Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Kichwa Cha habari kinajieleza na picha ipo chini.
20221106_195217.jpg
 
Kikosi cha zima moto na uokoaji , kinatakiwa kutafakari katika haya hivi karibuni moto uliwaka kule mlina Kilimanjaro lakini jitihada za kuuzima moto zilikuwa siyo effective sana ikichangizwa na vifaa vilivyokuwa vikitumika, leo tena Ndege imedondoka lakini pia tumeendelea kushuhudia bado kikosi hiki hakijajipanga kisawasawa kukabiliana na matukio ya dharula katika maeneo tofauti tofauti. Serikali ione umuhimu wa kukiwezesha kikosi hiki ili kifanye wajibu wake kisheria kikamilifu... Roho za watu hazina spare...Mlima Kilimanjaro unaiingiza serikali fedha nyingii sanaaa. Basi upewe kipaumbele maalumu.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
Tusiwalaumu,budget ndogo na hawana vifaa.
 
Kampuni yenyewe inalipa kidogo .ila mkiwashitaki inabidi muombe kiasi kikubwa na mnegotiate. Unafikiri wakitoa tu wenyewe watatoa nyingi bila kushurutishwa ?
Hapo sasa inategemea policies zao
Kulaliana ni kawaida ya waswahili ila ngoja tutasikia tu mana wapo waliopona!
 
angalau nimeichuua hii clip kabla Chalamila hajaifuta! Eti waliuwa wanawasiliana na marubani, shame!

Mkuu, sijui ni macho yangu yananidanganya nimeona kwenye instagram wakazi wa manispaa ya Bukoba walivuta ndege kwa kamba wakiwa na lengo la kuikwamua majini sijui!! Yaani mafundi/mainjina wa mkoa hata ubunifu hawana kabisa au ndio "AKAJALAMUKO" yaani hata kufikiria kwamba waleta four wheel drive heavy duty trucks au tractors zifungwe in tandem watafute chain au kamba ndefu ifungwe kwenye ndege ili ifutwe kirahisi na kwa haraka - madam President wewe ni mwelewa wa mambo hata ya kiufundi ukifafanuliwa vizuri na watu weledi na wabunifu - hivi Mh. Rais inaingia akilini kwamba situation kama hii unaweza kweli ukategemea Manpower (wanavuta kwa kamba -ooh,ooh,vuteni,vuteni!!) kuliko Horse Power (Mashines ie magari/tractor) kuvuta ndege kutoka majini in no time - Watanzania tukoje lakini??
 
Watu 26 wameokolewa swali wameokolewa vipi? walitoka kwenye emerg exit na kama walitoka vipi mkuu wamkoa unakuja kusema bado tunawasiliana na rubani kwanini maelezo hayaingii akilini. cockpit inasehemu ya kuvunja na kutoka je kama exit imewatoa watu mnaosema wameokolewa hao wengine wako wapi? hii ni recevory ya ndege au ni rescue mbona mnatisha watu ku report hali halisi kweli hakuna hata picha za waliokolewa? siri za nini? hii ni accident sisemi muoneshe maiti lakini wale waliowazima shida iko wapi watu wapate faraja kidogo. watu wanavuta kamba askari kasimama na silaha utasema kuna vita. Aibu tena aibu sana. Hongera kwa wananchi wanawake kwa wanaume wanafanya wanachoweza.

Bado naitafakari kauli ya RC, tunawasiliana na mapilot, ina pilots walikuwa wazima muda huo.

Inabaki palepale kuchelewa uokozi ndio kumesababisha vifo vya watu hawa.
 
Hii ajali kama ni pilot error ndo imeisha hiyo maskini mana na pilot mwenyewe kafariki hakuna kesi ila kama ni shida ya ndege basi byebye precision airways!

Hopefully tutajua what really happened baada ya uchunguzi!
 
Yaani maisha sijui hata yana maana gani, inauma na kuumiza sana!
Tunaweza kuilaumu serikali na watendaji wote wanaohusika na ukoaji kwa kutokuwajibika kwa namna moja au nyingine lakini ajali haina kinga, ajali haitangulizi taarifa kwamba itakuja...
Ndio ila pambana Sasa tuone,au timiza wajibu wako, tuseme kweli ilishindikana KWa mapenzi ya Mungu, mwinngine msimtwishe Mungu, bali ni uzembe ndo maana Mungu akaumba mwanadam KWa mfano wake, leo watu wanavutaje lindege wakati zana za kuvutia zipio, nayo tumlaum Mungu ebo
 
Hao ni askari na huduma ya kwanza wa nchi kavu,wataalamu wa hizo mambo za majini wako humo kwenye dege wanawaokoa wahanga wanawaleta nchi kavu kwa kutumia hizo boti maalum.
 
Hii ajali kama ni pilot error ndo imeisha hiyo maskini mana na pilot mwenyewe kafariki hakuna kesi ila kama ni shida ya ndege basi byebye precision airways!
Hopefully tutajua what really happened baada ya uchunguzi!
Shida ni hali ya hewa
 
Back
Top Bottom