Uchaguzi 2020 Bulembo: Taratibu za CCM haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli

Uchaguzi 2020 Bulembo: Taratibu za CCM haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli

downloadfile-360.jpg

Aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema taratibu haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli.

“Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana CCM, Rais anatakiwa awe katika vipi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?,” amesema Bulembo

Bulembo amesema hataki kugombea licha ya kwamba anajua atashinda na kwamba haiwezekani nyumba nzima wawe wabunge.

“Nataka niondoke salama, mtoto wangu Halima yupo kwenye jimbo, mke wangu naye yupo kwenye jimbo anagombea Viti maalum, haiwezekani nyumba yote kuwa wabunge haileti picha nzuri,” amesema Bulembo.
ingekuwa ni Chadema ndiyo wanafanya hivi MATAGA wote wangejitundika kwa hasira!
 
Kama ndo hivyo basi yesu angesubiri kuchukua fomu ya Nec ya uraisi kabisa na hasingechukua ya fomu ya chama
 
Katiba ya chama ndiyo yenye kusimamia haki ya kuwa mwanachama ama kiongozi ndani ya chama. Kanuni na taratibu za kuwa kiongozi huwekwa kupitia vifungu vyake. Kama katiba inatoa fursa hiyo, sasa nini kitakuwa chanzo cha kuogopa Mwenyekiti kushindanishwa na watia nia wengine?

Tumeshuhudia sifa luluki zikimwagwa juu yake ikiwa ndiye kama kiongozi wa kipekee kuwahi kutokea hapa nchini. Je! Hatuoni hii itakuwa ndiyo kete yake muhimu ktk kuwagalagaza washindani wenzake ktk kinyang'anyiro ndani ya chama na hatimaye ktk nafasi ya uraisi?
 
Huyu mgombea ni miongoni mwa wanachama wa ccm ambao ni mbishi na aliapa kugombea urais wa JMT akimpinga rais anaemaliza kipindi chake cha miaka mitano ya awali.

CCM ina tamaduni yake, mgombea wake kutoshindanishwa kwa muda wa miaka kumi, akimaliza ndipo wengine hugombea hiyo nafasi.

Lakini Membe alipinga na akaahidi kuuvunja utamaduni huo ,kulikoni yupo kimya? na muda unayoyoma wa kutafuta wadhamini nchini? au kakubali yaishe baada ya kichwa kuelekezwa kibla?

Je? anao uwezo wa kupambana na ccm nje ya ccm? anaejua habari za huyu gwiji na kachero mbobezi atujuze tafadhali
SUBIRI NGOMA MUTAICHEZA SOON... Ila hamtajua inapigwa wapi!

👊👊👊
 
Alikuwa Kiongozi wa chama Gani?Nyie Makarai mbona mnashindwa kuelewa
Alifukuzwa kwenye kikao kipi? Unamfukuzaje mtu kwa maneno tu bila ya kumkabidhi barua?

Membe hakuwa mwana chama kama ulivyo wewe huko kwenu mbwinde, Membe alikuwa ni kiongozi wa ngazi za juu ndani ya ccm. Hawezi kufukuzwa kama utakavyo fukuzwa wewe.
 
downloadfile-360.jpg

Aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema taratibu haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli.

“Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana CCM, Rais anatakiwa awe katika vipi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?,” amesema Bulembo

Bulembo amesema hataki kugombea licha ya kwamba anajua atashinda na kwamba haiwezekani nyumba nzima wawe wabunge.

“Nataka niondoke salama, mtoto wangu Halima yupo kwenye jimbo, mke wangu naye yupo kwenye jimbo anagombea Viti maalum, haiwezekani nyumba yote kuwa wabunge haileti picha nzuri,” amesema Bulembo.
Ukichunguza sana utakuta uyu mzee ni hata shule hakuwahi kwenda
 
Atachukua form tu ingawa nasikia katibu anakimbia ofisi kama wale ma DED wanavyo kimbiaga wagombea wa cdm wakati wa kurudisha form kwenye chaguzi za marudio
Tena Bashiru aelewe hakuna Mwenye hati miliki na Chama ,so kama kweli anakimbia ofisi huko ni kukihabisha Chama ,magu si anapendwa na wanaccm ?wape watu form na ni haki yao kuchukua hata Mimi ningekua mwanachama ningechukua ,haya ya kusema kama ya bulembo eti anachukua magu form tu ni kutojielewa,maana magu Chama amekikuta,Bashiru Chama nae amekikuta hata hao wakina polepole na wataondoka watakiacha maana si Mali binafsi ya mtu.
 
Back
Top Bottom