Bulembo: Polepole ni Unyasi kaletwa CCM na kokoro, V8 ameijulia CCM, Bashiru alitoka CUF. Nataka Mdahalo na Polepole

Bulembo: Polepole ni Unyasi kaletwa CCM na kokoro, V8 ameijulia CCM, Bashiru alitoka CUF. Nataka Mdahalo na Polepole

Kwamba leo haya ni maneno ya bwana Abdallah Bulembo:

IMG_20211212_185614_232.jpg

Kuwa si muda mrefu uliopita akisema hivi:

Tupiganie katiba mpya wandugu kuondoa uhuni wa kiwango hiki katika nchi.

Ikumbukwe Polepole anaonya kwa hati ya dharura: "bado wapo wahuni wengi huko."
 
Katiba Mpya ndio itakuja kutuondoa kwenye huu mkwamo hasa ile rasimu ya Warioba, hata hawa vijana waliopo sasa wanaotegemea nafasi kwa kujipendekeza nao wakizeeka ndio watakuwa wazee wa hovyo kabisa.

Ni muhimu hili taifa liondokane na huu mfumo wa kurithishana madaraka ili kutengeneza kizazi kinachojiamini ambacho ujengaji wa hoja ndio itakuwa msingi wake.

Wazee waliotumia muda wao mwingi madarakani kuliibia taifa hawana njia nyingine zaidi ya kuhakikisha watoto wao wanashika hatamu ili kuwapa ulinzi wazee wao waliotenda jinai watapostaafu, wao wanachojua ni kujipendekeza na kufumbia macho maovu.
 
Mara baada ya Rais Samia kuingia madarakani kama Rais wa JMT tumeona watu ndani ya CCM wakiibuka na kutoa matamko ya kwenda kinyume na awamu ya sita. Wengi wao kwa sasa wamenyamaza na kuamua kusapoti serikali iliyopo huku wengine wakiwa kimya hawaeleweki. Aliyekuwa Katibu mwenezi ndo kabaki akiongea mengi yaliyo kinyume na serikali iliyopo kama vile naye ni mpinzani. Kuanzia chanjo ya Covid19 hadi ishu ya wamachinga kaonyesha upinzani mkubwa kuliko hata CHADEMA wenyewe.

Kama vile haitoshi akaamua kuwa na program yake ya Shule ya uongozi huko you tube ambapo ukimsikiliza bado masomo yake ni ya kupinga serikali iliyopo. Hivi majuzi naona baada ya kuona kuna dalili ya yeye "kufinywa" kaamua aje na press conference kutaka huruma za wananchi. Mimi ninamshauri ikiwa bado mapema huyu jamaa awatake radhi viongozi wote wa CCM na serikali kuanzia Rais hadi wengine ambao anajua kawakosea. Baada ya hilo zoezi akae kimya kabisa ikiwezekana astaafu siasa na kufanya mambo mengine.

Tuhuma za mambo maovu kuhusu Polepole ni nyingi sana kiasi kwamba inashangaza anapojitokeza hadharani na kuropoka. Polepole ni miongoni mwa watu wachache walioratibu uchaguzi mkuu wa mwaka jana ambao haukuwa huru... kwa uchaguzi ule kama ingekuwa nchi jirani kungetokea ghasia kubwa. Ni Mungu tu aliepusha.

Nimkumbushe kwamba serikali ya sasa hivi ni ya watu wanaojua siasa kiundani na sio siasa za awamu iliyopita zenye ubabe wa kijinga. Hawa viongozi wa sasa hivi ni wanasiasa waliobobea.. wanakupa kifinyo kimyakimya huku umma ukiwa hauelewi kinachoendelea. Yaani Polepole akija kushtuka kashachakazwa. Ukiangalia wanaotajwa kama maswahiba wa Polepole hawana mizizi yoyote ndani ya chama wala hawana uzoefu na siasa za CCM.

NDUGU YANGU POLEPOLE KAA KWA KUTULIA.
 
Na juhudi za kutoka hapa tulipo zisipofanyika mapema hali itakuwa mbaya huko mbele ya safari, fikiria hawa wazee wa sasa wenye nafuu waishe halafu PolePole, Nape, Msukuma & Co ndio wachukue hizo nafasi za Uzee😂
 
Wacha hizi fisi ziraruane

👇
"Najiuliza Mzee Philip Mangula yupo wapi kwa hili linaloendelea kwa Polepole? Kama aliweza kuwahoji makatibu wakuu Wazee Makamba na Kinana, ameshindwa nini kwa Polepole? Naamini, Polepole analo jambo na ukitaka kufanya jambo, usiseme nishikeni nisipigane, wewe pigana tu" - Bulembo
 
Mara baada ya Rais Samia kuingia madarakani kama Rais wa JMT tumeona watu ndani ya CCM wakiibuka na kutoa matamko ya kwenda kinyume na awamu ya sita. Wengi wao kwa sasa wamenyamaza na kuamua kusapoti serikali iliyopo huku wengine wakiwa kimya hawaeleweki. Aliyekuwa Katibu mwenezi ndo kabaki akiongea mengi yaliyo kinyume na serikali iliyopo kama vile naye ni mpinzani. Kuanzia chanjo ya Covid19 hadi ishu ya wamachinga kaonyesha upinzani mkubwa kuliko hata CHADEMA wenyewe.

