo mengi ya vioo vilivunjika-vunjika na wetu wengi walitibiwa kwa Presha,wakati huo Benki kuu ya Uganda nayo ikapigwa.
Battelfield tactics zilipangwa na Col. Lupogo.

Makamnada walioongoza vita walikuwa ni Brig. Marwa, Brig. Mayunga, Brig. Kiwelu, na Brigadier Walden. Hawa ndio waliongia msituni na wapiganaji. Makamanda hawa alipata vyeo vyao hivyo kutokana na umahiri wao wa katika uongozi wa kijeshi, na wote walihudhuria mafunzo ya uongozi wa kijeshi ndani na nje ya nchi mara kadhaa. Baada ya Uhuru hatukuwa na wasomi wengi katika majeshi yetu. In fact ni hawa hawa makamanda walioweka mkakati wa kuhimiza elimu jeshini na kuanzisha Elimu ya sekondari compulsory kwa wanajeshi wote na kuhimiza ajira za kijeshi kwa wasomi.

BRIG GEN MOSES NNAUYE
huyu alishiriki kama muhamasishaji ..ni muhimu sana kuwa na vikosi vya bendi na burudani...[ie Mwenge jazz,na kwaya ya Marehemu Luten komba...]Hawa walikuwa na wajibu wa kuhakikisha askari wanaburudishwa na kuliwazwa baada ya kazi ngumu...na kuwatia hamasa...na propaganda za ushindi...

CHANGAMOTO ZA VITANI
Kuna askari wengi waliokuwa mstari wa mbele wanasema Lupogo alishindwa KABISA kuendesha vita na kurudishwa makao makuu. Kikosi chake cha 205 kuchukuliwa na Kimario. Kimario aliendesha mapigano makali na kikosi chake cha 205 kiliweza kukata katikati ya Uganda mpaka Nimule kwenye mpaka wa Uganda na Sudan. 205 ndiyo kikosi kilichopoteza kifaru kimoja baada ya mapigano makali ya masaa 8 ili kuteka daraja muhimu la Maporomoko ya Karuma Kwa maajabu, Mwl Nyerere alimpandisha cheo Lupogo kuwa Meja Jenerali na kumuacha yule aliyepiganisha vita na kushinda Kimario.

Wewe jiulize inakuaje aliyeshindwa vita kupandishwa cheo na yule liyeshinda kuachwa mpaka alipopandishwa cheo na Rais A.H Mwinyi.Hizo ndizo changamoto za Mstari wa mbele walizokuwa wanazipata wapiganishaji wetu. ikimzunguzia Marehemu Gen. Imran Kombe. Katika makamanda waliopiganisha vita kitaalamu na kwa ufundi wa hali ya juu mmoja wao alikuwa ni Gen Kombe.

Gen Msuguri alikuwa siyo msomi Lakini mabrigedia wake walikuwa wanaelimu ya kutosha na ndiyo maana waliweza kupanga mashambulizi ya kiufundi, ungeweza kuona jinsi hivi vikosi vilikuwa vinasonga mbele kwa kasi basi ungeona haikuwa kazi ya kubahatisha. Kutokusoma kwa Gen Msuguri siyo hoja kwani alikuwa na uwezo wa kujua mapungufu yake na ndio maana alizungukwa na makamanda wazuri, na hiyo ni sifa kubwa kwa kiongozi.
Askari wa Lupogo walipata matatizo kwasababu walikuwa wanapigana na kikosi cha Amini kilichokuwa mlimani.Hivyo wao walikosa OP Obsevartion Post wakajikuta wanashambuliwa kirahisi.

kuna uwezekano kabisa kwamba Lupogo alipandishwa cheo kwa kuzingatia rekodi yake ktk vita nzima na siyo wiki tatu za mapambano ambayo alifanya vibaya. labda tatizo lilitokana na intelligence na military planning.
Lt.Col.Ben Msuya. Huyu ndiyo aliongoza utekaji wa jiji la kampala, na baadaye ku-act kama mayor wa kampala, mkuu wa itifaki, na mwisho kuandaa shughuli ya kuapishwa Yussuf Lule. Lt.Col.Hassani Boma na Lt.Col.Mazora wametajwa kwa umahiri wao ktk medani ya vita.

Maj.Gen.Silas Mayunga "mti mkavu" ndiyo aliingia kijiji cha koboko ambako alizaliwa Iddi Amini.
luteni col Ben msuya ..alistaafu jeshi akiwa MEJA JENERALI..na jukumu lake la mwisho alikuwa mkuu wa kamandi ya tabora...yenye jukumu la kuangalia hadi Kigoma, Rukwa ..Masaka na Mbarara zilikuwa smoothered na mizinga kabla ya kutekwa. Hapo hatukupoteza askari wengi. Amini na askari wake waliingia uoga tangu wapigwe na kutolewa Kagera. walianza kudai kuna Wacuba,Wachina,...ati wanasaidia Tanzania.
baada ya Mbarara kutekwa Mayunga alipandishwa cheo kuwa Major General na kupewa Brigade mbili kuziongoza. Chini yake walikuwepo Brig.Hemedi Kitete[rip] na Brig.Roland Makunda.

