Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Awamu ya majanga.

Ajali, ukame na bado njaa.

Tatizo hawamwamini Mungu.

Wameweka matumaini kwenye kitu kinaitwa Jamhuri.

Mungu ana nafasi yake jamani.
 
Mbona wote hamjagundua kuwa hili ni jaribio la kuona utayari wa vyombo vya uokoaji. Kumbuka Mwaka jana kipindi kama hiki lilitokea pia eneo hili hili. Akiri mu kichwa
Precision air wenyewe wamethibitisha kwamba ndege Yao imepata ajali, hii ni ajali kweli mkuu
FB_IMG_1667723619705.jpg


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Alisema ina logo nyekundu na itakatika katikati. Utabiri wake sio wa ndege hii maana haina logo nyekundu na haijakatika katikati
Ukielewa maana ya utabiri utaacha kuhoji. Hakuna mtabiri anayetaja details 100%, hiyo sio forensic investigation. Tena utabiri unaweza enda chaka kidogo, ukataja baba fulani atapanda cheo na isitokee kwake ikatokea kwa mkewe. Kwenye utabiri kuna nguvu mtabiri hazijui au hawezi kuzitafsiri, hiyo ya cheo unakuta bread maker ni mama au unakuta ndio alijilipia dowry au ndie ana kauli nyumbani
 
Jwtz ni jeshi la kizamani sana,hawana mitumbwi ile ya hewa ambayo wangefika nayo hapo,hii ndege ingeanguka kati kati ya ziwa watu wote wangekufa, nchi zilizoendelea huwa tunaona kwenye media jeshi linafika kwa ndege na askari wanashuka kwa parachute ziwani

Kama nchi haitonunua vifaa siku moja itazama ndege kzti kati ya ziwa watu wote wafe
Hata hapo watakaotoboa ni wachache
 
Ukielewa maana ya utabiri utaacha kuhoji. Hakuna mtabiri anayetaja details 100%, hiyo sio forensic investigation. Tena utabiri unaweza enda chaka kidogo, ukataja baba fulani atapanda cheo na isitokee kwake ikatokea kwa mkewe. Kwenye utabiri kuna nguvu mtabiri hazijui au hawezi kuzitafsiri, hiyo ya cheo unakuta bread maker ni mama au unakuta ndio alijilipia dowry au ndie ana kauli nyumbani

Ndio maana nimewaambia wafocus zaidi kwenye "Itatokea ajali ya ndege ya abiria"...........Mtabiri kwangu amepatia kwa 100%.
 
Aanh

Ni hatari sana kupanda usafiri wa meli na ndege kwa hizi nchi zinazoitwa 3rd countries

Mika 5 nyuma nakumbuka natoka dar naenda mbeya na hizi ndege za mtumba alizotuletea anko magu
Maeneo ya iringa pale kitonga, ndege linayumba kwa sababu ya kani ya mvutano

Nilisali salamu maria mara 1, baba yetu mara 2
Na nikapiga Alu akbar kama 5 hivi
Mabasi managpi yanapata ajali ? Hizi ni ajali kama ajali zingine mbona hata mataifa ya ulaya ndege zinapata ajali na kuanguka
 
Kwa jinsi ilivyozama inaonekana ni runway overshoot.

Ila hapo abiria watapitia wapi maana milango yote iko under water
Hapo sasa ingekuwa kwa wenzetu huko majuu saa nyingi hiyo ndege ingekuwa inaelea ama kwenye maji au angani !! Vifaa vyetu ni duni sana !! Poleni sana ndugu zetu
 
Hiyo ndege mbona kama imeenda pachikwa hapo tu kisilencer.. embu hichunguzwee hii.. hujuma..

Ajali fake hii..kwa ajali za ndege zinavyokuaga..
Hujajua ajari za ndege zinakuwaje. What if hii ni runway skid off ambayo imepelekea ndege kwenye tope la maji na kuzuia isiharibu airframe. Na vipi ulitaka ndege ivunjike watu wafe ndio iitwe ajari
 
Back
Top Bottom