Uchaguzi 2020 Bulembo: Taratibu za CCM haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli

Uchaguzi 2020 Bulembo: Taratibu za CCM haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli

Tena Bashiru aelewe hakuna Mwenye hati miliki na Chama ,so kama kweli anakimbia ofisi huko ni kukihabisha Chama ,magu si anapendwa na wanaccm ?wape watu form na ni haki yao kuchukua hata Mimi ningekua mwanachama ningechukua ,haya ya kusema kama ya bulembo eti anachukua magu form tu ni kutojielewa,maana magu Chama amekikuta,Bashiru Chama nae amekikuta hata hao wakina polepole na wataondoka watakiacha maana si Mali binafsi ya mtu.
Ujumbe umefika mkuu labda watabadilika
 
Kwamba CCM anyetakiwa kuchukua fomu ya kugombea urais kisheria ni mmoja tu?

Bahati mbaya sana sheria za nchi, katiba na kanuni za CCM hazisemi hivyo!!!!. Sasa kafundisha somo gani zuri?

Laiti angesema kuwa kwa mazoea yetu CCM mgombea urais ni mmoja na fomu imechapishwa moja tuuuuuu.
Sio hivyo mkuu
Tuombe uhai 2025 uone watakavyochukua wengi
 
downloadfile-360.jpg

Aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema taratibu haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli.

“Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana CCM, Rais anatakiwa awe katika vipi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?,” amesema Bulembo

Bulembo amesema hataki kugombea licha ya kwamba anajua atashinda na kwamba haiwezekani nyumba nzima wawe wabunge.

“Nataka niondoke salama, mtoto wangu Halima yupo kwenye jimbo, mke wangu naye yupo kwenye jimbo anagombea Viti maalum, haiwezekani nyumba yote kuwa wabunge haileti picha nzuri,” amesema Bulembo.
Katiba ya chama inasemaje nayo
 
Logic hawana,mgombeaji ni Mwenyekiti ambae ni Raisi ndie mtetezi huyo huyo wa kiti cha uraisi , angepitishwa bila drama kwa kuwa CCM hairuhusu kumshindanisha sitting president na mtia nia yeyote.

Kwa hiyo hakuna sababu za msingi kupitia mchakato wa kugombea uraisi kwa tiketi ya CCM kwa sababu HAKUNA WAGOMBEA.

Kwa hiyo uteuzi wa Raisi Magufuli hauitaji kupitia CC,NEC na mkutano mkuu kwa kuwa hakuna jambo la kujadiri wala kupigia kura. Wangewahurumia wananchi kutumia pesa za kutia nia iende mfuko wa afya.

Lakini kama bado wanadai utaratibu wa CC,NEC,NC.kuwa una muhimu kwa Raisi Magufuli ,utakuwa ni batili kwa kuwa endapo mkutano mkuu ungetilia shaka uwezo wa Raisi Magufuli itabidi watia nia wapya wachukue form na kusaka wadhamini nchi nzima katika week mbili,harafu ipitie CC,NEC na mkutano mkuu NC.

Utaratibu wa one man show wa CCM ni kizingiti endapo yule mtetezi akikumbwa na matatizo hawana second runner.
Hujui kwamba Kuna kura za ndiyo na hapana? Wajumbe wakipiga hapana mchakato utaanza upya. Kumbuka hata chadema walimpa Sumaye ugombea pekee kule pwani lakini akapigiwa hapana nyiingi mchakato ukaanza upya.
 
Wakianza upya muda si rafiki,ni uzembe mkubwa kwa chama kikubwa na kikongwe.
 
Yaani chama kongwe mmeshindwa hata kuweka wagombea wa kupanga ili kuzuga watu.
Chama kongwe haliwezi kufanya Mambo ya kuzuga, kinafanya Mambo ambayo ni halisi, ya kuzuga fanyeni nyie watoto chadema muwazuge hao wasiojielewa.
 
Ni kautaratibu tu
Hakana madhara yeyote kwenye demokrasia
Natamani kila kitu nchi hii kingeendeshwa na kautaratibu badala ya sheria na regulations zake.
Unajua mtu yeyote awaye akitaka kufanya ya kwake anaanzisha kautaratibu nje ya mifumo rasmi. Ni sdhida sana kwa watu wa kawaida.
 
downloadfile-360.jpg

Aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema taratibu haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli.

“Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana CCM, Rais anatakiwa awe katika vipi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?,” amesema Bulembo

Bulembo amesema hataki kugombea licha ya kwamba anajua atashinda na kwamba haiwezekani nyumba nzima wawe wabunge.

“Nataka niondoke salama, mtoto wangu Halima yupo kwenye jimbo, mke wangu naye yupo kwenye jimbo anagombea Viti maalum, haiwezekani nyumba yote kuwa wabunge haileti picha nzuri,” amesema Bulembo.
Chama kinaendeshwa kwa taratibu sio katiba? Wekeni huo uraratibu kwenye katiba
 
Back
Top Bottom