Namkumbuka Brig. Gen. Ramadhani Haji Faki kama mmoja wa makamanda toka Zenj waliotunukiwa nishani na Mwalimu Nyerere uwanja wa taifa. Mchango wa Mwita Marwa ktk vita vya Kagera ulikuwa mkubwa.
Ndugu zangu, vita huwa havipiganiwi ardhini, angani au kwenye maji peke yake, vita hupiganwa pia kwenye Media, na kuongeza chumvi hufanya watu wasife moyo na kuwapa motisha..., "Ingekuwa ajabu sana kama vyombo vya habari vya nchi yetu vingesema jana tulipigwa sana lakini leo afadhali tunajaribu kuwapiga.." Think about it.

[/QUOTE]
kwa msaada wa mitandao
 
Thanks JokaKuu. Bahati mbaya hatuna tabia ya kuandika vitabu. Kuna mengi sana tunayakosa sababu tu yalifanywa na watanzania wenzetu majasiri, ila hakuna aliyepata wasaa wa kuandika kwa ajiri ya vizazi vijavyo

..fikiria kwa mfano Waisraeli walivyoandika kuhusu Entebe Raid.

..Watanzania tunaweza kuandika kuhusu mapigano ya Lukaya. Bila kuwapiga vibaya Walibya pale Lukaya huenda historia yetu, na matokeo ya vita vya Uganda, ingekuwa tofauti.

..Pia kuna mapigano ya Sembabule ambayo yalikuwa ya muda mrefu, wiki tatu, na kuna wakati Jwtz walikuwa wameelemewa, but somehow they pulled through.

..hiyo ni kwa upande wa vita vya Uganda. Sasa kuna vita vya Msumbiji, operation za Comoro I & II, na operation ya Seychelles.
 
Mkuu ulichoeleza ni sahihi kabisa na umeleta kumbu kumbu nzuri sana.

Baada ya vita huyu kamanda Kitete alikuwa maarufu nadhani kifo chake kilichotokea mapema kimechangia sana jina lake kutosikika. Nakumbuka ilikuwa kawaida kusikia ''supersonic'' au kumsikia Kitete.

Kuna tatizo kubwa sana katika kuweka kumbu kumbu za vita ya Kagera. Wapo watu walioshiriki na michango yao haielezwi. Tungewatumia akina Major General Msuya ambaye yupo kuweka kumbu kumbu sawa sawa.

Msuya naye ni kama Kitete, ushiriki wake hasa kuteka Kampala hauelezwi vema. Ni wachache sana wanaojua

Kuna askari kama akina Brigedia Ambrose Bayeke, huyu alikuwa na cheo kidogo wakati wa vita, lakini alipanda sana hata kuongoza vikosi vyetu kule Kongo. Ni watu wenye hazina ya historia ya JWTZ. Sijui yupo wapi

Mwingine ni Major general Maneno, naye kama Bayeke alikuwa ni afisa wa ngazi za kati.

Pengine washauriwe kuandika 'memoir ' na JWTZ iwasaidia katika kufanikisha hilo.

Nilimshauri Pascal Mayalla kupitia ''Media yake ya PP'' aandae documentary ya vita.
 
..hiyo ni kwa upande wa vita vya Uganda. Sasa kuna vita vya Msumbiji, operation za Comoro I & II, na operation ya Seychelles.
Seychelles ilikuwa na Luteni Jenerali Shimbo kama sikosei.

Vita ya Msumbiji tulikosa sana faida kutoka kwa Luteni Jenerali Tumainieli Kiwelu. Huyu alikuwa na mengi sana ya kueleza, na ndiye aliyemkabili Mwalimu akimweleza kwanin tunaua vijana wetu kwa vita ya ''wajomba''

Hiyo ilikuwa breakthrough ya kumaliza vita ya FRELIMO na RENAMO ambayo kwa kiasi fulani ilikuwa biashara ya viongozi na si vita ya wananchi.
 
Please please, wapo watu wa kukusaidia dondoo za kuchokoza mada kabla ya kuwaona wahusika.
Fanyia kazi mkuu, hili ni jema kwako na kwa Taifa na najua unaliweza bila chembe ya shaka.
Its true, linawezekana haswa kwa kuzingatia mimi mwenyewe baada ya JKT, nilikwenda straight JWTZ,
Kati ya kazi ngumu sana za utengenezaji documentary, ni documentary za vita. Kuna waandishi waliokuwa front line wawili nawakumbuka walikuwa AVI, Dickson Saileni na Dick Kaombwe, ila pia changamoto ni nyingi, inahitaji
1. Passion
2. Dedication
3. Commitment
4. Equipments
5. Contents Resourceful personnel
6. Financial Resources
7. Logistics
Kwa fani yetu high season hutokea mara moja kila baada ya miaka 5, by now mawazo yote ni October, ila everything is possible.
P
 
Turudishe hizi historia kwenye shule zetu

Brigedia kitete na wenzake sio wa kusahaulika
 
Wewe weka hata na donkey wacha mapunda, mradi kuna "Ahmed' huyo hafai kabisa, atakuwa ni "mfia dini" tu huyo.

Hata Mkwawa alikuwa ni Abdallah, ndiyo wale wale.
Akili unaacha sebleni unalita chakula sebleni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…