Brother amepata likizo anakuja kagua mashamba na mtaji nilishakula sijui nifanyeje

Usijali.yatapita.
Usikimbie Hilo Ni kosa..
Subiri aje utajua itakavyo kuwa.
Akisema umlipe mwambie akupe MUDA.
Mimi nilipewa milioni 2.
Za mteja alikuwa anawekeza nikala.
Siku alipoibuka ilikuwa Ni kasheehe.
Walikutana Hadi na bosi siku hyo nilitamani ardhi ipasuke.
Ila nilimuomba Mungu akanipa nguvu ya kusimama
nikawakabili nikawambia nitawalipa.
Na kweli niliwalipa.
 
Wewe ni popoma , Mungu Hana kingine cha kufanya kukutoa ..... Bahati haiji mara mbili ndug , solution hapo ni kutubu na kuomba msamaha af usikilizie second chance , miaka 33 huna mbele wala nyuma na Una degree moja kichwan ...Mungu kapambana akutoe ila akili huna, na umebakiza miaka 7 kufikia umri wa kufunga mahesabu ....
 
Mwambie tu ukweli atakuelewa ishamtokea jamaa yangu. alipewa mtaji wa milion 32 naye akaongeza miioni 8 iliwafanye biasha ya kununua na kusaga mawe ya dhahabu. Mara ya kwanza ikaenda poa, mara ya pili akampa mtu akampiga akabaki na milioni 8 tu. Akawa anaogopa kumwambia bro wake ukweli akawa anamdanganya sana kila mara. Ila uongo una mwisho ilifika muda akawa na stress sana. Mimi nikamshauri mwambie ukweli jamaa anaogopa sana. Akawa anataka kwenda kwa mganga eti ampe dawa akimwambia bro asimaindi. Mimi nikamwambia usiende kwa mganga ngoja mimi nikupe dawa mimi kijukuu cha Mshana. Nikampa kimti tu halafu nikamwambia mpigie umwambie. Jamaa akapata confidence bwana, akampigia akamwambia ukweli. Bro wake ajabu hakumaindi ila akasema kwanini hakumwambia muda wote angekuwa ashaongeza pesa waendelee na uzalishaji.

Napoandika haya leo jamaa na bro wake wana mtaji mkubwa sehemu mbili tofauti biashara yao iliendelea. Wanaongelea hundreds of millions kila baada ya mieizi miwili mpaka mitatu.

We mwambie ukweli tu japo umechelewa mkuu.
 
yatapita tu some tyme huwa hivyo hasa watu wenye malengo makubwa na teyar umri umesogea ni rahisi kutumbukia kwenye makorongo/trap km hayo..

nikushauri tu ili usolve hilo swala mwambie kwanza mama yako umeshaharibu ila utalipa mweleze ukweli wote ili ubaki huru then akija kaka yk mama ndio ataitisha kikao afu wewe hakikisha unakaa na mama karibu hapo pembeni maana chochote kinaweza kutokea shekh..
 
Penye miti hapana wajenzi
Mkuu subiri upambane na hali yako

Hivi hizo hela ungezitolea jasho unafikili ungezichezea kupeleka qnet sababu ulikuwa huna machungu nazo

Mimi nasimama na kaka ako chochote kile atakachoamua kuhusu wewe hela inauma sana unamwamini ndugu yako mfanye kitu anafanya madudu
 
Mhanga wa Qnet
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…