Hahaha watanzania tunashida sana, Umeandika vizuri kuonyesha umeelewa udanganyifu alioufanya. Sasa hizo chuki,roho mbaya na kuchomeana zimetoka wapi?
Rudi mwanzo, Je alidanganya ama Hakudanganya. Kam alidanganya muajiri anakosa gani hapo? Au mahakama inakosa gani kutoa hukumu? Muajiri anajukumu la kufuatilia watumishi wake wakiwa masomoni, kama mtumishi amepewa ruhusa ya miaka mitatu kwenda masomoni. Miaka mitatu imeisha unadhani ni nani mwenye jukumu la kufuatilia kama mtumishi kamaliza au hajamaliza masomo? Muajiri anatakiwa apewe report, awe ka fail na anarudia mwaka, au ana suppliment, still muajiri anapaswa kupewa report hiyo. Ikiwa muajiri hato pata hiyo taarifa kwa maandishi, ni wajibu wa muajiri kuwasiliana na chuo anachosoma mwajiriwa na apewe taarifa ya nini ni nini au kipi na inawekwa kwenye personnel record za mwajiriwa/mtumishi.
Hili lazima lifanyike kwasababu huyo mwajiriwa/mtumishi analipwa mshahara, na unaweza kuta na ada ananlipiwa kulingana na mkataba waliokuwa nao. Na kama muajiri hafuatilii watumishi wake huyo muajiri ni mwendawazimu.
Sio kila kitu mnachomewa, au kufitiniwa kuna vitu viko straight foward, hakuna mchawi.
Mwajiri kafuatilia kapata report yeye kaandika barua ya kudanganya. Muajiri akamshitaki, yeye mtumishi alipaswa aombe msamaha hatua za awali za kesi, na amuombe radhi muajiri wake kwa kueleza ukweli ngesamehewa. lakini kakubali kuumeza ukweli na kwenda na ukweli mahakamani kesi/shauri limeendeshwa mpaka hukumu imetolewa, wewe unasema kachomewa.
Mahakama zikitenda haki hamtaki, zisipotenda haki hamtaki, hata hamueleweki.