TANZIA Brigedia Mstaafu Hassan Ngwilizi Afariki Dunia

TANZIA Brigedia Mstaafu Hassan Ngwilizi Afariki Dunia

Mwenyewe nilishawahi kupakaziwa mtoto enzi za ujana, nilikuwa na umri wa miaka 19 tu. Nikakataa katakata. Yule binti alipoona hakieleweki akapeleka tumbo kwa mwingine, naye pia akakataa lakini binti akamng'ang'ania hadi kadi ya kliniki akamuandika. Mtoto akazaliwa, sasa hivi ni mtu mzima na anafanana kabisa na yule jamaa wa pili, japo yule mama yake aliolewa na mtu mwingine.
Maisha yetu ya vijijini yalikuwa na changamoto nyingi kwa vijana, labda kuliko siku hizi.
Sishangai mtu mkubwa mwenye cheo cha kijeshi kama yule kuwa na watoto wengi, na sishangai wengine akiwakataa maana mazingira mengine yanaongeza sana uwezekano wa kupakaziwa watoto.
Yah kweli mkuu, wanawake hawa tunazaa nao na kusaidiana nao kulea lkn weng wana siri kubwa mioyoni mwao. Anaweza kukupa mtoto ambae si wako na ikabaki kuwa siri kubwa kwake au pengin na yule aliempa hiyo mimba. Ndio maana nchi zilizoendelea wengi huanza kwanz kufanya vipimo kabla ya kuendelea na huduma za mimba.
 
HAPANA mkuu Mauritius ni kisiwa kikubwa sanasana tu, ni hivi visiwa vidogovidogo vipo km vi5 hivi, shelisheli Ngazija na wenzake ambao mpaka leo wanagombana utawala, JWTZ waliombwa kwenda tuliza ghasia kwani uchaguzi ulishindikana, baada ya kumuweka Rais akarudi
Shukrani mkuu kwa haya madini
 
basi alikuwa mtu wa aina yake,kupewa urais wa nchi jirani...mi nilimjua akiwa mkuu wa mkoa wa Dar kama sikosei

..unashangaa!?

..mbona Lt.Col.Benjamin Msuya aliongoza kikosi kilichoteka Kampala, halafu akalinda jiji hilo mpaka Raisi[ Yussuf Lule] wa serekali ya muda ya Uganda alipoapishwa?

..Ngwilizi alikuwa kamanda wa kikosi cha Jwtz kilichokwenda kulinda visiwa vya Seychelles.

..Pia aliongoza kikosi cha Jwtz kilichokwenda kusaidiana na Majeshi ya Msumbiji, na Zimbabwe, kupambana na waasi wa Renamo.

..Mwanachama mwenzetu Echolima alikuwepo ktk operation ya Seychelles / "Operation Mahe." Nachukua nafasi kumpa pole kwa kuondokewa na kamanda wake.

..Pia pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.
 
R.I.P.
ngwilizi+hasani.jpg
 
Moja maswali yaliyokuwa yanaulizwa kwenye Civics.

Ni Waziri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa.

Br. Ali Hassan Ngwilizi.
 
Back
Top Bottom