Kama vile haitoshi akaamua kuwa na program yake ya Shule ya uongozi huko you tube ambapo ukimsikiliza bado masomo yake ni ya kupinga serikali iliyopo. Hivi majuzi naona baada ya kuona kuna dalili ya yeye "kufinywa" kaamua aje na press conference kutaka huruma za wananchi. Mimi ninamshauri ikiwa bado mapema huyu jamaa awatake radhi viongozi wote wa CCM na serikali kuanzia Rais hadi wengine ambao anajua kawakosea. Baada ya hilo zoezi akae kimya kabisa ikiwezekana astaafu siasa na kufanya mambo mengine.

Tuhuma za mambo maovu kuhusu Polepole ni nyingi sana kiasi kwamba inashangaza anapojitokeza hadharani na kuropoka. Polepole ni miongoni mwa watu wachache walioratibu uchaguzi mkuu wa mwaka jana ambao haukuwa huru... kwa uchaguzi ule kama ingekuwa nchi jirani kungetokea ghasia kubwa. Ni Mungu tu aliepusha.

Nimkumbushe kwamba serikali ya sasa hivi ni ya watu wanaojua siasa kiundani na sio siasa za awamu iliyopita zenye ubabe wa kijinga. Hawa viongozi wa sasa hivi ni wanasiasa waliobobea.. wanakupa kifinyo kimyakimya huku umma ukiwa hauelewi kinachoendelea. Yaani Polepole akija kushtuka kashachakazwa. Ukiangalia wanaotajwa kama maswahiba wa Polepole hawana mizizi yoyote ndani ya chama wala hawana uzoefu na siasa za CCM.

NDUGU YANGU POLEPOLE KAA KWA KUTULIA.
Wahuni mna mikwara! HPP sisi tuko nyuma yako usikate tamaa ulitutetea sana sisi wamachinga.
 
Tuko kipindi ambacho Wazee wengi siyo wasuluhishi wa Amani tena bali wanatafuta Ugali na ugali wa watoto wao,ama wao au Watoto wao wapewe nafasi za Uongozi 😂😂😂
lisi yao ni kama hii

1. Mwinyi
2. Philip
3. Msekwa
4. Jk
5. Mkapa R.I.H
6. Makinda
7. Makamba
etc
 
Na juhudi za kutoka hapa tulipo zisipofanyika mapema hali itakuwa mbaya huko mbele ya safari, fikiria hawa wazee wa sasa wenye nafuu waishe halafu PolePole, Nape, Msukuma & Co ndio wachukue hizo nafasi za Uzee😂
😅😅😅😅😅
 
Maneno ya Bulembo!

Polepole ni unyasi mkavu ni mdogo sana Mangula ashughulike naye.

Bulembo anataka mdahalo na Polepole na yuko tayari kulipia ukumbi.

Bashiru wa CUF hakutakiwa kuwa pale maana hajakulia katika chama cha mapinduzi! Sasa najiuliza kumbe chama cha mapinduzi ili uwe kwenye kundi la mwenye chama unatakiwa uwe umekulia humo!

Inaonekana pia suala la kinana na makamba ni kubwa hawa wazee ndo CCM yenyewe!

Paramagamba Kabudi aliharibu mahusiano ya kimataifa na Rais Samia sio sawa na Magufuli!

Hayo ni mambo ya Bulembo! Mmoja ya wenye COmbi.

Ombi! Vijana ambao Baba zenu sio wenye chama mwisho wenu 2025!

======

View attachment 2041643
Sitaki kumjibu Polepole, kwenye CCM ni mchanga, ni sawa sawa na mtoto wa darasa la kwanza anajibiwa na wa chuo kikuu. Polepole ni sawa na unyasi mkavu. Siku Polepole anaingia kwenye chama kujitangaza, alipewa nguo za CCM na Nape Nnauye- Abdallah Bulembo

Najiuliza Mzee Philip Mangula yupo wapi kwa hili linaloendelea kwa Polepole? Kama aliweza kuwahoji makatibu wakuu Wazee Makamba na Kinana, ameshindwa nini kwa Polepole? Naamini, Polepole analo jambo na ukitaka kufanya jambo, usiseme nishikeni nisipigane, wewe pigana tu- Bulembo

Polepole hawezi kuwa mzuri kwa Magufuli kuliko mimi. Nimekaa na Magufuli siku 90 kwenye kampeni za uchaguzi. Nimebadilishana naye nguo wakati wa kampeni. Polepole anampenda Magufuli kwa kuwa alimpa zawadi ya nafasi- Abdallah Bulembo

Lengo la Polepole ni kumkatisha tamaa Rais Samia. Hawezi ni mdogo sana. Rais Samia aachwe, namjua anaweza. Nimekaa naye namjua. Aachwe afanye kazi, lakini wakija vijana wenzenu na shule ya uongozi, huwezi kuifanya ukiwa mbunge, subiri umalize ubunge. Hivi unasema lipi?- Bulembo

