Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Precision air yapata ajali Bukoba ziwa Victoria

View attachment 2408189
View attachment 2408195



===
NDEGE YA PRECISION YAANGUKA ZIWANI BUKOBA

Ndege ya Shirika la Ndege la Precision, imeanguka ziwani mjini Bukoba, Mkoani Kagera asubuhi ya leo Novemba 6, 2022

Taarifa za awali zinaonesha ndege hiyo imeanguka ziwani, uokoaji wa abiria unaendelea.

Taarifa kwa kina zinafuata

Hiyo ndege mbona kama imeenda pachikwa hapo tu kisilencer.. embu hichunguzwee hii.. hujuma..

Ajali fake hii..kwa ajali za ndege zinavyokuaga..
 
Aanh

Ni hatari sana kupanda usafiri wa meli na ndege kwa hizi nchi zinazoitwa 3rd countries

Mika 5 nyuma nakumbuka natoka dar naenda mbeya na hizi ndege za mtumba alizotuletea anko magu
Maeneo ya iringa pale kitonga, ndege linayumba kwa sababu ya kani ya mvutano

Nilisali salamu maria mara 1, baba yetu mara 2
Na nikapiga Alu akbar kama 5 hivi
Hatari Sana Yaani Hatuijui Dakika Moja Mbele Kutatokea Nini
 
Ni kweli.
Hali ya hewa ilikuwa ni ya mvua nyingi. Na inaonekana landing alianzia upande wa Zamzam ambako kuna obstacles.

All in all, tunaanza kulikumbuka wazo la Magu la kurefusha uwanja upande wa ziwani. Hii sijui iliishia wapi! Sasa tunaanza kuona madhara ya kupuuza wazo hilo.

Mimi katika uhai wangu, hii ni ndege ya pili kupata ajali ya aina hiyo kwenye hiyo site. Ya kwanza ilikuwa ndege ya jesh(siyo ya kivita) wakati wa vita na Iddi Amin. Ndege hiyo ilikuwa aina ya Buffalo.
Nime google labda nitapata breaking news update nimeingia site yao hakuna habari yoyote napata mashaka na hizi habari jambo kama hili kweli hakuna sehemu tukapata habari za uhakika
 
Fastjet na precisionair wanatumia ndege za mtumba. Na fastjet ndio zilikuwa kimeo kabisa. Magu alilijua hili na ndio maana kwa kutumia kodi zetu akataka atuhakikishie usalama pia kwa kununua ndege mpya.

Lengo ilikuwa usalama kwa watanzania badala ya kusubiri majanga.
Watu humponda Magu pasipo kujua, hizo ni mitumba , hatari kwa usalama wa wananchi, lakini wenye roho nzuri wana kuambia Magufuli aliwafukuza, hii nchi watu wanaongea sana with zero facts.
 
Lakini Precicion wana ndege nzuri sana,hizi ATR ni ndege zenye historia nzuri sana angani,sijajua kutakuwa kumtokea nini,kuna uwezekano mkubwa sana kuwa ni uzembe...
 
Aanh

Ni hatari sana kupanda usafiri wa meli na ndege kwa hizi nchi zinazoitwa 3rd countries

Mika 5 nyuma nakumbuka natoka dar naenda mbeya na hizi ndege za mtumba alizotuletea anko magu
Maeneo ya iringa pale kitonga, ndege linayumba kwa sababu ya kani ya mvutano

Nilisali salamu maria mara 1, baba yetu mara 2
Na nikapiga Alu akbar kama 5 hivi
Hahaha dah! Ulisahau na nyimbo za vilingeni[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom