Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Habari hii nilitarajia itataja idadi ya majeruhi pamoja na walioruhusiwa,hakuna
 
Hii Ajari Kuna watu mnataka kuitumia ili mjipatie umaarufu wa kijinga ,sijui mtabiri nk

Acheni hayo mambo hakuna hata binadamu mmoja mwenye huwezo wa kufahamu kuhusu Kesho Nini kitatokea Katika Maisha ya Binadamu.
Ni kubahatisha bahatisha tu !!
 
Ndege ya precision air imeaguka mita 100 kabla ya kuifikia barabara/runway ya uwanja wa ndege wa Bukoba
View attachment 2408442
Hapa chini ni Link ya video ya jiografia ya uwanja wa Bukoba... Instagram mcshonde

Ajali imetokea saa 2 asubuhi na taarifa zimesambaa tangu muda huo wewe unaleta "Breaking News" more than saa 6 tangu ajali itokee!!!!🤔🤔🤔
 
Msiwe kama waoga nje kuogopa kuchunguliwa
Subili serikali iseme k2
IMG-20221106-WA0007.jpg
 
ina maana hata jeshi letu la wananchi hapo Bukoba halina Helicopter hata mbili au tatu na chap kwenda pale kufanya tandemn lifting na kuipull chap hiyo ndege kwenye kina kidogo nchi kavu?.

Hapo ziwani Bukoba kabisa hakuna tag boats za kuivuta hiyo ndege?.

Ina maana hapo Bukoha mjini hakuna sling au belts za zaidi ya 20tons zikaungwa kama wananchi walivyounga hiyo kamba na Bulldozer ikavuta ikiwa nchi kavu?.

Miaka yote hapo kiwanjani pamoja na kuwa karibu na ziwa hakuna rescue yenye watu mahiri na vifaa kuokoa ziwani?.

Naamini ndege ilivyokuwa mwenye maji ndani ya ndege hakukuwa na power supply, hivyo hakukuwa na hewa, zaidi ya 1hrs ndani ya maji mkiwa kwenye ndege bila hewa... MUNGU UWANUSURU NDUGU ZETU.
 
Sasa HV ndio CMG eti ndio wanaleta breaking news yao wakt jf inesharipot tukio hili muda mchache tu baada ya tukio kutokee

Kuna saa nilipost ndege ya precious ule mkia ukiwa unaonekana haujazama wote jamaa mmoja akanitext kuniuliza leo unaenda kupanda ndege nni Hapo Hapo nikatoka kufuta ile stutus nikasema nchi hi inawajinga wengi sanaa sijamjibu had sas nikamekausha
 
Kwahiyo Mitambo ya Simu za Mkononi huwa inashika hata kama Mitambo ya Umeme ya Ndege ikiwa imezama na Ndege iko Majini kwa 95% kama hivyo?

Kwa simu za mkononi mawasiliano yanakuwepo sababu ile ni wireless connection kati ya antenna iliyopo kwenye simu na antenna iliyo katika mnara wa mawasiliano wa simu (tigo, voda, airtel, halotel) ulio karibu...

Na hiyo ndege haijazama kina kirefu kiasi cha RF signal kuwa blocked au faded...
 
Precision air yapata ajali Bukoba ziwa Victoria
View attachment 2408224
View attachment 2408189
View attachment 2408195



===
NDEGE YA PRECISION YAANGUKA ZIWA VICTORIA MJINI BUKOBA

Ndege ya Shirika la Ndege la Precision, imeanguka ziwani mjini Bukoba, Mkoani Kagera asubuhi ya leo Novemba 6, 2022

Taarifa za awali zinaonesha ndege hiyo imeanguka ziwani, uokoaji wa abiria unaendelea.

Taarifa kwa kina zinafuata

=====

NDEGE YA PRECISION AIR ILIKUWA IKIJIANDAA KUTUA
Mmoja wa abiria wa Precision Air, Simon Mkina amesema tukio hilo limetokea asubuhi ya leo Novemba 6, 2022 Saa mbili kasoro dakika 10 wakati ndege ikiwa inajiandaa kutua.

Amesema “Nipo eneo la tukio, nilikuwa naisubiri hiyo ndege kurudi Dar es Salaam, ghafla tukaona ndege umepitiliza, rubani ikashindwa kutua kwenye njia yake, inawezekana amekosa mawasiliano au kuna hitilafu ilitokea.

Ameongeza “Mpaka sasa hatujajua nini hasa ni chanzo kwa kuwa rubani mwenyewe bado hajatolewa ndani ya ndege na uokoaji unaendelea.”

ABIRIA waliokuwa katika ndege ya shirika la ndege la Precision Air iliyoanguka katika Ziwa Victoria kabla ya kutua uwanja wa ndege wa Bukoba wameokolewa, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amethibitisha.

Akitoa taarifa ya awali kuhusu ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Mwampaghale amesema manusula wote wamepelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Kagera kwa ajili ya matibabu.

“Ndege ilipata ajali mita 100 kabla ya kutua uwanja wa ndege. Abiria wameokolewa na jitihada zinaendelea,” amesema nakuongeza “tukio lipo ‘under control.’”

Mwampaghale amewataka wananchi kupunguza haharuki na kuondoka eneo la tukio ili kuruhusu vyombo husika kuendelea na shughuli za uokozi.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi Zabron Muhuma amesema jeshi linaendelea na uokoaji ili kuhakikisha ndge hiyo inatolewa majini.

Imeandaliwa na Diana Deus

====

UPDATE: WATU 26 WAMEOKOLEWA KATI YA 43 KATIKA AJALI YA NDEGE
Ndege ya Precision Air iliyopata ajali wakati wa kutua Bukoba ilibeba watu 43 na tayari waliookolewa ni 26 ambao wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa taarifa hiyo kuhudu ndege hiyo ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF ambayo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Bukoba na ilikua na safari ya kurudi Dar.

Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amesema zoezi la uokoaji la ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba linaendelea kwa kuivuta ndege kuelekea ufukweni.

===============
Chalamila hoi hapo
 
Back
Top Bottom