Brother amepata likizo anakuja kagua mashamba na mtaji nilishakula sijui nifanyeje

Brother amepata likizo anakuja kagua mashamba na mtaji nilishakula sijui nifanyeje

Hiyo wazee mjini tunasema umepiga alafu na wewe ukapigwa !

Ova
 
Kuna mahala umesema you're in 3rd floor (33 years old) ila mbona hauna ukomavu huo? No offence bro, una utoto sana.

Kama ulivyowasilisha bandiko lako hapa mwambie kaka yako hivyo hivyo. Usimletee akili za kitoto pia umesema mambo yako hayapo sawa, kwa nini umletee upumbavu mtu anayeweza kukutoa?
 
Wewe ni tatizo sana. Kwanza wewe ndo ulikuwa tatizo kwenye ndoa ya dadako, ndiyo maana baada ya kuondoka wewe wao wakarudiana so usiende kwa dadako tena. Ila torokea sehemu yoyote nyingine, andika meseji ya kusema ukweli na kuomba msamaha then tupa line katafute kibarua nje ya mji wako ufanye mwisho mwa 2021 uwe na kiasi cha kuanza kupunguza deni au kununua mashamba ili kurudisha uhusiano uliodorora!

Next time use your brain, huwezi kuwa graduate halafu unatapeliwa kizembe namna hiyo. Elimu haijakukomboa nenda ukafanye tuu vibarua!
 
Kaka yako nae atakuja kuandika ushuhuda humu
 
Asee Christmas kwangu imekuwa ya hovyo balaa, naona kama imekuja niumbua.

Kwanza kabisa mimi ni kijana wa miaka 33 ni degree holder lakini mpaka sasa sina kazi ya kueleweka, jambo ambalo limefanya nishindwe kuwa na familia.

Maisha dar yalinitandika haswa ikabidi nirudi kwa mama ndio mpaka sasa nilipo,.. Niliwahi bahatisha kazi kwenye berau de change dar lakini 2018 December tulivamiwa ofisini na askari wakatukamata japo baadae tuliachiwa lakini kibarua kikaota majani .

Baada ya hapo nilitafuta kazi bila mafanikio nikashindwa lipa pango ikabidi niendee kukaa kwa sista aka kwa shemeji nimekaa pale sana bila mishe yoyote kama miezi 6, kumbe shemeji, alikuwa anachukia ikabidi wanitengenezee zengwe pamoja na sista.

Siku hiyo asubuhi mimi sina hili wala lile nasikia ugonvi kati ya sista na shemeji, baadae sista akakasirika sana akachukua mabegi akaondoka. Mimi nikabaki najiuliza nimfate sista au niendele kukaa kwa shemeji? Nikasema wee mjinga usinitanie hapa siondoki,

baada ya siku mbili sista kaniambia ameshafika nyumbani, shemeji nae siku hiyohiyo akaniambia kesho inabidi uondoke ninasafari ya kikazi nashukuru alinipatia kiasi kidogo nikachukua vyangu nikasepa kurudi kwa mama maana nilikuwa sina jinsi

Nimerudi home haikupita hata wiki mbili sista huyo akarudi kwa mumewe, nilimuuliza sista kama naweza rudi akasema nitulie kwanza.... hali iwe shwali.

Bahati nzuri mwaka huu brother kapata dili kwenye kampuni kubwa hapo dar es salaam, ikabidi nitumie fursa ya kilimo kupata mtaji kutoka kwake kwa makubaliano kuwa tutakacho pata faida nusu kwa nusu mtaji wake ubaki pale pale

Mpaka sasa ameshanitumia kama millioni 4.5 pia alinunua pikipiki kutoka kwa rafiki yale alikuwa kafulia akanikabidhi kuwa niwe nafanyia patrol kwenye shughuli za shamba.

Nifupishe tu pesa yote kuna jamaa alikuja akatushauri kwenye kikundi kuwa tukiwekeza kwenye kampuni yao kiasi cha 4.5m tutakuwa tunapata dola kati ya 100 na 200 kila mwezi, akatuonesha document yeye anavyolipwa nikaona hii ndio shortcut. Pia katuambia mtaji kwa mtu mmoja mmoja ni 5m hiyo 4.5m ni mkiwa kikundi kuanzia watu 4

Mpaka naandika hapa sijawahi pokea hata shilingi kumi jamaa hatujamuona baada ya danadana kibao juzi hapa tunasikia kakamatwa sijui hata nianzie wapi.

Brother nae kila muda anataka nimtumie picha za mazao juzi nilisikia anaongea na mother kwenye simu kuwa anaumwa hawezi kuja kula Christmas jana usiku akapiga tena kuwa kapata nafuu ameshakata tiketi ya kuja asee nilivyosikia nimechanganyikiwa.

Leo asubuhi nimetoka njee nikakuta mbwa wanafanya mapenzi wamenasiana asee hasira zangu zote nimemaliza kwao nimewatandika bakora za kiwango cha stieglas gorge
hadi raia wakaingila kati, toka asubuh sijarudi nyumbani napiga hesabu sijui nitamwambieje brother
Goodmorning billionaire
 
Hizo pesa bro na sista wanazotuma kwa mama mimi ndio huwa nazipangia matumizi sasa kwenye hizo hizo pesa nitazibana mpaka hiyo pesa itoshe hata kama ni nisu,
 
Hizo pesa bro na sista wanazotuma kwa mama mimi ndio huwa nazipangia matumizi sasa kwenye hizo hizo pesa nitazibana mpaka hiyo pesa itoshe hata kama ni nisu,
Wwe jamaa yani nimetafakari nashindwa niseme nini, huyo chawa ndiye atakuja mwambia bro wako ukweli
 
Hizo pesa bro na sista wanazotuma kwa mama mimi ndio huwa nazipangia matumizi sasa kwenye hizo hizo pesa nitazibana mpaka hiyo pesa itoshe hata kama ni nisu,
hutatatua tatizo hapo umeongeza tatizo any ngoja na mm nipambane na yangu kila mtu na yake...
 
Now siangalii chawa au tatizo kutotatuka. Ila nahitaji kutafuta pesa japo asilimia kadhaa za ule mtaji
 
Back
Top Bottom