Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Akitoa taarifa ya awali kuhusu ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba

UZOEFU WA MAZOEZI YA UTAYARI KUKABILIANA NA MAJANGA UTUMIKE
Kazi sasa ya vikosi vya uokozi na usalama kuja na ule mpango kazi walionao wa utayari kukitokea majanga kama haya.

Idara jeshi la Zimamoto, Mamlaka za Viwanja vya Ndege, Mamlaka ya Bandari Tanzania, Polisi na serikali ya mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na serikali kuu taifa pia bila kusahau Ma -Engineer wanatakiwa kuingia kazini kwa pamoja kufanya uokozi kwa kutumia vifaa vyao na utaalamu wao.
 
Kwahiyo Rubani Mzoefu Kazamisha Ndege au? Halafu naomba kujua inawezekana vipi Ndege kama hiyo ikwa imeanguka na Kuzimika kabisa hata kwa Mitambo yake halafu Marubani wake bado wawe na access ya Mawasiliano na Mkuu wa Mkoa Samjo Samjo ( Msanii ) kama Albert Chalamila na Wengineo?
Muwe mnachezaga hata simulator za ndege
 
ina maana hata jeshi letu la wananchi hapo Bukoba halina Helicopter hata mbili au tatu na chap kwenda pale kufanya tandemn lifting na kuipull chap hiyo ndege kwenye kina kidogo nchi kavu?.

Hapo ziwani Bukoba kabisa hakuna tag boats za kuivuta hiyo ndege?.

Ina maana hapo Bukoha mjini hakuna sling au belts za zaidi ya 20tons zikaungwa kama wananchi walivyounga hiyo kamba na Bulldozer ikavuta ikiwa nchi kavu?.

Miaka yote hapo kiwanjani pamoja na kuwa karibu na ziwa hakuna rescue yenye watu mahiri na vifaa kuokoa ziwani?.

Naamini ndege ilivyokuwa mwenye maji ndani ya ndege hakukuwa na power supply, hivyo hakukuwa na hewa, zaidi ya 1hrs ndani ya maji mkiwa kwenye ndege bila hewa... MUNGU UWANUSURU NDUGU ZETU.
Unajua hiyo ndege ina tani ngapi?

Vitu vingine usiongee bila kujua
 
Huyo aliyepewa ubunge wa EA na kumuacha @paschalmayalla.
Familia ya Mzee Kachwamba ukoo wa panya walikula KCU hadi kubaki mifupa na bado wanae na wajukuu wanazawadiwa vyeo huko CCM...smahani wakuu nimekuwa too emotional na kusahau "msiba"
Kwahiyo aliekufa ni mbunge au mtoto wa mbunge?
 
Unajua hiyo ndege ina tani ngapi?

Vitu vingine usiongee bila kujua

iko kwenye maji mzee, two hellicopters za kawaida kabisa zikifanya tandemn lifting na kuipull nchi kavu inawezekana kabisa...

tunazungumzia slight lift na pull, unaona hapo huo mtumbwi wa wavuvi unachofanya kuivuta maana tayari ni boyancy hiyo inaelea na kuivuta ni simple.
 
Ingekuwa kipindi cha Magufuli tungeambiwa hamna MTU hata mmoja aliyefariki,nakumbuka kipindi kile tren imeua watu wengi Dodoma lakini vikaripotiwa vifo so chini ya 10.
Hapana!!! Mimi siyo wala sikuwahi kuwa mshabiki wa JPM lakini kwenye hili ninamtetea!!. Tena nakumbuka taarifa ya habari inasomwa na Betty Chalamila saa 2 usiku akatoa angalizo kuwa picha zitakazofuata ni mbaya. I still have in my mind picha za watu watoto kwa wakubwa walivyobanwa kwenye mabehewa!!. Hapana hawakuficha idadi ya waliofariki sababu hata memorial yao ipo Dodoma sehemu walipozikwa wale walioshindwa kutambulika
 
Kama kuna vifo basi vinatokana na uzembe katika uokozi, na vifo vitakuwa vimetokana na watu kukosa hewa wakiwa ndani ya Yai majini.

Haraka baada tu ya kuwa majini, ilipaswa ivutwe chap nchi kavu maana inaonekana sio mbali na then kuitoboa au kufungua milango haraka na kutoa watu ikiwa nchi kavu.

Uzembe mkubwa sana wa mamlaka husika kushindwa kuwaza haraka na kufika kwenye eneo husika kwa haraka na vifaa husika kwa haraka kuokoa maisha ya watu.
Hivyo vifaa vya kufanya hayo unayosema vipo?
Kama kuna vifo basi vinatokana na uzembe katika uokozi, na vifo vitakuwa vimetokana na watu kukosa hewa wakiwa ndani ya Yai majini.

Haraka baada tu ya kuwa majini, ilipaswa ivutwe chap nchi kavu maana inaonekana sio mbali na then kuitoboa au kufungua milango haraka na kutoa watu ikiwa nchi kavu.

Uzembe mkubwa sana wa mamlaka husika kushindwa kuwaza haraka na kufika kwenye eneo husika kwa haraka na vifaa husika kwa haraka kuokoa maisha ya watu.
 
Wavuvi wenzangu wa Nyamukazi mmehitahidi sana, masaa zaidi ya manne mnapambana, Polisi na vikosi vya usalama hakuna ambaye uniform yake imedondokewa na tone la maji! Helikopta zipo kwa ajili ya kupeperusha mabango ya sensa!

Aibu kubwa sana kwa serikali hii, Waziri wa uchujuzi usipojiuzuru tutakushughulia kwa nguvu ya umma!
Siwatetei polisi,hivi kamandi ya maji ya JWTZ kazi yake ninini,au wao ni kufanya maonyesho Disemba?Wote hapo wanatakiwa kushirikiana.
 
Mungu awaokoe waliomo. Maana ziwa kubwa kama hilo lakini hatuna mfumo mzuri wa kuokoa watu wakipatwa na majanga.

Tangu ajali ya Mv Bukoba mwaka 1996 ilipotokea hakuna juhudi za maana za kuwa na mfumo wa kisasa wa uokozi kwenye ziwa hilo kubwa barani Afrika.
Ndege huwa inaruka angani japo ikitua ziwani inavyo vifaa vyake vya uokoaji yaani fulana na maboya ila inahitaji wahudumu wake walio makini na jasiri. Ndege ina milango na boya kubwa ambalo hutumika kuwatoa abiria ndani tayari wakiwa wamevaa fulana za kuelea japo haziwazuii samaki na mamba kutafuna miguu.
 
Hapo unatamani ungesikiliza yale maelezo ya usalama (safety instructions) yanayotolewa na cabin crews ambayo huwa watu wanapuuza kusikiliza.

Unaweza hata usilione boya ukamyang'anya mwenzako 🤣
IMG-20221106-WA0021.jpg
IMG-20221106-WA0021.jpg
 
Back
Top Bottom