TANZIA Brigedia Mstaafu Hassan Ngwilizi Afariki Dunia

TANZIA Brigedia Mstaafu Hassan Ngwilizi Afariki Dunia

Kiongozi shukrani kwa madini. Ila hapo uliposema alienda kulinda kisiwa dhidi ya US na SA umeniacha kidogo.
Seychelles ilikuwa ni :socialist entity" katika bahari ya Hindi. 7th Fleet ilikuwa Mediterranean Sea. 6th Fleet ilikuwa Indian Ocean. Kusini kwa Africa kulikuwa na South Africa. Kikwazo kulikuwa ni Frontline States zikiongozwa na Tanzania. Mission number moja wakati huo ya USA, UK (CIA) ilikuwa ni kuondoa hicho kikwazo yaani Tanzania na "tentacles" zake ikiwemo Seychelles. Akigundua Hilo ndiyo maana Albert Rene aliomba msaada kwa Mwalimu Nyerere. TPDF wakampeleka Ngwilizi.
 
Kijeshi hakuna cheo cha Brigedia, Bali Brigedia Jenerali, na anakuwa na nyota moja kwenye gari yake.
 
Hapo kwenye watoto wengu. Mmoja wapo ni rafiki yangu. Aiseee. Anasema hata hajui alie au afanye nini maana huyu mzee hajawahi kuwa kwenye maisha yake na alikua hataki kumtambua kama mwanae.
Kuna mwanae mmoja niliskuli nae advance enzi za BWM president mkazi wa hiyari wa lushoto sasa, analia sana mdada wa watu japo now ni mmama muhenga mwenzangu.
 
Mkuu bila kuingia kwa undani uelewe kuwa wakati ule ulikuwa wakati wa "cold war". Makaburu walikuwa wanasaidiwa na Margareth Thatcher (UK) na Ronald Reagan (USA). Africa kulikuwa na "Frontline states " zikiongozwa na Mwalimu Nyerere na Salim Ahmed Salim akiongoza mapambano hayo U.N. Rais wa Seychelles wakati huo Albert Rene akiwa ni msoshalist aliomba msaada kwa Mwalimu alindwe kutokana na Marekani na Makaburu. Kumbuka Makao Makuu ya Jeshi la Marekani 6th Fleet yalikuwa Diego Garcia ambayo ni kilomita chache toka Seychelles. Katika Mazingira hayo ndiyo General Ngwilizi alipelekwa kukilinda kisiwa hicho dhidi ya US na SA. General Ngwilizi aliifanya kazi hiyo kwa ufanisi na mafanikio makubwa.
Operesheni ya pili ya kutukuka aliyoifanya ni ya Msumbiji. Kumbuka ndiye kamanda as TPDF aliyeongoza vikosi hivyo nchini huko kwa muda mrefu zaidi mpaka vita hivyo vinaisha. Wakati anaenda huko alikuwa ametokea Quetta, School of Infantry and Tactics, Pakistan. Kauli mbiu ya hicho chuo ni."Those who die for their country, never die".
RIP GENERAL HAH NGWILIZI
Huko Diego Garcia ndio inasemekana ndege ya Malaysia iliyopotea ilipelekwa huko
 
Back
Top Bottom