Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa Ndege ilivyozama vile ulikuwa Unawategemea kweli kabisa Mkuu wangu?Sijaona taarifa ya majeruhi.
Ni kubahatisha bahatisha tu !!Hii Ajari Kuna watu mnataka kuitumia ili mjipatie umaarufu wa kijinga ,sijui mtabiri nk
Acheni hayo mambo hakuna hata binadamu mmoja mwenye huwezo wa kufahamu kuhusu Kesho Nini kitatokea Katika Maisha ya Binadamu.
Sato wameshaanza Kula Visigino vyao.Hivi Marubani bado hawajatolewa tu, bado wazima kweli?🤔
Niko folen hosp hapa hii comment yako imenifanya nionekana chiz kwa kuchekaKwamba ndege itaanguka hapa jamii forums. We mkuu utakuwa umeamkia k vant
Ndege ya precision air imeaguka mita 100 kabla ya kuifikia barabara/runway ya uwanja wa ndege wa Bukoba
View attachment 2408442
Hapa chini ni Link ya video ya jiografia ya uwanja wa Bukoba... Instagram mcshonde
Sangara anapambana sasa Kulila la Pili.Bwana rubani hayo Macho yako vzuri kwel
Ni ma freemason yanakuwa na ratiba za matukio waliyo yaratibu kutokeaKuna mtu alitabiri juzi hapa kuwa ndege itaanguka tena hapa jamii forums....
Yule jamaa ni mchawi
Kwahiyo Mitambo ya Simu za Mkononi huwa inashika hata kama Mitambo ya Umeme ya Ndege ikiwa imezama na Ndege iko Majini kwa 95% kama hivyo?
Ule uzi kwasasa unafwatiliwa na watu wa usalama wa timu ya tiss aviation wing na tiss terrorism protection wing kuwa makini.Utabiri wa yule jamaa umetimia mwenye uzi wake alete hapa aseee
So sad mbona tuliambiwa wote wametoka salama 😪Unfortunately mpaka Muda huu zaidi ya watu kumi wamepoteza maisha hizi habari nimepewa na ndugu yangu yupo hapo Government hosptal Bukoba
So wanaosemwa wameokolewa 26 ulikua mda GANI Kama hutajali, au unamanisha zoezi limeanza saa sita wakianza na watatu uliyowataja?Walianza saa sita
Pole sana kwa wafiwa Mungu awape Nguvu katika kipindi hichi kigumu sana !Unfortunately mpaka Muda huu zaidi ya watu kumi wamepoteza maisha hizi habari nimepewa na ndugu yangu yupo hapo Government hosptal Bukoba
Chalamila hoi hapoPrecision air yapata ajali Bukoba ziwa Victoria
View attachment 2408224
View attachment 2408189
View attachment 2408195
===
NDEGE YA PRECISION YAANGUKA ZIWA VICTORIA MJINI BUKOBA
Ndege ya Shirika la Ndege la Precision, imeanguka ziwani mjini Bukoba, Mkoani Kagera asubuhi ya leo Novemba 6, 2022
Taarifa za awali zinaonesha ndege hiyo imeanguka ziwani, uokoaji wa abiria unaendelea.
Taarifa kwa kina zinafuata
=====
NDEGE YA PRECISION AIR ILIKUWA IKIJIANDAA KUTUA
Mmoja wa abiria wa Precision Air, Simon Mkina amesema tukio hilo limetokea asubuhi ya leo Novemba 6, 2022 Saa mbili kasoro dakika 10 wakati ndege ikiwa inajiandaa kutua.
Amesema “Nipo eneo la tukio, nilikuwa naisubiri hiyo ndege kurudi Dar es Salaam, ghafla tukaona ndege umepitiliza, rubani ikashindwa kutua kwenye njia yake, inawezekana amekosa mawasiliano au kuna hitilafu ilitokea.
Ameongeza “Mpaka sasa hatujajua nini hasa ni chanzo kwa kuwa rubani mwenyewe bado hajatolewa ndani ya ndege na uokoaji unaendelea.”
ABIRIA waliokuwa katika ndege ya shirika la ndege la Precision Air iliyoanguka katika Ziwa Victoria kabla ya kutua uwanja wa ndege wa Bukoba wameokolewa, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amethibitisha.
Akitoa taarifa ya awali kuhusu ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Mwampaghale amesema manusula wote wamepelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Kagera kwa ajili ya matibabu.
“Ndege ilipata ajali mita 100 kabla ya kutua uwanja wa ndege. Abiria wameokolewa na jitihada zinaendelea,” amesema nakuongeza “tukio lipo ‘under control.’”
Mwampaghale amewataka wananchi kupunguza haharuki na kuondoka eneo la tukio ili kuruhusu vyombo husika kuendelea na shughuli za uokozi.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi Zabron Muhuma amesema jeshi linaendelea na uokoaji ili kuhakikisha ndge hiyo inatolewa majini.
Imeandaliwa na Diana Deus
====
UPDATE: WATU 26 WAMEOKOLEWA KATI YA 43 KATIKA AJALI YA NDEGE
Ndege ya Precision Air iliyopata ajali wakati wa kutua Bukoba ilibeba watu 43 na tayari waliookolewa ni 26 ambao wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa taarifa hiyo kuhudu ndege hiyo ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF ambayo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Bukoba na ilikua na safari ya kurudi Dar.
Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amesema zoezi la uokoaji la ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba linaendelea kwa kuivuta ndege kuelekea ufukweni.
===============