Uchaguzi 2020 Bulembo: Taratibu za CCM haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli

Uchaguzi 2020 Bulembo: Taratibu za CCM haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
downloadfile-360.jpg


Aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema taratibu haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli.

“Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana CCM, Rais anatakiwa awe katika vipi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?,” amesema Bulembo
“Taratibu haziruhusu Mwanachama mwingine kuchukua fomu zaidi ya Magufuli kwa mujibu wa sheria kama wewe ni Mwana-CCM, Rais anatakiwa awe katika vipindi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu?, unajadiliwa kikao gani?”-ABDALLAH BULEMBO
(via Clouds360 ya Clouds Tv)

Bulembo amesema hataki kugombea licha ya kwamba anajua atashinda na kwamba haiwezekani nyumba nzima wawe wabunge.

“Nataka niondoke salama, mtoto wangu Halima yupo kwenye jimbo, mke wangu naye yupo kwenye jimbo anagombea Viti maalum, haiwezekani nyumba yote kuwa wabunge haileti picha nzuri,” amesema Bulembo.
 
Huyu mgombea ni miongoni mwa wanachama wa ccm ambao ni mbishi na aliapa kugombea urais wa JMT akimpinga rais anaemaliza kipindi chake cha miaka mitano ya awali.

CCM ina tamaduni yake, mgombea wake kutoshindanishwa kwa muda wa miaka kumi, akimaliza ndipo wengine hugombea hiyo nafasi.

Lakini Membe alipinga na akaahidi kuuvunja utamaduni huo ,kulikoni yupo kimya? na muda unayoyoma wa kutafuta wadhamini nchini? au kakubali yaishe baada ya kichwa kuelekezwa kibla?

Je? anao uwezo wa kupambana na ccm nje ya ccm? anaejua habari za huyu gwiji na kachero mbobezi atujuze tafadhali
 
Bulembo ametoa somo zuri
Kwamba CCM anyetakiwa kuchukua fomu ya kugombea urais kisheria ni mmoja tu?

Bahati mbaya sana sheria za nchi, katiba na kanuni za CCM hazisemi hivyo!!!!. Sasa kafundisha somo gani zuri?

Laiti angesema kuwa kwa mazoea yetu CCM mgombea urais ni mmoja na fomu imechapishwa moja tuuuuuu.
 
He! tena kwa hiyo mnaogopa nini wakati Mkuu anapendwa na wanaccm, ruhusuni watu wachukue form ili awaonyeshe kwamba ana pendwa kwa kuwagalagaza kabla hajakutana na upepo wa nje, hii pia inasaidia kumuongezea hamasa kuelekea uchaguzi mnao shauri hii mnampoteza sana Mgombea wenu
 
CCM adabu buana!! Na ndiyo Maana kuna watu kule! Kwingine unalazimika kupaisha sifa za Chama ili ruzuku ziwe nyingi kumnufaisha mmoja?

Hovyo kabisa
 
Huyu alikuwa mwenyekiti wa chama lakini taratibu hata hazijui sheria haimruhusu mtu kugombea zaidi ya vipindi viwili hayo mengine wanafanya kama mazoea
 
Aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema taratibu haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli.

“Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana CCM, Rais anatakiwa awe katika vipi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?,” amesema Bulembo
Duuh. . . . . . democrasia 2020
 
Back
Top Bottom