macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Mosi: Waandishi wa Tanzania jifunzeni kutumia maneno ''hata hivyo'' kwenye habari. Hili ni kosa linalojirudia mpaka kwenye vyombo vikubwa vya habari. Sahihi hapa ingewa ''pamoja na hayo'' etc. Ukishasema ''hata hivyo'' sentensi inayofuata ni lazima ikinzane na unachozungumzia. egHata hivyo, Jeshi la Polisi limegundua kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia mbinu ya kutoa msaada kwa familia zenye uhitaji kila Jumamosi, ambapo baadhi ya familia hizo huwatuma watoto wao kufuata mahitaji yao ofisini kwake, na ndipo hutumia nafasi hiyo kuwafanyia ukatili huo.
Source: Swahilitimes
Pili: Ubakaji wa watoto Tanzania uko juu sana sababu kubwa ni wazazi 1. kutokuwa waangalifu na kuamini watu kirahisi 2. Kutokuwa karibu na watoto wao na kuwa wakali. 3. Serikali kutokuwa na mikakati ya kuzuia na kutoa elimu na rushwa kwa polisi au mahakama.