Magufuli alituwekea Profesa Kabudi mambo ya nje akavuruga mahusiano yote ya kimataifa. Mama Samia kaingia amemteua Balozi Liberata Mulamula, leo Mama Samia amehutubia mikutano huko UN. Mambo ya kimataifa nchi zinaingiliana- Abdallah Bulembo

"Tuliwaheshimu Polepole na mwenzake kutoka CUF anaitwa Bashiru kwa sababu tu aliyewateuwa tulikuwa tunamheshimu, Magufuli alimteuwa Bashiru Kutoka Cuf kuja kutuhoji kuhusu mali za chama nikamgomea kunihoji nikamwambia yeye sio mwana CCM" Abdallah Bulembo

ZAIDI SOMA;

Dar es Salaam. Mwenyekiti mstaafu wa jumuiya ya wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemtaka mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole amwache Rais Samia Suluhu Hassan atekeleze majukumu yake.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Desemba 12,2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari akimjibu Polepole kuhusu lawama alizotoa dhidi ya Samia ambaye ni mwenyekiti wa CCM.

Bulembo amemuomba makamu mwenyekiti wa chama hicho bara, Philip Mangula kumuhoji Polepole kama alivyowahoji makatibu wakuu wa zamani, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba ambao sauti zao zilivuja wakikosoa viongozi na mwenendo wa chama hicho tawala, akitaka Polepole naye aitwe kamati ya maadili.

Huku akisisitiza kuwa anakemea suala hilo kama mwanachama wa kawaida na hajatumwa na mtu amesema, “kama Polepole anataka kutoka atoke atuachie CCM maana ana wenzake wanaomshawishi kuanzisha chama chao, asitapetape na kuongea mambo ambayo hayaeleweki.”

"Hawa kina Polepole waliojificha hawatusumbui ndani ya CCM kwa mujibu wa kanuni na katiba ya chama kama mwanachama anaenda tofauti kuna onyo, kufungiwa au kufukuzwa uanachama.”

Bulembo amesema anamfahamu Polepole tangu mwaka 2012 alipoteuliwa na rais mstaafu Jakaya Kikwete kuwa mjumbe wa iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba.

"Siyo kwamba ndani ya CCM tulifurahia uteuzi wake wa ukatibu mwenezi Taifa bali tuliheshimu mamlaka ya aliyekuwa mwenyekiti Taifa hayati John Magufuli bali. Hamjali Samia na kimsingi hawezi kumpangia rais cha kufanya, yeye ni nani,”amesema Bulembo
View attachment 2041667
Polepole mtu mdogo Sana,inatakiwa atiwe adabu haraka,anataka kuivuruga serikali
 
Hii nchi inahitaji mabadiliko makubwa sana. Hii nchi inatakiwa ipate wenye ujasiri wa kusema pale ambapo Mambo yanaharibika na sio kuishi kinafiki. Kama prof kabudi alikuwa anaharibu mbona miaka yote walikaa kimya au ndio walikuwa mezani pamoja kula keki ya taifa. Ni basi tu wanashindwa kusema hata huyo aliyetutoka aliharibu sana tu coz kabudi hakuyafanya hayo bila support ya huyo aliyetutoka
 
James Lembeli aliwahi kusema kuwa sio kila upepo ukivuma unaweza kufunua uchi wa kuku. Alisema kuna aina ya upepo mahususi kwa ajili ya kufunua uchi wa kuku. Nadhani kwa sasa kwa hali ilivyo na fukuto linaloendelea ndani ya CCM huenda haya ndo majira ya ako ka upepo kakumfunua kuku uchi hatimaye tuweze kuuona.
 
"Tuliwaheshimu Polepole na mwenzake kutoka CUF anaitwa Bashiru kwa sababu tu aliyewateuwa tulikuwa tunamheshimu, Magufuli alimteuwa Bashiru Kutoka Cuf kuja kutuhoji kuhusu mali za chama nikamgomea kunihoji nikamwambia yeye sio mwana CCM" Abdallah Bulembo

Nje ya mada H: hivi Binti yake na Bulembo bado ni mbunge wa vitu maalum?
 
Hatari sana, wahuni kumbe wako wengi wanazidi kujitokeza!! Yajayo yanasikitisha!
 
"Tuliwaheshimu Polepole na mwenzake kutoka CUF anaitwa Bashiru kwa sababu tu aliyewateuwa tulikuwa tunamheshimu, Magufuli alimteuwa Bashiru Kutoka Cuf kuja kutuhoji kuhusu mali za chama nikamgomea kunihoji nikamwambia yeye sio mwana CCM" Abdallah Bulembo

Nje ya mada
Yaani hilo mzee jinga kabisa! Jitu limeiba mali za chama miaka na miaka!
 
Chama kipya kitapata wanachama wengi sana. Sisi wamachinga tunakisubiri kwa hamu kubwa maana kitakuwa mfariji wetu.
 
List ya Wahuni hadi sasa hivi ambao Jiwe likewapata gizani:
Nape,
Bulembo,
.........
..........
 
Back
Top Bottom