Bukoba: Mwalimu atakiwa kurejesha Mshahara aliolipwa kwa kufanya Udanganyifu kwa Mwajiri

Bukoba: Mwalimu atakiwa kurejesha Mshahara aliolipwa kwa kufanya Udanganyifu kwa Mwajiri

K
Jifunze kusoma vizuri mkuu. Huyu mtumishi aliomba ruhusa akasome shahada ya kwanza,,baada ya kumaliza hyo shahada ya kwanza alitamani aendelee na shahada ya pili lakini ruhusa akawa hana maana ruhusa ambayo alipewa ni ya kusoma shahada ya kwanza ilikuwa imeisha.

Hivyo akalazimika kufanya udanganyifu wa kumuandikia muajiri wake barua kuwa hajamaliza shahada ya kwanza kwa sababu kadhaa(alifoji sababu) hivyo anaomba apewe ruhusa aweze kumalizia..malengo yake ni kwamba hyo ruhusa angepewa angeenda kusoma Shahada ya pili.

Umeelewa?
Weli
Novemba 22, 2023 katika Mahakama ya Bukoba imeamriwa kesi ya Jamhuri dhidi LYDIA KOKUSHOBOKA KAOO, ambaye ni alikuwa mwalimu wa Shule ya Msingi Kashai- Manispaa ya Bukoba.

Imemtia hatiani kwa makosa mawili la kwanza matumizi ya nyaraka kumdanganya mwajiri kwa kuandika barua kwa mwajiri kujifanya hajamaliza masomo ya shahada ya kwanza ndani ya muda aliopewa na mwajiri wake ili aweze kuendelea na shahada ya pili.

Kosa la pili ni kuisababishia Serikali hasara kwa kuendelea kulipwa mishahara kwa kipindi cha udanganyifu asichokuwepo kazini.

Mshtakiwa ametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 3 or fine ya 1 milioni kwa kosa la kwanza. Na kifungo cha miaka 3 bila fine kwa kosa la pili.

Pia imeamuliwa jumla ya sh. 22,252,134.73/= iliyopokelewa kama mishahara azirudishe kwa mwajiri wake.
Walimu wengi midomo Yao iko wazi Sana,hawana Siri na hawajui kukàa kimya.mafriji Yao hayagandishi
 
Maelezo yanaonesha, alikuwa na ruhusa ya kusoma shahada.

Lakini alipomaliza shahada, akaandika kwa mwajiri kuwa hajamaliza hiyo shahada yake kwahiyo anahitaji muda zaidi (ili atumie huo muda kusoma, Masters).

Sasa inavyoonekana Kuna elements zenye Chuki, roho mbaya na kuchomeana zimehusika hapa.
Mbona ni kitu kidogo tu hicho,...?

Watanzania kwa chuki [emoji119][emoji119]
 
Miezi mingapi,!? Mbona ni pesa nyingi Sana .
Inawezekana kama analipwa Million moja kwa mwezi labda baada ya makato na alikaa miaka miwili bila kuonekana kituo cha kazi mkwanja lazima marundo yasome huko mbali hivyo 😂😂 maana hapo inaonekana na kufoji amefoji nyaraka !!

Daah kama alitumia hizo vizuri ambazo hakua kazini kwenye shughuli zake labda itamsaidia.
 
Hiyo adhabu ya pili ya kifungo cha miaka mitatu bila faini ndiyo ngumu.

Hao waalim wameminywa hata kwenda kusoma ruhusa unanyimwa. Angejiongeza hiyo master angesoma Open University ili awe anaenda kazini.

Sawa, sasa faini atailipa na nini na atakuwa hana ajira tena, maana amefungwa.

Wanasheria nguli watamtetea.
 
Maelezo yanaonesha, alikuwa na ruhusa ya kusoma shahada.

Lakini alipomaliza shahada, akaandika kwa mwajiri kuwa hajamaliza hiyo shahada yake kwahiyo anahitaji muda zaidi (ili atumie huo muda kusoma, Masters).

Sasa inavyoonekana Kuna elements zenye Chuki, roho mbaya na kuchomeana zimehusika hapa.
Kudanganya mwajiri wako ni jambo jema?

Maana unaposema roho mbaya unamaanisha angeendelea kudanganya?
 
Kudanganya mwajiri wako ni jambo jema?

Maana unaposema roho mbaya unamaanisha angeendelea kudanganya?
Hata kuruhusu mtumishi kujiendeleza kwa kadri anavyoweza bila kuweka vijikwazo kwaso vya kiboya ni jukumu la mwajiri
 
Back
Top Bottom